Hakika Mkuu, hapo kibonzo kinachagiza kuhusu uendeshaji wa shughuli za kisiasa nchini zilivyokinzana na matakwa ya katiba na sheria. Uwepo wa sheria mama yaani katiba, ni kama kichwa, ili kusimamia haki, uhuru, maadili ya vyama vya kisiasa kuendesha shughuli zao.
Mtu asiyekuwa na kichwa akiwa ameketi kitandani ni kasoro kubwa ya kimfumo kwa kulinganisha na haki za kikatiba huku rangi zilizopo kitandani, makopo ya rangi na ukutani ni chagizo kuhusu uwepo wa vyama tofauti vya kisiasa nchini vyenye sifa na nguvu tofauti.