Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

Hapo unakosea kusema kutooa au kutokuolewa sio kosa. Ni kosa.

Ni sawa na kusema kutengeneza silaha na anayezitengeneza sio shida shida ni matumizi ya hiyo silaha. Sasa hiyo silaha isingetengezwa madhara ya silaha yangekuwapo?

So kimsingi nataka ufahamu jambo moja, kuna maisha nje ya mfumo wa Ndoa ambayo ndio haya yaliyotapakaa sasa na kuna maisha yaliyo ndani ya mfumo wa ndoa.

Ukisema sio kosa kuishi nje ya ndoa jua unahalalisha na kusema sio kosa kuwa single mother, sio kosa kulala na wanaume wengi, sio kosa kutembea na kuwapa mimba wanafunzi, sio kosa kuwaharibia mabinti wadogo direction kwa kulala nao kisha kuwatema na kwenda kutafuta binti mpya wa kumharibu, unasema ni sawa kutoa mimba, unasema ni sawa maisha ya kufanya kazi kwa bidii halafu pesa inaishia kununua makahaba na kulewa vitu ambavyo baadae ndio chanzo kikuu cha maradhi ya kuambikizwa na yasiyo ya kuambukiza mwilini.

Kwa kifupi unaposema ndoa sio necessary kwenye maisha ya kijana au binti maana yake unafungua mjadala mpya kabisa wa namna ya kuishi kwenye ulimwengu nje ya kanuni tulizowekewa za kimaadili. Hauwezi ishi nje ya mfumo wa ndoa halafu ukawa mstaarabu na kuwa comfortable at the same time. Pia mfumo wa maisha nje ya ndoa ndio huo huo mfumo unawaletea shida sana waliopo ndani ya Ndoa kushindwa kutulia na kufanya maisha yao kwa umakini na kuendelea kuimarisha jamii.

So tengua kauli yako kuwa ndoa sio lazima, cha msingi fanya kwenda kujielimisha kwann kuna ndoa na nini kinatokea kusopokuwa na ndoa.
 
Kweli kabisa na ndio maana wanalalamika kwa nini wazazi, ndugu na jamii inawauliza, kama hilo jambo la kutokuwa na ndoa si kosa la kimaadili kwa nini nafsi yako inakuuma kama huna kosa au hatia na wengine wamethibitisha kuwa kuwa wanaumia kuulizwa.

Ni bora mtu useme bado hujajipanga lakini sio eti sio lazima kuoa na ili hali unaonekana unaingiza wanawake tofauti tofauti kila kukicha.

Mimi nilipofika umri wa kuanzia miaka 28 wazazi na ndugu wa jirani walinishauri sasa na vizuri upate ndoa nikajipanda nilipofika miaka 30 nikaoa.
 
Nakutana nazo sana kwenye matukio ya kijamii,kiukweli niliplan kuoa 2014 ila niiyekuwa nae alimpata mwengine alivyo enda kusoma nikaplan tena 2017 still demu akarudi kwa ex-wake. Yaani mpaka sasa sijui nitaoa lini kwani hawa ambao ninao kutana nao wote vichomi, unaweza ukasema wanatumia template moja ya ujinga,kuendesha mahusiano.

Kuna dem mmoja tu alikuwa rafiki yangu kipindi nipo O-Level na Advance, yule nahisi ndiye kama alikuwa mke wangu. Sema ndio hivyo uoga plus udomo zege kipindi hiko,baadae tukawa tunasoma sehemu tofauti then sasa hivi kaolewa.

Ila swala la kuoa nimemuachia Mungu, sometimes unataka kuforce ila vichomi unavyo kutana navyo bora ubaki single.
 
Kuoa ni heshima full stop

Kuona kwako walevi wameoa haimaanishi kuoa siyo kitu cha maana na heshima.
Tusipingane na ukweli ,ili tujue mwanaume umekamilika kuoa hakukwepeki familia ni nguzo muhimu sana msichokijua vijana hakuna raha Kama umetoka kazin umerud na kimfuko cha mazaga madogo wanakimbia baba baba cha kumuomba mungu ni akupatie mke sahihi vyote vitajiset alafu Sasa mungu anakuangalia kwa jicho la pekee kwenye ridhiki bachela kulala njaa ni kawaida Ila si kwa Alie na familia anaechakalika oeni vijana na Kuna baadhi ya madili yanahusisha mpunga mrefu unaweza pishana nayo Kama huna family jamii inakuchukulia mhuni tu
 
Nadhani ingekuwa vema tukaelewa nini maana ya kutooa au kutoolewa.

Kufafanua hilo, naomba nirejelee Agano Jipya.

Yesu anawaambia wafuasi wake kwamba, (si nukuu rasmi) "kama mtu ataweza kuishi kama mimi (Yesu) atakuwa ametenda jambo njema sana duniani".

Aidha, Petro katika Agano hilohilo anawaambia wafuasi haohao kuwa, mtu asieweza kudhibiti au kukabiliana na tamaa za mwili, basi na aowe na aolewe.

Kutooa au kutoolewa maana yake ni kutoshiriki kufanya mapenzi au ngono, ni kutojamiana.

Kwa hiyo, hayo uliyoyataja hapo juu kwenye comment ni makosa dhidi ya ndoa. Yeyote aliye katika hali hiyo, amefanya kosa dhidi ya akili.

Kama mtu anazini, au anafanya uasherati, ni single mama au baba, huyo ameoa na ameolewa. Mtu yeyote aliye katika hali hii hawezi kusema hajaoa au hajaolewa.
 
Mkuu fanya I'ma uoe fanya jui chini uoe najuta kuchelewa kuoa japo Nina mtoto ambae hatuelewani nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…