Matajiri wengi wa Zambia hasa wenye Asili ya Nakonde, ama kutoka miji ya jirani na Nakonde, ama wanaokuja kununua Mzigo Tanzania, Wametajirika zaidi baada kuwa na urafiki na Watanzania!
Watanzania wanawapeleka kwa Waganga hapa Tanzania ili wawe Matajiri....!
Hata kama huamini Uchawi hiyo haindoi Ukweli wa uwepo wake!
Watu hapa wanawaona Wazambia wasio na akili kwa walichokifanya ila wamevumilia sana wakitafuta Mchawi ni nani, mpaka kuja kufanya walichofanya walikua na Ushahidi wa Mazingira!
Zaidi ya watu 100 wameuwawa vifo vikifuatana vikifanana, kunyofolewa viungo vya Binadamu.....! Miezi michache kupita Kaka wa huyo Mzambia Marehemu, anahukumiwa miaka 50 jela kwa kukiri kwake kuhusika na kifo cha Mtu mmoja ambaye nae alinyofolewa viungo vya mwili, majuzi kuna Marehemu amekutwa hana Viungo, wananchi kwa kupepeleza wakapenyezewa habari juu ya uhusika wa huyo Rasta ambaye ni Rafiki wa Tajiri wa Kizambia, ikasemwa kila akionekana eneo flani baada ya siku chake, mwili wa mtu aliyeuwawa unapatikana na yeye kutoonekana tena, wamemfata Raia wenye hasira, kumweka mtu kati anasema yeye anatumwa tu, anatumwa na nani...!?
Akamtaja huyo Tajiri YAKAIPA kwamba ndo huwa anampa kazi, Hasira za Wanachi zikawaka, safari kwenda kwa Tajiri ikaanza, Tajiri kuona Raia wana hasira akataka kuruka Ukuta ikashindikana, akatoa Bastola atishe Raia haikusaidia, yakaanza Maswali, wakambeba yeye na Marasta mpaka ndani ya Nyumbani, kufika ndani wakaanza kufanya Ukaguzi, kuna Chumba kimoja wakakuta Jeneza kufungua Jeneza kuna Vitu vya ajabu.....!
Kilichotokea ndo kilichosikika.