Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
Mkali wa wimbo ‘Bado’ Harmonize amefunguka na kuelezea harakati zake za muziki mpaka anafika kwenye mafanikio huku akiweka wazi jinsi alivyoambiwa hajui kuimba na Master J katika shindalo la BSS.

Muimbaji huyo ambaye alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuondoka na taji hilo, amesema baada ya kuambia hajui kuimba katika shindalo hilo alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba.

“Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo, the way nilivyokuwa naimba kwenye BSS, hata mimi ningekuwa ni jaji, ningesema wewe huwezi Walter Chilambo anaweza,” alisema Harmonize. “Sikupaniki kwa sababu toka nikiwa nje Master J aliambia tangu ukiwa nje nilikwambia no, kwa Master J alinichana kabisa hajui kuimba,”

Muimbaji huyo alisema kauli hiyo haikumkatisha tamaa kwani aliendelea kupambana na kutafuta njia yakutokea.

xharmonize-bongo.jpg.pagespeed.ic.HGSijcGNBT.jpg


“Mimi nilikuwa naimani moyoni mwangu, kwamba kuna siku Watanzani wataisikia sauti yangu, japo kuwa ukimwelezea mtu mwingine mimi nakipaji hichi, naimba anasema wewe hujui, Master akaniambia wewe hujui, lakini kwa mtazamo wake alikuwa sahihi kwa sababu the way nilivyokuwa naimba hata kama ningekuwa jaji ningejitoa. Lakini mimi moyoni mwangu nilikuwa nasema ninakitu fulani, sikukata tamaa nikaendelea kufanya muziki mzuri na kweli Mungu ameniona sasa hivi nimesikika,”

Pia alisema alikuwa anahudhiria show mbalimbali ili kujifunza jinsi ya kuperfom katika matamasha mbalimbali.
 
Master J anao mtizamo hasi kwa wanamuziki wenye sauti kama Harmonize. Sio yeye pekee aliokumbana na hiyo kadhia, wapo wengi ila walijitahidi na wakatoka. Nakumbuka kuna mwanamuziki kutoka Tanga nae aliambiwa hajui kuimba ila alitoka. Na ukumbuke kipindi hicho studio zilikuwa chache na wote walikuwa wanalimiliki soko la muziki, ila huyo Bwana alipenya. Kwa ujumla hukumu ya Master J isiwafanye vijana wakakata tamaa.
 
mhuuuuuu[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji15] [emoji15]
 
duh Dogo akipita hapa naamini na nyie atawachana kwenye vyombo vya habari kua mmemwambia hajui
 
hujui kuimba Bob unamwiga boss wako basi kama vipi kachonge vinyago umakondeni au ukaungane na wamakonde wenzako kufanya uchinga manake siku si nyingi wabongo watakutema kwa style za kucopy....nimtazamo tu naomba tusitafutane
 
Master J anao mtizamo hasi kwa wanamuziki wenye sauti kama Harmonize. Sio yeye pekee aliokumbana na hiyo kadhia, wapo wengi ila walijitahidi na wakatoka. Nakumbuka kuna mwanamuziki kutoka Tanga nae aliambiwa hajui kuimba ila alitoka. Na ukumbuke kipindi hicho studio zilikuwa chache na wote walikuwa wanalimiliki soko la muziki, ila huyo Bwana alipenya. Kwa ujumla hukumu ya Master J isiwafanye vijana wakakata tamaa.
mkuu kwa mtu yoyote aliefuzu sound engineering mtu mwenye kuimbia puani kama huyu hawezi kuwa mwimbaji mzuri kwake tena huyu bahati yake siku hizi studio zipo mpaka vichochoroni enzi zile angeishia kuuza madafu na kahawa mziki angebaki kuwa msikilizaji tu
 
Back
Top Bottom