KERO Masikitiko yangu Kilwa road na Chang'ombe road inakwenda kuwa na foleni kubwa sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni kweli hatukatai maendeleo ila huyu aliyebuni huu mradi na kupendekeza sijui aliwaza nini? Umeshapita hiki kipande kuanzia ulipokuwa mzunguko wa BP kuja stesheni? Kwanza njia ni moja tu mpaka unafika posta ya zamani na kibaya sasa hizo taa na zinavyoongoza unakuta ya mbele nyekundu ya nyuma yake inawaka kijani. Najiuliza gari zitatembea kweli? na je gari ikipata hitilafu zingine zitapita wapi? Huku mjini hakukutakiwa kuwa na njia nyembamba kwani mwendi kasi wangeunga ikapita kamata hadi kariakoo ikaunga na za morogoro road kulikuwa na shida gani mpaka kuja haribu mji hivi? sasa hivi mjini ni foleni mno
 
hapo watu wamekula percent kwenye tenda ya taa, hii nchi sio kabisa, ujanja ujanja kila seehemu
 
Ni chaos, mkuu.. halafu hizi barabara za mwendo kasi vituo kila vaada ya mita 200! enzi hizi za magonjwa ya NCDs na watu wavivu wavivu mnaweka vituo kila baada ya mita 100 au 200? vituo viwekwe sehemu za muhimu tu ili watu watembee wafanye mazoezi, Barabara zitengenezwe vizuri na zijumuishe pedestrian lane ili watu watembee wafanye mazoezi

Hii Kilwa road baada ya taa kuwashwa imekua tabu haswa leo halafu kutoka bandarini kuingia kilwa road wameweka njia moja sijui hawa watu wanatumia akili za wapi.. Ukifika hapo njia ya kuingia sokoine drive kuna njia moja mpaka stesheni kuelekea kule St joseph... Kama hatuna maeneo ya kutosha tunalazimisha mwendo kasi kupita kila mahali ili iweje? Kwa mfano kuna ulazima gani kupitisha mwendokasi Azikiwe kama kuna kituo cha posta ya zamani? Pale Akiba/CBE sijui wanafanya kituko gani pale maana hamna eneo kabisa inawezekana napo kukawa na njia moja tu!
 
Duu ! Foleni balaa ! Siku za nyuma nilikuwa nikitoka Temeke sipiti taa za Changómbe napitia JKT then Kilwa Road Posta nilikuwa nafika chap ! Lakini leo ! Duu imenichukua karibu saa nzima ! Sipiti tena Kilwa Road taa zinachelewsha kinoma !
 
Duu ! Foleni balaa ! Siku za nyuma nilikuwa nikitoka Temeke sipiti taa za Changómbe napitia JKT then Kilwa Road Posta nilikuwa nafika chap ! Lakini leo ! Duu imenichukua karibu saa nzima ! Sipiti tena Kilwa Road taa zinachelewsha kinoma !
Hayo ni mahesabu ya kawaida tu siamini walioidhinisha hilo kama wako sawa
 
Haihitaji elimu kubwa kulitambua hili ila kilichofanyika barabara ile ni upumbavu wa hali ya juu. Uwepo wa taa za barabarani hatulipingi ila sio utitiri wa kiasi kile
 
Haihitaji elimu kubwa kulitambua hili ila kilichofanyika barabara ile ni upumbavu wa hali ya juu. Uwepo wa taa za barabarani hatulipingi ila sio utitiri wa kiasi kile
Kweli kabisa
 
Foleni itakwisha mwendokasi ikianza kwani daladala zote zitaondoka.v
 
hakuna taasisi yenye watendaji mizigo kama tanroads aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…