Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Siku ya kwanza unamuomba mtoke chakula cha jioni ili kufahamiana (dinner date), anakuomba nauli na hela ya kusuka, mara hana viatu, nusu saa kabla amekuomba umnunulie salio. Achana na hayo matatizo ndugu unakaribisha umaskini. Maskini huwa hawana aibu rafiki yangu, muache atafute kwanza shughuli ya kufanya ndiyo aingie kwenye mahusiano. Atafute kazi ya kuingiza kipato kwanza.
Maskini wengi hawajui kupenda, hisia zao zinaongozwa na njaa, tena njaa kali sana, njaa yake ikiisha ndiyo anagundua kuwa hajawahi kukupenda hata kidogo. Achana na matatizo hayo. Kimbia janga hilo. Tafuta mtu mwenye akili timamu, na sio mtoto ambaye anatembea kwa kunusa pesa za watu bila jitihada.