Patrick Pas
New Member
- Oct 27, 2024
- 4
- 6
Habari ndugu zangu,
Naitwa Paschal, nipo Dar es Salaam, Kigamboni. Nimekumbana na changamoto ya kimatokeo, kwani inatakiwa niingie mwaka wa tatu katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Hata hivyo, naona kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kuendelea kutokana na somo moja la semester ya kwanza mwaka wa pili. Katika somo hili, nilipata "sup" lakini sikuridhishwa na matokeo hayo.
Hata hivyo, nilikubaliana nayo na kufanya "sup", kisha nikapata "retake". Hata baada ya kukata rufaa, matokeo yamebaki yaleyale, jambo ambalo linanihuzunisha sana kwani katika masomo mengine nilipata A na B+; ni hili tu ambalo linanikwamisha.
Kutokana na hali hiyo, inabidi nirudie mwaka wa pili. Hili limekuwa gumu zaidi kwangu kwa kuwa nina shida ya macho na wakati huohuo napambana sana kuendelea na masomo. Hivyo, itabidi mwaka huu nimalize semester ya kwanza na nisubiri hadi mwakani ili niweze kuendelea na mwaka wa tatu.
Hapa ndipo ninapokumbana na changamoto ya kifedha: nitapata wapi ada na hela ya kujikimu katika mwaka wa tatu, maana sasa hivi ninategemea mkopo ambao mwakani nitakuwa nimeshamaliza mkataba nao. Naomba ushauri na maoni yenu ndugu zangu, maana kwa kweli kichwa kinawaka moto kwa wiki nzima sasa.
Asanteni sana.