Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Tatizo kubwa kwa yote uliyosema nu watoto vichwa kupata Moto kwa kujazwa misomo isiyoamsha vichwa vyao kujiajiri na kufanya mambo kitaalamu unawajaza vichwa mi kiswahili,mi historia na mi Civics unapobteza nguvu za akili kwa kuwajaza mavitu ambayo sio basic need ya kuwasaidia wajitegemee.Wabafika huko juu vichwa vimechoka kwa kujaza mitakataka mingi isiyohotajika kwenye maisha yao ya kujitengemea
Nimekuuliza vingine unajibu vingine!
Unalo tatizo la communication skills?
 
Somo la agriculture science ni muhimu Sana,tulio lisoma zamani na badae kujakusoma CBA na kwenda SUA linatusaidia mnoo.shule niliyosoma ilikua na ufundi pia hapo kuna wanafunzi walikua hawasomi history na biology walikua wanachukua Kama option pia sasaivi Ni wakandarasi bora na wako vizuri.kwakeli mfumo wa elimu unabidi kuingiza masomo ya ufundi Kama electrical installation, technical drowning, computer, agriculture science, plumbing, namengine ya ujenzi na nimasomo ambayo bado yapo shida nihayapo shule za kata hivyo kufanya watu wengi kutotasoma.
 
Suala la kuchagua ndio la msingi. Mtu unasoma masomo kumi! Mi ningeshauri secondary watu wasome masomo yasiyozidi sita, yaani Kiswahili, English na Mathematics yanakuwa ni compulsory then mtu baada ya hapo anaweza chagua masomo mengine matatu ya kus-pecialize atakayoenda nayo hadi form six au chuo. Hii ianzie form one. Biashara, Kilimo, Sayansi ( Ningependa iwepo na Ufundi lkn na hakika facilities za kufundishia na uchache wa walimu itakuwa changamoto kubwa sana)
Wazo zuri kuhusu facilities hasa za ufundi ningeshauri kufanywe intergration na vyuo vya VETA kwa kuanzia.Sylabus ya VETA iwe intergrated kwenye secondary na karakana zao zitumiwe na wanafunzi was secondary kuhusu walimu tunaweza import kwa kuanzia kwenye nchi za wenzetu wa dunia ya Tatu Bei zao nafuu wakati tukiandaa wetu ndani ya miaka mitano twaweza kuwa na wa kwetu wa kutosha wa kilimo ,ufundi na ufugaji
 
Unajua implications za hayo masomo kuondolewa?
Kwani sasa hivi watu hawalimi?
Wanaolima na kuvuna wanapata masoko ya uhakika?
Kwenye soko la dunia, mazao/ malighafi kutoka Tanzania yanao ubora wa kushindana?
Hao wahitimu wa vyuo vya ufundi hawatengezi bidhaa kwa sasa? Na kama wanatengeneza bidhaa zao zinavutia soko?
Kwa nini kuna mlundikano wa bidhaa za kichina na mataifa mengine ya nje?
Hadi hapo tatizo ni kiswahili, Historia, & co?
Hadi hapo akili yako imeanza kufunguka?
Kwa hiyo wakisoma kiswahili,Civics,na history hayo matatizo ndio yataondoka?
 
Uko sahihi lkn Masomo hayo hayawezi kuondolewa ni muhimu sana tena sana. Labda ufikiri upya. Kilimo kitiliwe mkazo na wanafunz wafundishwe kitaalam na sio ilimradi tu.
Ivi history inaumuhimu gani apo mtaa unao ishi au hapo nyumbani kwako?namanisha hii ya darasani inayofundishwa mashuleni
 
Tatizo kubwa kwa yote uliyosema nu watoto vichwa kupata Moto kwa kujazwa misomo isiyoamsha vichwa vyao kujiajiri na kufanya mambo kitaalamu unawajaza vichwa mi kiswahili,mi historia na mi Civics unapobteza nguvu za akili kwa kuwajaza mavitu ambayo sio basic need ya kuwasaidia wajitegemee.Wabafika huko juu vichwa vimechoka kwa kujaza mitakataka mingi isiyohotajika kwenye maisha yao ya kujitengemea
Wewe ni shortsighted tu.

Shule isiyofundisha watu lugha sio shule hiyo!

Ndio maana uko hapa hata kuandika hujui lakini unajitutumua tu mradi uonekane una akili timamu!
 
Labda somo la viwanda ndio watakuelewa. Maana ndiko kulikojaa hewa kuliko kule kwenye watumishi hewa
 
Kwa hiyo wakisoma kiswahili,Civics,na history hayo matatizo ndio yataondoka?
Ndio ujue kuwa hukitendei haki kichwa chako! Sijasema kwamba wakisoma hayo masomo ya Kiswahili, Civics na History ndio tatizo linaondoka! Tatizo lako wewe umeshindwa kugundua shida iko wapi?
Shida ya elimu ya Tanzania ipo kwenye muundo ( structure), vitendea kazi ( facilities) na mfumo ( education system).
Kwa hiyo wewe ulishindwa kugundua tatizo na badala yake ulihamisha tatizo.
Na ili ujue kuwa hukujifikirisha vya kutosha wapo wahitimu kibao waliosomea taaluma za sayansi, biashara na ufundi wapo mitaani wameshindwa kujiajiri. Je, hao nao masomo waliosoma yafutwe?
Kwa hiyo wazo lako halikuwa na hekima na pia hujui adui wa tatizo la ukosefu wa ajira na kujitegemea ni nani.
Bila shaka hadi hapo nitakuwa nimekuongezea kitu kwenye ubongo wako tena bila ya kulipia ada yoyote.
 
Ndio ujue kuwa hukitendei haki kichwa chako! Sijasema kwamba wakisoma hayo masomo ya Kiswahili, Civics na History ndio tatizo linaondoka! Tatizo lako wewe umeshindwa kugundua shida iko wapi?
Shida ya elimu ya Tanzania ipo kwenye muundo ( structure), vitendea kazi ( facilities) na mfumo ( education system).
Kwa hiyo wewe ulishindwa kugundua tatizo na badala yake ulihamisha tatizo.
Na ili ujue kuwa hukujifikirisha vya kutosha wapo wahitimu kibao waliosomea taaluma za sayansi, biashara na ufundi wapo mitaani wameshindwa kujiajiri. Je, hao nao masomo waliosoma yafutwe?
Kwa hiyo wazo lako halikuwa na hekima na pia hujui adui wa tatizo la ukosefu wa ajira na kujitegemea ni nani.
Umechanganya mambo mengi waliosoma kilimo,ufundi na ufugaji hawahangaiki Mitaani walio wengi

Wanajishughulisha na kilimo,ufugaji na ufundi

Mada yangu imejikita kwenye haya masomo matatu usirundike ambayo sijayaongekea
Haya matatu Nina. Uhakika wa watu kujiajiri

Wako kibao wanachapa kazi hao wasoma kiswahili, history na Civics Ni mzigo kwa taifa
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Masomo ya O level kama Kiswahili, Civics na Historia yanapoteza tu muda watoto.

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na raslimali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaji vito vya madini,madini tunayo nk ili mtoto akimaliza Form Four awe tayari kukabiliana maisha.
Kwenye ufundi, walipouwa zile shule tano za ufundi kwa kuziongezea makorokocho mengine nikajua ufundi ndo basi tena... IFUNDA TECH, TANGA TECH, MOSHI TECH, MAZENGO NA MTWARA TECH...
 
Umechanganya mambo mengi waliosoma kilimo,ufundi na ufugaji hawahangaiki Mitaani walio wengi

Wanajishughulisha na kilimo,ufugaji na ufundi

Mada yangu imejikita kwenye haya masomo matatu usirundike ambayo sijayaongekea
Haya matatu Nina. Uhakika wa watu kujiajiri

Wako kibao wanachapa kazi hao wasoma kiswahili, history na Civics Ni mzigo kwa taifa
Kwa hiyo unao uhakika kabisa wakiyaondoa hayo basi tatizo la unemployment & underemployment litaisha?
 
Mkuu napenda niitetea civic(uraia) ,hili ni somo muhimu sana kwa watoto na taifa kwa ujumla,hebu nikupe maana ndogo tu ya neno civics#this is the study of human rights and responsibilities of citizens,sasa ukitaka somo la uraia liondolewe maana take unataka watoto wetu wasijue haki zao na wajibu wao kwa taifa letu .

Pia somo la uraia linamsaidia mtoto kuwa mzalendo kwa taifa lake,katika somo hili tuna topic nyingi sana ambazo zinamfanya mtoto kuwa na uelewa mpana kwa taifa lake,hivyo sidhani wala sitegemei kwamba kuna siku serikali yetu itaondoa somo la uraia kwa nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja! Masomo ya Historia na Civics Yanatakiwa kufundishwa katika hatua za awali baada ya hapo yaachwe.
 
Somo la History na Civics ndo naona la kuunganishwa linakuwa 'History and Civic Education'

Agriculture iwe lazima kama Bios
... we are slowly moving from agrarian to industrial society. It is projected that come 2100 Dar-es-Salaam alone will be home to more than 70 milion and more than 60% of Tanzania population will be living in cities. Halafu mnataka Agriculture liwe some la lazima! Mmefikiria sawa sawa kweli? Badala yake Entrepreneurship ndio inapaswa somo la lazima. YEHODAYA
 
Na kwenye literature watoe vitabu vya kina Onkokwo badala yake waweke Think big grow rich au rich Dad and poor Dad etc.
Unaonekana msomaji mzuri sana ,wazo lako naliunga mkono
 
... we are slowly moving from agrarian to industrial society. It is projected that come 2100 Dar-es-Salaam alone will be home to more than 70 milion and more than 60% of Tanzania population will be living in cities. Halafu mnataka Agriculture liwe some la lazima! Mmefikiria sawa sawa kweli? Badala yake Entrepreneurship ndio inapaswa somo la lazima. YEHODAYA
Looking at the indicators of development and if we take the models of development, our agriculture sector isn't yet mature to feed heavy industries /factories. Most of the farm products aren't full utilized, a lot is wasted in the farm to the consumers as we have little storage capacity and our people lacks these agricultural skills.
If we manage that, automatically industrial and entrepreneurship skills will diversify the two sectors.
Primitive society - Agriculture - industrial - developed society (high mass consumption)
 
... we are slowly moving from agrarian to industrial society. It is projected that come 2100 Dar-es-Salaam alone will be home to more than 70 milion and more than 60% of Tanzania population will be living in cities. Halafu mnataka Agriculture liwe some la lazima! Mmefikiria sawa sawa kweli? Badala yake Entrepreneurship ndio inapaswa somo la lazima. YEHODAYA
Nimeongelea vitu vitatu kilimo,ufundi na ufugaji population ikiwa kubwa mafundi.ujenzi, pikipiki ,magari,mafundi kupika watakuwa wengi kuanzia chips kuku etc ufugaji Kuku utapaaa consumption ya vyakula itakuwa juu no hizo kazi tatu zotatoa ajira
 
Back
Top Bottom