DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mwigizaji Rose Ndauka na Msanii Lukamba wameeleza matamanio yao ya kumuona Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu akiachiwa na kushiriki shughuli za kisiasa kama ilivyokuwa hapo awali.
Kupitia mtandao wa Instagram Lukamba amechapisha picha ya Lissu akiambatanisha na maneno “Tunawaomba wakubwa tupeni na sisi haki yetu ya msingi Mtoeni Baba etu Ndani”
Katika andiko hilo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche amemjibu Lukamba akiandika “ Watu imara wanajisimamia, lakini watu imara zaidi wanasimama kwa ajili ya watu wengine, Mungu akubariki”
Kwa upande wa Ndauka Jana Oktoba 1, 2025 baada ya kuchapisha picha ya Lissu ameandika “Huyu jamaa ndio mpinzani wa kweli, atolewe tu. Hapa Siasa imeaanza kuwa tamu”
Hawa wanakuwa miongoni mwa wasanii maarufu wa mwanzo kwa siku za karibuni kujitokeza hadharani kuonyesha kumuunga mkono Lissu.