Lethergo
JF-Expert Member
- Aug 7, 2023
- 6,534
- 11,421
Alisema Billion 1.3 km anayo mengine Manne basi atajipongeza kwa kuyapiga mnada ili alipe billion 5kwani lile orofa lake ni bei gani tuone kama tutapunguza deni.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alisema Billion 1.3 km anayo mengine Manne basi atajipongeza kwa kuyapiga mnada ili alipe billion 5kwani lile orofa lake ni bei gani tuone kama tutapunguza deni.
Billion 5 sio Billion 500 hio 500 umesema wewe labda umechafuliwa kwengine hukoB500 Masudi nae hayuko serious inakuwa kama kiki tu ya kuikuza Crown kwamba sasa watu wamfatilie Mwijaku akiwa Crown anasema nini kuhusu hilo huku clouds ikiendelea kufuatiliwa.
Mwijaku akiwa ameweka Billion 5 mezani au sio?Ila pia naona hizi shutuma zikiishia kwenye baraza la usuluhishi tuu maneno yasizidi kuwa mengi
Watakavyo ona wao ina faaMwijaku akiwa ameweka Billion 5 mezani au sio?
What a rubbish comment!!..Vipi mwijaku akisimama mahakamani na kusema Kipanya alikuwa akifanya biashara haramu ya kutangaza pombe kipindi cha maisha plus . Unywaji wa pombe ni hatari kwa afya za vijana wengi. Kidini upande wa uislam pombe ni haram
Amesema aje mezani na Billion 5 ushaelewa yaan wakitaka wayamalize nje ya MAHAKAMA asogee mezani na kibunda cha Billion 5 sio vinginevyoWatakavyo ona wao ina faa
Maana huyo aliye ongea inawezekana kabisa hajabahatisha na huyu aliyesemwa anajijua
HayaBillion 5 sio Billion 500 hio 500 umesema wewe labda umechafuliwa kwengine huko
Wale wanasiasa na hawa ni wasanii vijana kabisa.Kamuulize Musiba mbona uko kimya siku hizi?
KP kafanya kitu cha maana,waropokaji hawa wamezidi kisa tu kuna visenti wanapewa.Kwa mujibu wa Wakili wa Masoud Kipanya, amesema Mtangazaji huto maarufu kwasasa anapata shida kujitokeza mbele ya watu kutokana na tuhuma za kujihusisha biashara haramu zilizotolewa na Mwijaku
Hayo yamebainishawa na Wakili wa Mtangazaji Masoud Kipanya, Alloyce Komba kutoka kampuni ya Haki Kwanza Advocates ambapo amedai mmteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa mpaka kuna baadhi ya makampuni zimesitisha mikataba ya kufanya naye kazi.
Wakili huyo amemtaka Mwijaku kutoa ushahidi wa tuhuma hizo au alipe Tsh 5 Bilioni.
View attachment 3018050
View attachment 3018110
View attachment 3018111
Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba
Mchora katuni maarufu, Ally Masoud Nyomwa “Masoud Kipanya”, anakusudia kumshtaki Mahakamani na kumdai fidia ya Tsh. Bilioni 5, Burton Mwemba Mwijaku kwa madai kumkashifu na kuandika maudhui ya uongo dhidi yake katika ukurasa wake wa Mtandaoni wa Facebook ambayo pia yanadaiwa kusambaa kwenye kurasa nyingine.
Ikielezwa kuwa hali hiyo imesababisha kumshushia heshima na kupelekea baadhi ya taasisi kusita kufanya naye kazi mbalimbali.
Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ni Wakili wa Kipanya ameyasema hayo Juni 14, 2024, Jijini Dar es Salaam.
Wakili huyo akizungumzia suala hilo mbele ya Vyombo vya Habari anasema Mwijaku alitoa maneno ya uongo bila ushahidi, kwamba Kipanya anabiashara haramu na ambayo imechangia kuharibu vijana wengi.
Madai mengine ambayo Wakili anadai yalitolewa na Mwijaku ni kwamba Kipanya amezoea kuwazodoa viongozi wa Nchi na marais kwa kuwadhalilisha pamoja na madai Kipanya amekuwa akihongwa kuichafua Serikali na viongozi wake.
Wakili huyo amesema Kipanya kabla ya kuja mbele ya Vyombo vya Habari na Umma alimpa siku tatu Mwijaku kuomba radhi kwa uzito uleule aliotumia kumchafua sambamba lakini siku tatu zilipita bila kufanya alivyoelekezwa.
Anasema barua hiyo iliyoandikwa Juni 7, 2024 na kupokelewa siku tatu tokea siku hiyo, ilimwelekeza Mwijaku kujitafakari na kuomba radhi kwa maandishi kupitia mitandao yote aliyotumia.
Aidha, amedai licha ya uwepo wa taarifa inayodaiwa kuwa ni 'Press Release' iliyotolewa na Mwijaku amesema Mteja wao msimamo wake kwa sasa ni kwamba anaona kwamba njia pekee ya kutumika kumrejeshea heshima yake ni Mahakama.
Wakili huyo amesema madai ambayo yametolewa na Mwijaku dhidi ya Kipanya hayana ukweli wowote na kuwa yameendelea kumuathiri mteja wao ambaye amekuwa akifanya majukumu yake yanayogusa jamii kwa uchanya.
Amesema kwa kuwa madai hayo yanagusa mamlaka nyingine, ameeleza matarajio yao kwa Vyombo vya dola na taasisi nyingine zitakuwa zinachukua hatua, lakini amedai kwa upande wao pia wapo tayari kutoa ushirikiano kulingana na taratibu.
Amesisitiza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ambayo imefanyiwa marekebisho mara kadhaa, inatoa uhuru wa kujieleza lakini pia uhuru huo una wajibu.
Pia Soma:
- Mwijaku amwandikia Waraka Mzito Masoud Kipanya, adai anafanya biashara haramu
- Mwijaku amuomba msamaha Masoud Kipanya baada ya kumtuhumu kuwa “anafanya biashara haramu” na kutukana Viongozi akiwemo Rais
si ile nyumba yake 1.3B alisemaga auze aone kama atapata hata 200m bomboclaatAta 1% ya iyo hela Mwijaku hana.
Pombe haramu ,kiimani au kwa mujibu wa sheria za nchi? Kumbuka hii nchi haiongozwi kwa sheria za dini.Vipi mwijaku akisimama mahakamani na kusema Kipanya alikuwa akifanya biashara haramu ya kutangaza pombe kipindi cha maisha plus . Unywaji wa pombe ni hatari kwa afya za vijana wengi. Kidini upande wa uislam pombe ni haram
Ile nyumba ya 1B kweli?si ile nyumba yake 1.3B alisemaga auze aone kama atapata hata 200m bomboclaat
Mkakati wa kuzungumzwa huo mkuuNimeipenda hii , safi sana KP
Kwamba hy ni script?Mkakati wa kuzungumzwa huo mkuu