Masikitiko makubwa Ziara yangu ya siku 2 Hifadhi ya Serengeri

Masikitiko makubwa Ziara yangu ya siku 2 Hifadhi ya Serengeri

Nikiwa ndani ya Hifadhi nilijaribu kuuliza baadhi ya wafanyakazi kulikoni wengi walinijibu siasa imekuwa kubwa sana kiasi hata wataalam wanadarauliwa.

Kuna mambo mengi yanatia woga na kuleta masikitiko sana. Sijui nini kinaendelea kwenye nchi yetu. Ngumu kujua na kusema
 
Mkuu Mgongo

Kipindi cha Hando Serengeti ilikuwa the best National Park duniani katika kusimamia Management Plan...

Viongozi wameingilia na kuweka Maslahi yao huko ukigangamala sheria za uhifadhi unafukuzwa mbali..Vilima vyote vimevamiwa ....kuna wakati unasikia aibu mbele ya wageni maswali wanayouliza baada ya kushuhudia ujenzi holela...Hata hiyo 4seasons ni uharibifu tu haipo kwenye Management Plan ya Senapa


Ngongo
 
Ukitaka kuishi kwa amani usiyachukulie mambo too personal.

Be serious only on you and yourself!
 
Hizo hotel Ni machaka ya majingili wanaotuibia rasilimali wanyama poro yetu Mana huwezi ukaiba ukachuna ngozi ya kenge usiku huo huo na kusafirisha ssa wanajenga mahoteli ili watufilisi mazima
 
Heshima sana wanajamvi,

Nimekuwa na utaratibu wa kutembelea hifadhi zetu za wanyama kwa muda mrefu sasa labda huu ni mwaka wa 10 au zaidi.

Nimetembelea hifadhi ya Serengeti zaidi ya mara nne au tano,mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2016.

Ukweli mchungu sisi waafrika sijui tuna laana gani ?.

Kumekuwa na utaratibu wa ajabu ajabu wa majenzi ya Camps sites nyingi hadi nature imeanza kuondoka au imeshaondoka.Usiku taa zinawaka pengine ungefikiri upo Washington au majiji mengine makubwa.Camp Site nyingi na Lodges zimejengwa hovyo hovyo kiasi ungefikri labda kuna mpango mahsusi wa kuiua Serengeti.

Ikiwa hata kusimamia nature tu inatushinda nini tutaweza !.

Kama hali ya majenzi holela holela itaachiwa iendelee ndani ya miaka mitano au chini ya hapo Serengeti itakuwa haina tofauti na majiji tunayoyaona leo.

Hakika nimesikitika na kushangazwa jinsi tunavyoshindwa kuilinda na kuisimamia Serengeti pengine na hifadhi nyingine.

Ngongo kwasasa Kilima Tembo.
Hayo mambo ya mipango ya hovyo sisi Tanzania ndio magwiji dunia nzima, wacha nisiende huko manake naweza kuchoma moto camp za watu.
 
halafu baadae tutalalamika wazungu na waarabu wametufanyia ukoloni na kuchukua rasilimali zetu

Watu weusi wamelaanika
 
Back
Top Bottom