Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

Kwakweli inabidi kupelekana mahakamani kwa sababu uhuru wa kuongea haimaniishi kumchafulia mtu kwa kumtaja jina.

Mwenzake Doto Magari huwa anamponda mtu kwa mafumbo na hataji mtu, sasa huyu Mwijaku kajiamini kupitiliza, aisee ni hatari kumtaja mtu tena kwa jina hata kama kweli anafanya hivyo, akienda mahakamani anakufilisi.
 
Sijui msomi gani yule, unaeza toa tuhuma bila hata kutaja jina, ili iwe ngumu kutiwa hatiani sasa yeye msomi hata mitego midogo ya kisheria hajui,
Hapo sasa! Mwenzake Doto Magari kuna siku alikuwa anatoa shutuma "mme na mke mmeenda kudanga Dubai" bila kutaja jina ni nani, lakini wakati huo huo ni Mwijaku na Mkewe walikuwa Dubai!
 
B500 Masudi nae hayuko serious inakuwa kama kiki tu ya kuikuza Crown kwamba sasa watu wamfatilie Mwijaku akiwa Crown anasema nini kuhusu hilo huku clouds ikiendelea kufuatiliwa.
Basi Masudi naye atakuwa mjinga. Atengeneze kiki ya kujichafulia jina! Mimi mwenyewe binafsi nilipoona Masudi anatuhumiwa kufanya biashara haramu nilishtuka mana jamaa tangu nikiwa mdogo nilikuwa naziona katuni zake nikawa namuona mtu wa maana!
 
Hata kama nikweli huwezi kuwa na ushahidi wa kuthibitisha hizo tuhuma, Mwijaku ajifunze kuucha kuropoka.

Huyu kijana amekuja mjini hazijui code za watoto wa mjini, wamemshirikisha kidogo Tu kwenye mishe ameanza kushika hela anaropokaropoka aangalie asije akalala mazima.
 
Tutachukua Shea za mwijaku kwenye hilo gorofa you will see

Haiwezekani. Sheria zina loopholes nyingi sana kwenye kesi za madai

Ni sawa na nyumba ya urithi ukachukue shea ya mrithi kwa sababu unamdai. Haiwezekani.

Mali ya wanandoa huwa haiguswi na mtu ambaye si mwanandoa.

Hata mmoja awe anadaiwa trilioni bado mali ya ndoa haiguswi
 
Huyo Chawa naye amezidi kuropoka
Alipe billion 5 sasa Mdomo unaponza yale majisifu ya ghorofa ayaonyeshe kwa kulipa hio billion 5 kuonyesha kwamba yeye ni mwamba kwenye tasnia ya kuropoka ovyo kuhusu watu wengine alipokanyaga kakanyaga pabaya angeendelea kukanyaga kule kule kwa kina Baba Levo, Dotto Magari, Kurwa Magari, kuwakandia akina H Baba, Homoniza na mwenzie DearMonde wanaojuana huko ndicho yasingemtokea puani
 
Back
Top Bottom