Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Pa
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Masomo ya O level kama Kiswahili, Civics na Historia yanapotezaa tu muda watoto.

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza Form Four awe tayari kukabiliana maisha.
Pamoja na kwamba wewe ni mpumbavu Sana kwenye siasa kwa hili nakuunga mkono.
 
Hiyo lugha ya Kiswahili akimaliza shule atatumia hiyo kama asset wapi ili apate pesa?
Hiyo civics ataitumia wapi ili ajiajiri aitumie imwingizie pesa?
Ndo akili ya mwafrika hii ilivyo, kama yako....Kwa hali hii wacha kozi zingine zisipatikane tu bongo,wenye uhitaji watazifuata South Africa na Northern hemisphere.
 
Hiyo lugha ya Kiswahili akimaliza shule atatumia hiyo kama asset wapi ili apate pesa?
Hiyo civics ataitumia wapi ili ajiajiri aitumie imwingizie pesa?
uko sahihi
Elimu Ni investment ambayo lazima upate return au faida kwa unayeyasoma ya moja kwa moja

Kuwekeza kwenye Kiswahili,Civics na Historia kwa watoto Wa O Level Ni uwekezaji mbaya na mbovu

Kundi Hilo kubwa la vijana likimaliza form four linatakiwa kuwa na skills za kujiajiri.
Elimu lazima iwe asset sio tu kujaza memory card ya akili za watoto kwa makorokoro yasiyowasaidia kwenye maisha wamalizapo form four Kama hayo madudu ya Kiswahili Civics na Historia.Yanajaza tu memory card za akili za watoto tu hayana faida kwenye maisha yao.
 
Yasiondolewe ila yawe na Pass ya Subsidiary km ilivyokuwa kwa BAM na GS.
Yanapotezea muda watoto .Wayasome primary tu anayeyataka kuendelea nayo akayoseme A level huko.ndio kuwe na hizo choice akitaka Civics , historia,au Kiswahili akaenedelee nayo huko yapishe masomo ya kilimo,ufundi na ufugaji ambayo Yana nguvu ya kutoa ajira kupitia kujiajiri
 
Zamani tulisoma sayansi kilimo,sayansi kimu......unafutaje somo la uraia mkuu? Unafutaje kiswahili? Historia nayo ni muhimu.....cha msingi ni kutengeneza nitalala bora tu
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Masomo ya O level kama Kiswahili, Civics na Historia yanapotezaa tu muda watoto.

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza Form Four awe tayari kukabiliana maisha.
Sasa kiswahili kikiondolewa utawezaje kuandika yaondolewe? Wewe mwenyewe kuandika neno rahisi la Kiswahili yaondolewe umeshindwa umeandika "yaendelewe" ndiyo nini sasa hiyo?
Kuna watu wanajifanya wajuaji nchi hii hadi kero.
Hao waliyoyaweka wanazo akili kuliko wewe.
Kasome; how a subject qualify to be a discipline.
 
We ni mpumbavu kweli.

Wakitoe Kiswahili halafu iweje? Kuna nchi duniani isiyofundisha watu wake lugha?

Tena mimi ningependa masomo ya lugha yaongezwe na yakaziwe msumari. Watu wajifunze lugha nyingi kadiri inavyowezekana.

Shida yenu hata maana ya elimu bora hamfahamu! Mmejaa siasa siasa tu na ushabiki maandazi.

Elimu ya Tanzania ni nzuri isipokuwa inahitaji maboresho machache. Masomo yaongezwe lakini wanafunzi wafanye uchaguzi.

Niliwahi kuandika hapa kwamba "specialization" ianze kufanyika mapema kuanzia sekondari badala ya kuwatwika wanafunzi masomo yote wasome kila kitu.

Ongeza masomo, zidisha specialization.
Yaani watu wanajifanya wajuaji wakati wenyewe ni mbumbumbu wa viwango vya hali ya juu.
 
Sasa kiswahili kikiondolewa utawezaje kuandika yaondolewe? Wewe mwenyewe kuandika neno rahisi la Kiswahili yaondolewe umeshindwa unaandika "yaendelewe" ndiyo nini sasa hiyo?
Kiswahili tunasoma miaka Saba primary pamoja na kuwa tunakiweza kukiongea mitaani hizo spelling mistakes kitu kidogo .
 
Kiswahili tayari tunacho.kichwani ni.lugha yetu ya kila siku shule za msingi mtu kasoma kiswahili miaka Saba Tena masomo yote Bado tununampa zigo O level.Somo la kiswahili na uraia yafundishwe mwisho primary .Mtu akitaka kuwa specialist wa hayo masomo akayasome A Level.akitaka.
Mfano somo la economics hakifundishwi primary Wala O level liko A level Ya combination za ECA,HGE na EGM

Form four mtoto anakuwa kaiva kiumri kujitengemea Huwezi rudisha mtoto mtaani awezaye ongea tu Kama bwege kiswahili, history na Civics wakati hajui kulima,kufuga,Wala kupika hata maandazi au chapati kutumia ngano yetu auze apate pesa aache kelele za kusema ajira hamna

Elimu itoe wanafunzi wa kuajirika au kujiajiri Civics,kiswahili na history hayana huo ubavu yanazalisha wajinga tu Mitaani wasioweza jiajiri au kuajirika
Hao waliyosomea mengineyo wameweza kujiajiri?
 
Na kwenye literature watoe vitabu vya kina Onkokwo badala yake waweke Think big grow rich au rich Dad and poor Dad etc.

Hivi onkokwo si ndo mwenye ile nyimbo ilofungiwa kenya inaitwa Utawezana?
 
Kiswahili tunasoma miaka Saba primary pamoja na kuwa tunakiweza kukiongea mitaani hizo spelling mistakes kitu kidogo .
Unajua implications za hayo masomo kuondolewa?
Kwani sasa hivi watu hawalimi?
Wanaolima na kuvuna wanapata masoko ya uhakika?
Kwenye soko la dunia, mazao/ malighafi kutoka Tanzania yanao ubora wa kushindana?
Hao wahitimu wa vyuo vya ufundi hawatengezi bidhaa kwa sasa? Na kama wanatengeneza bidhaa zao zinavutia soko?
Kwa nini kuna mlundikano wa bidhaa za kichina na mataifa mengine ya nje?
Hadi hapo tatizo ni kiswahili, Historia, & co?
Hadi hapo akili yako imeanza kufunguka?
 
Hao waliyosomea mengineyo wameweza kujiajiri?
Ndio waliosomea ya ufundi,kilimo na ufugaji kibao wamejiajiri lakini waliosoma kiswahili,historia na Civics wanazurura na vyeti barabarani hawajui Cha kufanya
 
Uko sahihi lkn Masomo hayo hayawezi kuondolewa ni muhimu sana tena sana. Labda ufikiri upya. Kilimo kitiliwe mkazo na wanafunz wafundishwe kitaalam na sio ilimradi tu.
 
Yasiondolewe ila yaongezwe,mwanafunzi achague mwenywe nini anataka kusoma,,,, lakinu hofu yangu kichwa kimoja mambo mengi kitamudu kweli
Suala la kuchagua ndio la msingi. Mtu unasoma masomo kumi, this is too much! Mi ningeshauri secondary watu wasome masomo yasiyozidi sita, yaani Kiswahili, English na Mathematics yanakuwa ni compulsory then mtu baada ya hapo anaweza chagua masomo mengine matatu ya kus-pecialize atakayoenda nayo hadi form six au chuo. Hii ianzie form one. Biashara, Kilimo, Sayansi ( Ningependa iwepo na Ufundi lkn na hakika facilities za kufundishia na uchache wa walimu itakuwa changamoto kubwa sana)
 
Unajua implications za hayo masomo kuondolewa?
Kwani sasa hivi watu hawalimi?
Wanaolima na kuvuna wanapata masoko ya uhakika?
Kwenye soko la dunia, mazao/ malighafi kutoka Tanzania yanao ubora wa kushindana?
Hao wahitimu wa vyuo vya ufundi hawatengezi bidhaa kwa sasa? Na kama wanatengeneza bidhaa zao zinavutia soko?
Kwa nini kuna mlundikano wa bidhaa za kichina na mataifa mengine ya nje?
Hadi hapo tatizo ni kiswahili, Historia, & co?
Hadi hapo akili yako imeanza kufunguka?
Tatizo kubwa kwa yote uliyosema nu watoto vichwa kupata Moto kwa kujazwa misomo isiyoamsha vichwa vyao kujiajiri na kufanya mambo kitaalamu unawajaza vichwa mi kiswahili,mi historia na mi Civics unapobteza nguvu za akili kwa kuwajaza mavitu ambayo sio basic need ya kuwasaidia wajitegemee.Wabafika huko juu vichwa vimechoka kwa kujaza mitakataka mingi isiyohotajika kwenye maisha yao ya kujitengemea
 
Back
Top Bottom