Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Pa Pamoja na kwamba wewe ni mpumbavu Sana kwenye siasa kwa hili nakuunga mkono.
 
Hiyo lugha ya Kiswahili akimaliza shule atatumia hiyo kama asset wapi ili apate pesa?
Hiyo civics ataitumia wapi ili ajiajiri aitumie imwingizie pesa?
Ndo akili ya mwafrika hii ilivyo, kama yako....Kwa hali hii wacha kozi zingine zisipatikane tu bongo,wenye uhitaji watazifuata South Africa na Northern hemisphere.
 
Hiyo lugha ya Kiswahili akimaliza shule atatumia hiyo kama asset wapi ili apate pesa?
Hiyo civics ataitumia wapi ili ajiajiri aitumie imwingizie pesa?
uko sahihi
Elimu Ni investment ambayo lazima upate return au faida kwa unayeyasoma ya moja kwa moja

Kuwekeza kwenye Kiswahili,Civics na Historia kwa watoto Wa O Level Ni uwekezaji mbaya na mbovu

Kundi Hilo kubwa la vijana likimaliza form four linatakiwa kuwa na skills za kujiajiri.
Elimu lazima iwe asset sio tu kujaza memory card ya akili za watoto kwa makorokoro yasiyowasaidia kwenye maisha wamalizapo form four Kama hayo madudu ya Kiswahili Civics na Historia.Yanajaza tu memory card za akili za watoto tu hayana faida kwenye maisha yao.
 
Yasiondolewe ila yawe na Pass ya Subsidiary km ilivyokuwa kwa BAM na GS.
Yanapotezea muda watoto .Wayasome primary tu anayeyataka kuendelea nayo akayoseme A level huko.ndio kuwe na hizo choice akitaka Civics , historia,au Kiswahili akaenedelee nayo huko yapishe masomo ya kilimo,ufundi na ufugaji ambayo Yana nguvu ya kutoa ajira kupitia kujiajiri
 
Zamani tulisoma sayansi kilimo,sayansi kimu......unafutaje somo la uraia mkuu? Unafutaje kiswahili? Historia nayo ni muhimu.....cha msingi ni kutengeneza nitalala bora tu
 
Sasa kiswahili kikiondolewa utawezaje kuandika yaondolewe? Wewe mwenyewe kuandika neno rahisi la Kiswahili yaondolewe umeshindwa umeandika "yaendelewe" ndiyo nini sasa hiyo?
Kuna watu wanajifanya wajuaji nchi hii hadi kero.
Hao waliyoyaweka wanazo akili kuliko wewe.
Kasome; how a subject qualify to be a discipline.
 
Yaani watu wanajifanya wajuaji wakati wenyewe ni mbumbumbu wa viwango vya hali ya juu.
 
Sasa kiswahili kikiondolewa utawezaje kuandika yaondolewe? Wewe mwenyewe kuandika neno rahisi la Kiswahili yaondolewe umeshindwa unaandika "yaendelewe" ndiyo nini sasa hiyo?
Kiswahili tunasoma miaka Saba primary pamoja na kuwa tunakiweza kukiongea mitaani hizo spelling mistakes kitu kidogo .
 
Hao waliyosomea mengineyo wameweza kujiajiri?
 
Na kwenye literature watoe vitabu vya kina Onkokwo badala yake waweke Think big grow rich au rich Dad and poor Dad etc.

Hivi onkokwo si ndo mwenye ile nyimbo ilofungiwa kenya inaitwa Utawezana?
 
Kiswahili tunasoma miaka Saba primary pamoja na kuwa tunakiweza kukiongea mitaani hizo spelling mistakes kitu kidogo .
Unajua implications za hayo masomo kuondolewa?
Kwani sasa hivi watu hawalimi?
Wanaolima na kuvuna wanapata masoko ya uhakika?
Kwenye soko la dunia, mazao/ malighafi kutoka Tanzania yanao ubora wa kushindana?
Hao wahitimu wa vyuo vya ufundi hawatengezi bidhaa kwa sasa? Na kama wanatengeneza bidhaa zao zinavutia soko?
Kwa nini kuna mlundikano wa bidhaa za kichina na mataifa mengine ya nje?
Hadi hapo tatizo ni kiswahili, Historia, & co?
Hadi hapo akili yako imeanza kufunguka?
 
Hao waliyosomea mengineyo wameweza kujiajiri?
Ndio waliosomea ya ufundi,kilimo na ufugaji kibao wamejiajiri lakini waliosoma kiswahili,historia na Civics wanazurura na vyeti barabarani hawajui Cha kufanya
 
Uko sahihi lkn Masomo hayo hayawezi kuondolewa ni muhimu sana tena sana. Labda ufikiri upya. Kilimo kitiliwe mkazo na wanafunz wafundishwe kitaalam na sio ilimradi tu.
 
Yasiondolewe ila yaongezwe,mwanafunzi achague mwenywe nini anataka kusoma,,,, lakinu hofu yangu kichwa kimoja mambo mengi kitamudu kweli
Suala la kuchagua ndio la msingi. Mtu unasoma masomo kumi, this is too much! Mi ningeshauri secondary watu wasome masomo yasiyozidi sita, yaani Kiswahili, English na Mathematics yanakuwa ni compulsory then mtu baada ya hapo anaweza chagua masomo mengine matatu ya kus-pecialize atakayoenda nayo hadi form six au chuo. Hii ianzie form one. Biashara, Kilimo, Sayansi ( Ningependa iwepo na Ufundi lkn na hakika facilities za kufundishia na uchache wa walimu itakuwa changamoto kubwa sana)
 
Tatizo kubwa kwa yote uliyosema nu watoto vichwa kupata Moto kwa kujazwa misomo isiyoamsha vichwa vyao kujiajiri na kufanya mambo kitaalamu unawajaza vichwa mi kiswahili,mi historia na mi Civics unapobteza nguvu za akili kwa kuwajaza mavitu ambayo sio basic need ya kuwasaidia wajitegemee.Wabafika huko juu vichwa vimechoka kwa kujaza mitakataka mingi isiyohotajika kwenye maisha yao ya kujitengemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…