Habari mimi kero yangu ni kuhusu Kampuni ya ulinzi ya Gardaworld Security Tanzania kama inavyofahamika, Mwaka 2025 Serikali ilipandisha kima cha chini cha mshahara kwa makampuni makubwa ya ulinzi ikiwemo kwetu.
Ilitakiwa kuanzia Januari 2026 waanze kulipa kwa maslahi mapya, ambapo baadhi ya makampuni mengine walifanya hivyo, lakini Gardaworld wao walilipa kiasi cha zamani tulipowauliza wakaanza kuleta visingizio mara tunalipa kulingana na mteja unapofanya kazi akikubali kuongeza malipo ya huduma.
Sasa walipoona watu tumekuwa wakali tukadai salary slip ambazo walikuwa wamekuwa wagumu kuzitoa, baadaye baada ya mashinikizo ya Wafanyakazi wengi zikatolewa zikiwa zinaonyesha basic salary ya mshahara mpya walichofanya hawakulipa sikukuu zote na overtime wakaweka fixed kwa wote.
Hivyo, malipo yakabaki jumla hayana utofauti na malipo ya Mwaka 2025, sasa naomba kutumia platform hii kuuliza, je Serikali ilipandisha mshahara ili wananchi wapate nafuu au kuwaridhisha?
JAMBO LINGINE
Pia, Gardaworld Security Tanzania imekuwa ikivunja Sheria nyingi za ajira, miaka kama 7 hivi nyuma ilizinunua kampuni mbili za ulinzi Kenya Kazi (KK) na Ultimate Security, haikuwabadilishia mikataba Wafanyakazi wa hizo kampuni, kila mfanyakazi aliendelea kulipwa kama ilivyokuwa analipwa na kampuni iliyopita.
Ingawa walibadilishiwa sare za kazi wote wakaanza kuvaa nembo za Gardaworld bila malipo yoyote, imefika muda sasa zaidi ya mwaka wanalazimisha Wafanyakazi wasaini mkataba wa Gardaworld bila kuwapa malipo ya kuvunja mikataba iliyopo.
Wiki iliyopita field officers walipita kwenye malindo wakiwa na mikataba mipya wakiwalazimisha watu wasaidi ambapo baadhi walikataa wengine walisaini.
Vijana wengi tunaotumikia ajira ya kampuni hiyo hatujui hatima yetu, tunataka Dunia ijue kinachoendelea.