Maskini wenye hasira kali Zambia wamuua kwa kumchoma moto Mtanzania

Maskini wenye hasira kali Zambia wamuua kwa kumchoma moto Mtanzania

Mbona unaeneza chuki mkuu unatatizo gani na waarabu?
Chuki unaijua wewe au unaropoka tu hapa? wewe ni mgeni hapa JF? wabongo wanauawa South Africa ila hatuoni povu hapa lakutukana mpaka dini ya hao wasouth,ila ikitokea mbongo akawa na tatizo kwenye nchi za lkiarabu au India hua mnatukana mpaka dini ya wahusika,double standard.
 
POLISI ZAMBIA wamethibitisha kifo cha Mfanyabiashara maarufu wa Nkeyema, Zambia, Sikaonga Ernest almaarufu Yakaipa na rafiki yake David Mwakyoma Mtanzania aliyechomwa moto na kundi la maskini wenye hasira kali.

Wawili hao wameuawa katika Wilaya ya Mumbwa na kundi la maskini wenye hasira kali wakati wa ghasia baada ya taarifa kuenea kuwa mtu mwingine aliyejulikana kama Mwiya Kashweka ameuawa na kuondolewa sehemu za siri ambapo kina Mwakyoma walidhaniwa ndo walifanya unyama huo.

Majengo mbalimbali ya umma yameharibiwa na wananchi waliofanya ghasia miongoni mwao ofisi ya Mifugo kuteketezwa na kuwa majivu, madirisha ya ofisi za Polisi, Uhamiaji na Usajili wa Taifa yote yamevunjwa.

Magari na lodge ya marehemu Yakaipa yaliharibiwa kwa kuchomwa moto. Hii ilikua tarehe 13/09/2023.

Binafsi nimesikitishwa sana na hizi taarifa na kulaani maskini wote wanaodhani matajiri wote wamepata utajiri wao kwa kutumia nguvu za giza. Wazambi ni wapole ila wana wivu mkubwa kwa kudhani wanaopambana na kufanikiwa hudhulumu haki zao. Ndugu Mwakyoma na mwenzie wameuwawa kwa kudhaniwa kuwa wanahusika na ushirikina uliosababisha kifo cha Mwiya. Na kwa siku za karibuni kumekuwa na kamata kamata ya watanzania waliopo huko.

Ila pia kwa upande mwingine kuna watanzania wenzetu wanaotuchafua sana kwa majirani kwa kuendekeza ushirikina. Mwaka jana kuna watanzania waliokamatwa Zambia kwa kwenda kufanya kazi ya kutoa uchawi kule Zambia kama wanavyofanya Kigoma na Sumbawanga. Ukiwa mtanzania kwa nchi za jirani unachukuliwa kama mbobevu kwenye ushirikina.
Siku zote lisemwalo lipo.
 
Da uharibifu mkubwa wa Mali!
Hapo familia yake itaishi vipi? Wafsnyakazi wake ajira ndio kwishnei!
Hatari sana
 
Da uharibifu mkubwa wa Mali!
Hapo familia yake itaishi vipi? Wafsnyakazi wake ajira ndio kwishnei!
Hatari sana
Jamaa ni tajiri ana mali nyingi sehemu mbalimbali za Zambia. Hapo kwenye ajira ndo wengi watapoteza mwelekeo. Inasemwa kuwa wakati wa uhai wake alikuwa kaajiri watu zaidi ya 500.
 
Apandacho mtu ndicho atakachovuna.
Marehemu huenda kavuna alichopanda aidha hadharani au sirini
Mungu anapopitisha hukumu hutumia sababu yoyote ile ili uhukumiwe
 
Back
Top Bottom