Masoud Masoud, Manju wa muziki ni nani?

Wanatafutwa watu kama hawa wanawekwa pamoja na kutupa nini kifanyike kwa mziki wa Tanzania...
 
Nilimsikiliza alipokua anamuelezea marehemu Zahara nilimvulia kofia..ni kama unaangalia documentary kwny TV.....kumbe redio...
 
Zile bendi zetu za Zamani hivi kweli zipo kama ipo katika msondo na Sikinde.. Taarabu nazo zilikuja kipindi flani sijui nani anaziendeleza.. Singeli kwa mbaaali
Msondo bado ipo na inaongozwa na wanamuziki waliokuwepo. Zamani ilikuwa chini ya Chama Cha wafanyakazi.

Sikinde bado ipo na inaongozwa na wanamuziki waliokuwepo. Zamani ilikuwa chini ya DDC. Japo hapa kati kulitokea mzozo Kwa wanamuziki na kukapelekea mgawanyiko ambao ukaibua sikinde original ambayo inaundwa na wanamuziki wengine wa zamani waliokuwepo Sikinde.

Kwa ufupi Msondo na Sikinde zote zipo, Zinakabiliana na changamoto ngumu ya kizazi Cha Sasa hakielewi aina ya muziki wanaopiga.
 
Taarabu na Singeli zingeinuliwa hata tuingie kwenye Tuzo za Kimataifa..
 
Si tu muziki, jamaa znajua sana historia. Kuna kipindi fulani cha tbc around saa 11 jioni jamaa alikua anatoa historia ya Lumumba kama filamu hivi
 
Ukitaka record za vipindi vyake vya uchambuzi wa muziki inapatikana na anakutumia popote ulipo
 
Nilimsikiliza alipokua anamuelezea marehemu Zahara nilimvulia kofia..ni kama unaangalia documentary kwny TV.....kumbe redio...
Aisee kwenye hii na mimi nilimsikia... nikajisemea huyu Mzee Mosoud ni balaa kwa uchambuzi..utasikia mpaka mahojiano na watu kadhaa kumhusu Sahara...
 
Ha
Huyu Bwana kama angepata wadhamini au Serikali ikamsaidia kutekeleza Mawazo yake hasa tungeweza kuwa na pakuanzia, Wizara ya Utamaduni wangeona ni wapi huyu bwana anaweza kufiti na kuanzisha vionjo vya Music wa Tanzania
Hakika anajua muziki
 
Nimemsikiliza juzi akiuchambua wimbo wa Water wa Tyala na kwanini umeshinda tuzo huko America na kuwabwaga wanaigeria.
Huyu jamaa ANAJUA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…