Masoko yaanza kuchomwa tena? Angalia Soko la Mbuyuni Moshi likiteketea

Masoko yaanza kuchomwa tena? Angalia Soko la Mbuyuni Moshi likiteketea

Taarifa ya Azam inaeleza kwamba soko la Mbuyuni huko Moshi linateketea usiku huu.

Moto umeanza usiku wa saa 7 tarehe 06/02/2024

Hivi kwanini masoko hayaungui mchana?

...............
Kufuatia ajali ya Moto iliyoteketeza Soko la Mbuyuni, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema moja ya changamoto zilizosababisha moto huo kutodhibitiwa kwa wakati ni Ubovu wa gari la Zimamoto la Manispaa hiyo, uliosababisha kuomba msaada wa gari kutoka TPC ambalo lilichukua takriban Dakika 30 kufika eneo la tukio

Amesema Serikali inafanya tathmini ya kujua chanzo na hasara za moto huo ulioanza majira ya Saa 7 usiku wa Februari 6, 2024

Ikumbukwe, Mnamo Februari 29, 2016 Soko hilo liliungua baada ya moto mkali kuzuka majira ya Saa 2 usiku, pia Februari 1, 2022 Soko hilo liliteketea upande wa Matunda na Mbogamboga kwa moto ambao chanzo chake hakikujulikana mara moja


View attachment 2895511
Mkuu saa 7 usiku ya tarehe 06.02.24 imeshafika?
 
tanzania na laana damudamu. mambo ya kufukarishana haya. wakimjua aliyefanya hayo wamlawiti kisha wamchome moto
 
Sababu sokoni ushirikina mwingi. Ukiwa na macho ya rohoni unaweza kuwaona wafanya biashara wengi wako uchi kwenye vizimba vyao.
Ushirikina kila mahali !
Duh 🙄! Watatumaliza!
Lakini mbona hatuwaoni wakitajirika ??
 
Back
Top Bottom