Maskini wenye hasira kali Zambia wamuua kwa kumchoma moto Mtanzania

Maskini wenye hasira kali Zambia wamuua kwa kumchoma moto Mtanzania

Huyo marehemu kama ilivyo kwa matajiri wengine hata hapa TZ alikuwa akituhumiwa kutumia ushirikina kwenye ishu zake. Kuna kesi ziliibuka za watu kupotea na kukutwa wameuwawa huku sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa. Watu wakawa wanamyooshea kidole kuwa ni mhusika. Tukio la kifo cha Mwiya ndo ikawa kama 40 yake ingawa bado wananchi hawakuwa na uhakika 100%. Mwakyoma nae alikuwa mfanyabiashara huko Mumbwa na alifahamika zaidi kwa jina la Dollar One (a.k.a). Huenda pia sababu nyingine iliyofanya maskini wawe na hasira ni tabia ya jamaa enzi za uhai wake kugawa pesa kwa kurushia watu.
Huyo mwenye dread ndiyo mtanzania
Aise kauwawa kifo cha kikatili sana

Ova
 
Kuna kitu nilijifunza kwa hao matajili wa Zambia na Tunduma Hadi mbeya
 
POLISI ZAMBIA wamethibitisha kifo cha Mfanyabiashara maarufu wa Nkeyema, Zambia, Sikaonga Ernest almaarufu Yakaipa na rafiki yake David Mwakyoma Mtanzania aliyechomwa moto na kundi la maskini wenye hasira kali.

Wawili hao wameuawa katika Wilaya ya Mumbwa na kundi la maskini wenye hasira kali wakati wa ghasia baada ya taarifa kuenea kuwa mtu mwingine aliyejulikana kama Mwiya Kashweka ameuawa na kuondolewa sehemu za siri ambapo kina Mwakyoma walidhaniwa ndo walifanya unyama huo.

Majengo mbalimbali ya umma yameharibiwa na wananchi waliofanya ghasia miongoni mwao ofisi ya Mifugo kuteketezwa na kuwa majivu, madirisha ya ofisi za Polisi, Uhamiaji na Usajili wa Taifa yote yamevunjwa.

Magari na lodge ya marehemu Yakaipa yaliharibiwa kwa kuchomwa moto. Hii ilikua tarehe 13/09/2023.

Binafsi nimesikitishwa sana na hizi taarifa na kulaani maskini wote wanaodhani matajiri wote wamepata utajiri wao kwa kutumia nguvu za giza. Wazambi ni wapole ila wana wivu mkubwa kwa kudhani wanaopambana na kufanikiwa hudhulumu haki zao. Ndugu Mwakyoma na mwenzie wameuwawa kwa kudhaniwa kuwa wanahusika na ushirikina uliosababisha kifo cha Mwiya. Na kwa siku za karibuni kumekuwa na kamata kamata ya watanzania waliopo huko.

Ila pia kwa upande mwingine kuna watanzania wenzetu wanaotuchafua sana kwa majirani kwa kuendekeza ushirikina. Mwaka jana kuna watanzania waliokamatwa Zambia kwa kwenda kufanya kazi ya kutoa uchawi kule Zambia kama wanavyofanya Kigoma na Sumbawanga. Ukiwa mtanzania kwa nchi za jirani unachukuliwa kama mbobevu kwenye ushirikina.

View attachment 2761245View attachment 2761246View attachment 2761248View attachment 2761249View attachment 2761250View attachment 2761252View attachment 2761253
Serikali inapozembea kuwapatia wananchi wake elimu bora haya ndiyo sehemu ya madhara ya kukosa elimu.

Msiwaite maskini, hao ni angry mob.

Elimu
Elimu
Elimu
 
Ghasia hizi waafrika tungeziweka kwa mafisadi wetu nahisi mpaka sasa tungekuwa mbali kiuchumi.
Mafisadi ni werevu kuliko maskini. Mafisadi hawafisadi mpaka wawachonganishe maskini. Maskini wakishaanza kugombana ndipo mafisadi wanafanya yao.
Hukuona akina msukuma wanapelekwa Dubai kabla ya DP world kufumka?
Au kubuniwa Royal Trip kabla hatupigwa cha juu kwenye malipo ya ndege na sasa mitumba ya train za sgr?
 
Majibu ya Wizara ya Mambo ya Nje yapo?
 
Serikali inapozembea kuwapatia wananchi wake elimu bora haya ndiyo sehemu ya madhara ya kukosa elimu.

Msiwaite maskini, hao ni angry mob.

Elimu
Elimu
Elimu
Wewe pia ni maskini mwenye ujuaji. Uwe unaandika tu kwa kiswahili
 
Wewe pia ni maskini mwenye ujuaji. Uwe unaandika tu kwa kiswahili
Usijali. Ulichoelewa chukua, kilichokutoa kapa achana nacho

Angry mob ni kundi la watu wenye hasira.

Najua ulidhani namaanisha njaa.
 
Angalau wewe umetoa ufafanuzi
Zamani nilikua nikipeleka Biashara Zambia, Lusaka, Ndola, Kitwe, Luanshya, na Boda ya Congo huko, so najua sana kuhusu Matajiri wakubwa wa Zambia kutajirika kwa Uchawi kutokea Tanzania, Waganga wao wapo Iringa na Mbeya, na kuna Mama mmoja alikua Morogoro ni Marehemu sasa.
 
Back
Top Bottom