Maslahi madogo Clouds yamtoa Ruby Fiesta

Wao wamekiuka vingapi? Luge anavopenda ligi tutaona km atampeleka mahakamani
Aliwahi kumpeleka mahakamani nani? Kwa issue kama hizi unaweza kumpeleka mahakamani featured act lakini sio yule ambae awepo au asiwepo bado hana effect yoyote kwenye show!!! Endapo Wiz Kid asingetokea pale, raia wasingeelewa but who cared kwamba Ruby hakutokea?!!
 
Umenena..wanawapa vichwa ndio maana wanaendelea kufanya upumbavu kwa watoto wa maskini wao wanendelea tu kufungulia mahawara zao maduka
 
Hawa wanaomsema huyu binti nawashangaa sana na kama ni wanaume wenzangu basi wavae bikini tu,yaani mtoto wa watu anapambana kupinga dhuluma kupitia kipaji chake watu wanamdhihaki na kumwambia ataporomoka,kweli!!!!!!nna uhakika hawa wanaosema haya ni wasomi zaidi ya huyo bint ila bado hawajiamini,yaan mtu anahisi hawez kuendelea kimuziki bila CLOUDS,haya leo TCRA wakiifungia?ina maana wasanii wote watapotea.
Mafanikio huja kwa kujaribu,vijana wenzetu wabadilike,ukibana pua kuwa "Bila Clouds HIFIKI MBALI" kweli hutafika....Sugu yule pale amepoooondwa 2010 na bado akashinda ubunge,walimghas sanaaa,mwaka jana ndo kaongoza kwa kura za UBUNGE.
ALITHUBUTU
 
Unataka kusema wasanii wote wametoka kisa clouds?ukinambia issue ya THT na akina Kibajaj sawa,ila kwa radio station sio kweli,nakupa mfano mmoja,akina nature walitamba Dar na nje ya Dar na wakat huo huko nje ya Dar hakukua na clouds TV wala Radio wala mtandao wa intanet wa kusikiliza na kuangalia..............Huyo Ruby unamaanisha hatafanya vizur kama ngoma zake zisipopigwa clouds?hapo ndo kuna kosa kwenye fikra zetu,
Kibiashara huenda huyu bint akatoka zaid baada ya kukataa kufanya kazi na hao jamaa.Inaonesha wewe kama ungekua mwanamuziki basi klaudz kama wangekuwa wanacheza nyimbo zako FIEST ungeomba upande bure,yaani UNAOMBA WEWE
 
Mi najiuliza tu ivi leo sugu anahitajika e fm kipindi cha joto la asubuhi je atakubali kufanya nao mahojiano maana hando alimsagia sana kipindi yupo clouds huo uchaguzi wa 2010
 
sugu hakusanda ila ruge alionaanachafuliwa sana kwa mixtape za matusi akaamua kuomba suluhu kwaviongoz wa chama na serikali kwa chama walikaa mbowe na sugu na viongozi wengne baadae serikali ikakaaa ikiwakilishwa na emmanuel nchimb kama wazir wa mambo ya ndani ndio wakapatanishwa maana watangazaji mashoga wa mawingu walisemwa live na wote wanaotumia ARV wamawingu walitajwa kulikokuendelea kuchafulia bora mkurugenzi akaombe suluhu tu
 
mkuu hiv kweli hizi tuhuma za ushoga pale clouds watangazaj gani hao watajwe
 
swala sio kutetea maslai yake ilibidi arudishe fadhira ametolewa bure vijana wangap wapo mtaani wanavipaji lakini hawana nafasi ya kuonekana pesa aliyokataa rub ni kubwa sana ni laki 8 sijajua kwa mkoa mmoja au yote
 
Nilipoisoma hii hoja yako nikalazimika kusoma mara mbili mbili hoja yangu kuangalia ni wapi niliposema wasanii wote wametoka kwa ajili ya Clouds... SIKUPAONA! Post uliyoni-quote ni hii hapa: Hayo uliyosema umeyatoa wapi?! Wapi nimezungumza suala la Clouds kupiga au kutopiga nyimbo?!

Sasa nije kwenye hoja yako! Kwanza wote nyinyi mnasahau hoja ya msingi! Nitaandika kwa herufi kubwa. RUBY ALISHASAINI MKATABA NA CLOUDS NA AKAWA ANA-POST PICHA HADI INSTAGRAM KUONESHA YUPO EXCITED NA FIESTA!!!

Sasa ina maana alisaini kabla hajafahamu maslahi yake? Kuna mdau alidai walisainishwa mbele ya kamera... nikahoji ikiwa hata posting alizokuwa anafanya Instagram nazo alikuwa amesimamiwa na kamera... hadi sasa sijapewa jibu!!! labda unipe wewe!! Kwahiyo jambo la kwanza anaonesha wazi si mtu wa kuheshimu mikataba! Music is business... ALWAYS biashara ya muziki inaenda na mikataba! Usipoweza kuheshimu mikataba kwenye biashara you'll never ever succeed! Ukiingia kichwa kichwa, that's your problem and no one's!

But second, hapa JF watu wana kiburi cha degree zao tena zingine zenye GPA za sifa! Bado hawa tunawaona wanalilia hata kufanya kazi za kujitolea for free... ukimpa nauli tu atakushukuru kweli kweli! Why?! Lengo lao ni ku-gain experience na ku-excel kwenye career zao. Leo hii CRDB, PSPF, PricewaterhouseCoopers, Law Firms n.k wakitangaza wanahitaji wafanyakazi wa kujitolea but hawatalipa chochote... applications za graduates zitamiminika kwenye milango yao hadi watazikimbia! Unataka kusema watakaofanya hivyo watakuwa ni wapum'bavu?!!

Mnaweza kuendelea kumtia ujinga ambao hata nyinyi wenyewe hamkuufanya wakati mnajenga career zenu! Hapa watu wanaweza kujifanya ni fighters lakini walisaini kazi ya mshahara wa laki 6 kwa mwezi na degree zao na wanawanyenyekea mabosi wao kama Mungu na hawana ubavu wa kutoka!!! Kwa pale alipo, Ruby yupo bado sana, tena sana! Hata ukimweka na Yamoto Band kwenye show yako bado huwezi kumweka Ruby kama featured act! Ruby analihitaji jukwaa la Fiesta kuliko jukwaa linavyomuhitaji yeye!! The problem mnadhani watu tunazungumzia kupiga nyimbo zake redioni!

Mwisho niseme kwamba, ikiwa wewe upo very successful kwenye career yako! Na kama kuna mwingine yeyote humu yupo very successful! Please, ningewashauri muache kuwatia watu ujinga kwa sababu hata nyinyi ni vile tu mtakuwa mmesahau mlikotoka hadi kufika hapo mlipofika!!! Si ajabu ni wale ambao walifanya field training for free wakati walikuwa wana-contribute!
 
Me naona aibu kabisa sijui nielezee vipi
 
Yale makaratasi tu ya show off za tv , na akashitakiwe basi
 
Me naona aibu kabisa sijui nielezee vipi
Wewe na wenzako ingawaje mnajifanya ndo mnajua lakini mnaonesha ni jinsi gani msivyofahamu masuala ya kibiashara! Huwezi kujitia kujua halafu unatetea mtu aliyeingia mkataba halafu anaacha kutekeleza mkataba wake! Kwani wakati anaingia mkataba alikuwa amelewa? Na kama alikuwa amelewa, ni tatizo la nani hilo?!
 
Yale makaratasi tu ya show off za tv , na akashitakiwe basi
Ilikuwaje akakukbali kusaini hayo makaratasi ya show off?! Ule ulikuwa ni mkataba wa kuwa tayari kufanya show Mwanza ili audience ifahamu ni nani na nani angepanda stejini! Na hapa chini akaonesha excitement yake ya kuwa tayari kwenda Mwanza!!

Na ukimsia alichoongea jana, utagundua hoja yake sio maslahi madogo bali ni hofu ya kulipwa! Sasa ulitaka aanze kulipwa kabla hata hiyo show hajafanya?! Yaani unataka kuniambia wengine wooooooote walioenda Mwanza walilipwa lakini angedhulumiwa Ruby peke yake?!
 
Hurnda alishang'atwa na nyoka so yuko conscious na ambacho kingeenda kutokea, labda ndio zao wale mapebari sio wa kuwatetea hata kidogo ruge anaroho mbaya sana
 
Hurnda alishang'atwa na nyoka so yuko conscious na ambacho kingeenda kutokea, labda ndio zao wale mapebari sio wa kuwatetea hata kidogo ruge anaroho mbaya sana
There you are! Tatizo lako wewe na wengine ni Ruge na sio issue ya Ruby!! Na wengine tatizo lao ni kutofahamu hii tasnia inaendeshwaje! Lakini narudi pale pale... endeleeni kumtia ujinga ambao hata nyinyi wenyewe hamjawahi kuufanya kwenye shughuli zenu huku hata wewe ukiwa unafahamu kwamba Ruby anaihitaji Fiesta kuliko Fiesta inavyomhitaji Ruby! Hata huu mjadala umekolea si kwa sababu ya Ruby bali kwa sababu ya Clouds!! Kama angekuwa amezinguana na wengine, hii mada wala isingepata attention! Hata kama show itakutanisha ONLY Baraka De Prince, Ya Moto Band, Ruby, Raymond, Harmonize, Dogo Janja, Young Killer na Stamina; bado kwenye hiyo show Ruby hawezi kupata status ya Featured Act!
 
Hayo unayasema wewe , muda utaongea kama kweli jukwaa na ruby nani anamuhitaji mwenzie maswala ya kupewa promo kisha unyimwe uhuru wako yamepitwa na wakati.
 
Sasa lakini jide si alikuwa tayar legend wakati analiamsha beef na clouds sasa ruby hata hit kumi hazijafika na wala nyimbo zake hazifiki hata 20
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…