Mtu asipooa au asipoolewa hafanyi kosa lolote kimaadili. Hilo si kosa la kimaadili wala la kisheria.
Sio dhambi kutokuoa au kutoolewa.
Lililo kosa la kimaadili au kosa dhidi ya akili yaani dhambi ni: KUVUNJIKA KWA NDOA au TALAKA, UZINZI NA UASHERATI; PONOGORAFIA, MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE. Haya ndio mambo watu tunatakiwa tutafakari, tuyachunguze, tufuatilie; tujue yanasabishwa na nini, na kwa nini; halafu tuamue.
Hebu fikiria ni ndoa ngapi zinavunjika? Jiulize: ni ngapi? Jiulize; ni mateso kiasi gani watoto wanapata na kupitia kiakili na kimwili kwa wazazi kutalakiani? Ni wangapi wanateseka kwa makosa haya ya wazazi kutalakiana, magonvi, au kutengana? Madhara yake ni nini? Jiulize!!
Kwa kufanya uzinzi na uasherati, ni wanawake wangapi wamezalishwa na kutelekezwa? Wanawake wangapi wamepigwa mimba na kutelekezwa? Wangapi? Hao watoto wanatunzwa na nani? Haya sio mateso? Huu sio uuaji? Na hivi ndivyo mambo au mpango unapaswa kuwa? Hili ndilo lengo?
Huyo Mungu ambae waafrika mnapenda kumrejelea na kuficha udhaifu au ukatili au ubaya au mapungufu yenu, kwa kukosa kwenu uelewa wa mambo na elimu ya vitu, hakuna mahali amesema watu lazima waoe na kuolewa au wazaee. Hakuna!
Mwenye huu uthibitisho alete hapa.
Watanzania ni watu ambao hawatumii akili kabisa, ukiacha hekima na busara. Wanafungisha ndoa huko wanakoita makanisani na misikitini, lakini hawasimamii hizo ndoa walizozifungisha. Watu wanatalakiana, wanaachana kila siku. Kila uchao ni ugomvi, mafarakano kwenye hizo ndoa.
Wasivyo na akili, hekima, na busara, wameshindwa kushughulikia matatizo ya ndoa, sasa wanataka kuwabagua watu wasio na kosa kimaadili, yaani wale wasiooa na wasioolewa.
Huu ni wendawazimu mkubwa.
Ndugu zangu watanzania acheni kushikilia mambo na kudhani kwamba haya ni mambo yetu; na yale ni mambo yao.
Tupende kufikiri, kuchunguza, kufuatilia na kisha kuamua. Tuache kuchukua mambo kama yalivyo bila kujua yalianza vipi, wapi na kwanini.
Hivi kweli suala la mtu kutokuoa au kutoolewa nalo ni jambo zito linalohangaisha jamii au familia, kwamba mtoto wangu hajaoa au hajaolewa?
Mtu asieoa au asieolewa ana kosa nini kimaadili au kiakili; au hata kimwili?