Masomo yangu chuoni

Masomo yangu chuoni

Patrick Pas

New Member
Joined
Oct 27, 2024
Posts
4
Reaction score
6
Habari ndugu zangu,

Naitwa Paschal, nipo Dar es Salaam, Kigamboni. Nimekumbana na changamoto ya kimatokeo, kwani inatakiwa niingie mwaka wa tatu katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Hata hivyo, naona kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kuendelea kutokana na somo moja la semester ya kwanza mwaka wa pili. Katika somo hili, nilipata "sup" lakini sikuridhishwa na matokeo hayo.

Hata hivyo, nilikubaliana nayo na kufanya "sup", kisha nikapata "retake". Hata baada ya kukata rufaa, matokeo yamebaki yaleyale, jambo ambalo linanihuzunisha sana kwani katika masomo mengine nilipata A na B+; ni hili tu ambalo linanikwamisha.

Kutokana na hali hiyo, inabidi nirudie mwaka wa pili. Hili limekuwa gumu zaidi kwangu kwa kuwa nina shida ya macho na wakati huohuo napambana sana kuendelea na masomo. Hivyo, itabidi mwaka huu nimalize semester ya kwanza na nisubiri hadi mwakani ili niweze kuendelea na mwaka wa tatu.

Hapa ndipo ninapokumbana na changamoto ya kifedha: nitapata wapi ada na hela ya kujikimu katika mwaka wa tatu, maana sasa hivi ninategemea mkopo ambao mwakani nitakuwa nimeshamaliza mkataba nao. Naomba ushauri na maoni yenu ndugu zangu, maana kwa kweli kichwa kinawaka moto kwa wiki nzima sasa.

Asanteni sana.
 
Hayo yote ulitakiwa uyajua kabla ya kuchukulia poa masomo yako...

Mimi kwa upande wangu nakushauri.

Soma hiyo Semester moja mwaka huu kwa mkopo kisha mwakani nenda katafute kazi Suma JKT umalizie chuo
 
Mambo ya carry over hayo yani kwa kozi za afya ukizingua somo tu unarudia mwaka, ila pole sana mkuu.
 
Hayo yote ulitakiwa uyajua kabla ya kuchukulia poa masomo yako... Mimi kwa upande wangu nakushauri... Soma hiyo Semester moja mwaka huu kwa mkopo kisha mwakani nenda katafute kazi Suma JKT umalizie chuo
Hamna kaka sikuwahi kuchukulia masomo poa nadhani kuna upepo mbaya tu umenipitia ila sina wa kumlaumu na sijilaumu, pia kwenda suma JKT sikupitia mafunzo ya JKT
Hayo yote ulitakiwa uyajua kabla ya kuchukulia poa masomo yako... Mimi kwa upande wangu nakushauri... Soma hiyo Semester moja mwaka huu kwa mkopo kisha mwakani nenda katafute kazi Suma JKT umalizie chuo
 
Namshukuru sana Mungu kanipigania hatimaye nimeweza kuondolewa hiyo retake nilikuwa na ufaulu mkubwa ila yalikuwa ni makosa ya mwalimu wa somo ila ndo hivyo walikula 50,000 yangu ya kukata rufaa, nashukuru hata kwenu wadau mliotoa ushauri hatimaye nimejua Mungu atabaki kuwa upande wangu daima na milele
 
Hayo yote ulitakiwa uyajua kabla ya kuchukulia poa masomo yako...

Mimi kwa upande wangu nakushauri.

Soma hiyo Semester moja mwaka huu kwa mkopo kisha mwakani nenda katafute kazi Suma JKT umalizie chuo
We jamaa Kila nkikuona nakumbuka jinsi ulivyotapeliwa na kalynda nacheka sana
 
Back
Top Bottom