Masoud Kipanya alimaanisha nini kwenye mchoro huu?

picha au michoro waweza kuwa na tafsri anuai kulingana na mtazamaji ila hiyo ni tafsri yako kuwa ni jpm ya kwangu mimi ni kuwa anacheza na mtoa roho ama mauti ambaye ni chama chake mwenyewe na ameishiwa move ndo maana amejiinamia
 
huyu kipanya ni mchochezi na anatumika vibaya kwa masilahi ya tumbo lake.
tuna muonya atumie vizuri taaluma yake, asilewe misifa! akajisahau.
 
Mwacheni tu atakamatwa soon kwa uchochezi maana ndio mashitaka yao pendwa , kuna watu wana sifa nchi hii nyie acheni tu
 
Wajane wa Mwendawazimu mna ”GUBU” mno. Mnajua kafa na kuoza lakini hamtaki kuamini😄😄
 
Aisee nimeona msokoto hapo kwenye hilo draft, weekend hii nangojea jioni nika-roll za kutosha nipoteze mawazo
 
Kwa kuichambua picha;hiyo skeleton iamevaa headphone nyekundu..rangi ya simba[emoji16] huku Kavaa kogia ya rangi ya CCM na yanga[emoji16],anavuta fegi huku akiwa amekunja nne.Pembeni kushoto chini ameweka bunduki(AK-47 ) .Ukiangalia hapo mezani kuna glass ya whiskey lkn ukiangalia kinywani kwake utagundua jamaa anakunywa damu na anaonekana kufurahia kabisa kinachoendelea hapo


Kwenye draft ameweka kalamu(ni km anacheza na kufundisha).Drafti Lina rangi ya yanga na CCM [emoji16]


Upande wa pili kuna mwanamke aliyevaa ushungi ambae anaonekana yupo ktk mchezo wa draft na hiyo skeleton lkn anaonekana amechoka sn Hadi kujiinamia na km amekata tamaa ya kuendelea na mchezo.Kitu cha ajabu kutoka kwake ni kwamba mikono yake ameota kucha km za mwewe au mnyama MLA nyama(predator)


Kuna kitu cha ziada kwenye hiyo picha nimekiona..ukimwangalia huyo skeleton ni km anacheka na kuongea maneno haya"mama nilikuambia enzi hizo ili ushinde huu mchezo unatakiwa uwe kauzu km nilivyokuwa Mimi.Ona sasa mchezo ulivyojushinda mapema sn hata mwaka haujamaliza"

Mama anatiwa moyo na mwalimu wake ambaye kiuhalisia hata yeye mwalimu mbinu zake ni km zilifeli na ndy maana yupi ktk state hiyo.. pamoja na kumiliki mititu ya bunduki na kuziba masikio na kunywa damu za watu alizoletewa na watu wasiojulikana lkn hakufua dafu..mama akatwe kucha!!


Sijui Nina maksi ngapi



Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mama anaweza acheze wapi hapo. Popote analiwa na vibwengo

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Majibu yapo hapa
 
Hiyo rafiki yako kaelewa kivyake
Wewe umeelewa nini?
Kumbuka
Rais wako anatakiwa kusukuma kete kwenye draft ya kijani
Anayecheza naye wala hana muda naye, anakula mziki na wine, ila ni skeleton!
Na pembeni yake ana mtutu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…