Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Na kwenye literature watoe vitabu vya kina Onkokwo badala yake waweke Think big grow rich au rich Dad and poor Dad etc.

By the way vile vitabu sijui lengo lake ni nini hasa.sijui kama vinasaidia kuandaa chochote au ni kufaulu mtihani tuu.

Nadhani serikali ingekuwa inaangalia mataifa mengine yanafundisha masomo gani.inawezekana tunafundisha vitu vilivyopitwa na wakati kabisa.

Kuna wakati huwa hata nadhani pengine taasis zinazolatibu mitaala ya elimu ni wavivu sana au ni watu wa zamani sana,kiasi mambo ya sasa ni magumu kwao kuelewa
 
Ulikurupuka mkuu haukufikira sawa sawa ,hayo masomo bado yana umuhimu mkubwa sana ila sipingi uwepo wa hayo masomo ya ufundi na Agriculture kikubwa ni kujiandaa vyema bila kukurupuka kama kuna umuhimu wa kuwepo .
 
kilimo ni uti wa mgongo hapa nchini
lakini cha ajabu halijapewa kipaumbele popote katk elimu ya awali hadi sec hahahaaaa
 
kilimo ni uti wa mgongo hapa nchini
lakini cha ajabu halijapewa kipaumbele popote katk elimu ya awali hadi sec hahahaaaa
Kuna tatizo kubwa Kama uti wa mgongo kilimo Cha kisasa kilitakiwa kuanza kufundishwa kuanzia chekechea mtoto anaanza kufundishwa kulima nyanya kisasa nk kuanzia kuandaa mbegu , kutengeneza kitalu na kumtaka mtoto apande haya nyanya moja nyumbani kwenye chungu Cha maua aitunze Hadi izae
 
Japo watanzania tunawalaumu viongozi wetu ila na sie tuna matatizo makubwa sana.
Imagine mtu kama wewe unatoa ushauri wa namna hii, je umewaza kwa mapama athari z hili jambo likitokea?
Tujifunze kutatua changamoto bila kusababisha changamoto zingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yasifutwe ila baadhi ya masomo kama geography na history waingizie syllubus ya hayo mambo
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Masomo ya O level kama Kiswahili, Civics na Historia yanapoteza tu muda watoto.

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na raslimali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaji vito vya madini,madini tunayo nk ili mtoto akimaliza Form Four awe tayari kukabiliana maisha.
Kwani hufahamu kuna somo linaitwa Stadi za kazi?
 
Kiufupi somo la history lingetolewa kabisa. Hebu nambie sasa history inafaida gani kwamaisha ya sasa? Yani unamtesa mtoto akariri miaka ya vifo vya watemi wakihistoria halafu akaaply wapi?. Duh hili somo lingeniona tumboni huku mpaka nataka kutapika
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Masomo ya O level kama Kiswahili, Civics na Historia yanapoteza tu muda watoto.

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na raslimali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaji vito vya madini,madini tunayo nk ili mtoto akimaliza Form Four awe tayari kukabiliana maisha.
Huoni prof kabudi anavotamba kwenye jukwaa,serikali Ni mfumo ambao unatakiwa kuwa na kila kitu ndo maana unakuta nchi Ina Hadi vichaa hao wote Ni government,Rudi nyuma pata ushauri
 
Huwezi kufuta masomo hayo katika elimu. nenda China wanafundisha lugha ya kichina, Uingereza wanafundisha lugha yao, ufaransa n.k. asiyejifunza historia ni mjinga Kwa vile hawezi kujua alikotoka Aliko na aendako. Hatusomi SoMo Kwa kuangalia interest ya mtu. Ukiona hayakufai soma yanayokufaa.
 
Back
Top Bottom