KERO Masikitiko yangu Kilwa road na Chang'ombe road inakwenda kuwa na foleni kubwa sana

KERO Masikitiko yangu Kilwa road na Chang'ombe road inakwenda kuwa na foleni kubwa sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sasa hivi kuna foleni ya hovyo sana inayochangiwa na ukanjanja wamipango
Upigaji mkubwa uko kwenye procurement. Mataa hayo ni dili la wahuni wachache.
 
Mhhh tutulie na tuwe wapoleee.
Saiv hamna haja ya polisi wa usalama barabarani kuwepo ni mwendo wa taa tuu.
Tuvumiliane na tuache vilio

Barabara inatakiwa iwe hivyo.
Yani
SHeria
Michoro
Alama
Taa
 
Ikishaanza mwendokasi dala dala zitapungua ... Foleni inasababishwa na vituo vya daladala ambavyo vipo barabarani mfano pale kwa azizi ally kipo karibu na round about kwa pande zote mbili kwenda mjini na kwenda Mbagala .. wala tusisingizie taa za barabarani
 
Uzi mzuri
Leo unaishi.
Sie watumiaji wa hii njia tunalilijua hili ila kwakuwa pia sisi ni watu wa lawama basi acha tunyooshwe maana no way out. Akikaa polisi ni lawana taa lawama matututa lawama
Matuta kulingana na wataalam wa barabara yana idadi kulingana na umbali.

Mkuu tuvumilie saivi tutanyooshwa na hayo mataa.toka ijumaa mpaka leo dah tushaanza kuona kero haswa
 
Ikishaanza mwendokasi dala dala zitapungua ... Foleni inasababishwa na vituo vya daladala ambavyo vipo barabarani mfano pale kwa azizi ally kipo karibu na round about kwa pande zote mbili kwenda mjini na kwenda Mbagala .. wala tusisingizie taa za barabarani
Siyo kweli! Kwanini baada ya taa ndiyo kuwe hivyo! Hapo kabla madaladala si yalikuwapo
 
Vipimo gani! Naposema mapana nimetumia kiswahili chepesi ili na wewe uelewe! Au unataka niandike kwa kimombo
Usiwe na makasiriko mkuu.
Kulingana na tanroad na tarura issue ya kuweka matuta wana vipimo vya umbal toka tuta moja hadi jingine so kama havijafikia hawawez weka maana pia wamiliki wa magar hulalamika matuta na rasta zikizid na huwalaumu kwa vitendo vyao vya kuongeza matuta na kushindwa kufuata kanuni zao.

Ndo maana unaweza kuta eneo la kivuko cha wanafunzi/watembea kwa miguu hamna tuta zaid ya alama za punda milia peke yake.
 
Siyo kweli! Kwanini baada ya taa ndiyo kuwe hivyo! Hapo kabla madaladala si yalikuwapo
Kwahio KILWA ROAD foleni imeanza baada ya taa? Pale jkt mgulani kila asubuhi na jioni gari zinashonana vibaya sana kabla ya taa. Afadhali kusubiria taa kuliko ile vurugu.
Pale chuo cha polisi jioni Kuba foleni hadi mivinjeni,kisa ni daladala zinapaki barabarani.
Pale central police to sgr station jioni kuna foleni balaa kisa ujenzi usioeleweka zaidi ya miezi mitatu sasa. Halafu foleni hizi unasingizia taa. Acha taa zifanye kazi madereva hamuwezi kujiongoza wote akili kama bodaboda.
 
Centro njia moja imefungwa hilo liko wazi!
Teknolojia hutumika kuondoa tatizo
 
Sijui hata cha kusema!

Lakini masikitiko yangu matokeo ya ufungaji wa taa za barabari Kilwa road na Chang'ombe road yanaenda kuibua kero kubwa ya msongamano wa magari kuliko ilivyo hata hivi sasa.

Lengo la taa limelenga kuvusha watembea kwa miguu salama lakini kwa upande wa pili linakwenda kuzalisha tatizo la foleni ya kujitakia!

Nashauri badala ya kuweka taa nyingi namna ile! Wangeweka taa sehemu chache ambazo ni muhimu tu na huko kwingine wakaweka matuta standard mapana ili kuruhusu Traffic flow.

Mbali na msongamano itakuja kulazimisha ongezeko la askari kusimama kwenye mataa ili kuruhusu magari ambao wangefanya kazi nyingine.

Siamini kama kweli hawa wanaofunga hawajui kwamba taa kila hatua 100 zinaongeza foleni unless huu mradi ulikuwa na faida kwa baadhi ya watu kupiga!
 
Kumbuka wavuka kwa miguu nao wanahaki tena ya msingi sana, hao na ni watoto, baba na mama za watu, tusiangalie upande mmoja tu, ni vyema kubalance kila mtu apate haki yake.
 
Siyo kweli! Kwanini baada ya taa ndiyo kuwe hivyo! Hapo kabla madaladala si yalikuwapo
Hizo sehemu nilizokwambia hata kabla ya taa kunakuwa na foleni kubwa sana unaweza poteza saa nzima .. kubali kataa vituo vya daladala vipo barabarani mno
 
Kumbuka wavuka kwa miguu nao wanahaki tena ya msingi sana, hao na ni watoto, baba na mama za watu, tusiangalie upande mmoja tu, ni vyema kubalance kila mtu apate haki yake.
Kwani wakivuka juu ya tuta pana lenye zebra kuna shida gan?
 
Sasa hivi kuna foleni ya hovyo sana inayochangiwa na ukanjanja wamipango
Kuna watu akili zao zina mentality za ukijijini sana hadi leo huona mataa ni ni kipimo cha maendeleo au fahari
 
Back
Top Bottom