Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Kwa master j anayejua kuimba ni sarah kaisi....huko kwenye mashindano hawezi kuiona chochote wakati sugua gaga ipo kichwani....joking
Master Jay amesomea mambo ya music kwahyo hajakulupuka
 
Katika mtazamo wa mtaalamu wa muziki ni kweli mdogo wangu hujui kuimba.
Ila kwa mtazamo wetu sisi ambao tunaangalia mashairi na mdundo unajua sana.
Hii haibadilishi ukweli kuwa hujui kuimba.
 
Kifesi mfikishie salaam hizi harmonize toka JF nahis atalia na atawatungia watu wa umu nyimbo [emoji28][emoji28]
 
hakuna anayemuonea wivu, hongera kwa mafanikio aliyofikia mpaka sasa, lakini ukweli unabaki palepake hajui kuimba... na sio mbunifu, anachofanya ni kucopy kwa boss wake.
Wanafanya biashara na boss wao kawaambia lazima wafatishe vile ye anaimba. siku domo akianguka hawa wote wanaingia mtaani kuuza vyupi.
 
Samahani Mzee je uliwahi kumsikia Suleiman Mbwembwe? Au Hemed Maneti? Au Hassan Rehani Bitchuka? Wote hawa ni watu waoghani sauti zao kwa kutumia sauti ya kwanza au ya pili, mbona wamekuwa ni magwiji wa muziki? Tatizo lipo kwa mahaba ya sauti.
Unawakumbuka Mopero na Josky Kiambukuta. Kuna watu walikuwa ni wapenzi wa Mopero kwa kuwa alikuwa na sauti nene, lakini ukimsikia Kiambukuta yeye alikuwa na sauti kali. Ingawa Mwawaita wabana pua, lakini wanafanikiwa kuteka nyoyo za watu wengi.
Najaribu kumuangalia jinsi King Crazy GK anavyohangaika na muziki wake wa Rap. Pia nikiangalia soko la wanamuziki ambao walikuwa wanasimamiwa na Master J wanavyohangaika kutoboa kwenye soko gumu la muziki wa leo, siipati picha. Ila mahaba ya sauti yasifanye wasimamizi wa muziki kuwaponda baadhi ya vijana, kwani kila binaadamu ameumbwa na bahati yake.

dooooh kweli mziki umeingilia kwa hiyo Suleiman Mbwembwe aka masharubu na Hassani Rehan Bitchuka walikuwa wanaimba kwa kubana pua kama anavyoimba Harmonise?!
Acha kufananisha Barcelona na Mbao fc ya mwanza eti kisa zote ni timu za mpira wa miguu
Au wewe ndio bwana Sallam S.K?!
 
Mkali wa wimbo ‘Bado’ Harmonize amefunguka na kuelezea harakati zake za muziki mpaka anafika kwenye mafanikio huku akiweka wazi jinsi alivyoambiwa hajui kuimba na Master J katika shindalo la BSS.

Muimbaji huyo ambaye alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuondoka na taji hilo, amesema baada ya kuambia hajui kuimba katika shindalo hilo alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba.

“Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo, the way nilivyokuwa naimba kwenye BSS, hata mimi ningekuwa ni jaji, ningesema wewe huwezi Walter Chilambo anaweza,” alisema Harmonize. “Sikupaniki kwa sababu toka nikiwa nje Master J aliambia tangu ukiwa nje nilikwambia no, kwa Master J alinichana kabisa hajui kuimba,”

Muimbaji huyo alisema kauli hiyo haikumkatisha tamaa kwani aliendelea kupambana na kutafuta njia yakutokea.

xharmonize-bongo.jpg.pagespeed.ic.HGSijcGNBT.jpg


“Mimi nilikuwa naimani moyoni mwangu, kwamba kuna siku Watanzani wataisikia sauti yangu, japo kuwa ukimwelezea mtu mwingine mimi nakipaji hichi, naimba anasema wewe hujui, Master akaniambia wewe hujui, lakini kwa mtazamo wake alikuwa sahihi kwa sababu the way nilivyokuwa naimba hata kama ningekuwa jaji ningejitoa. Lakini mimi moyoni mwangu nilikuwa nasema ninakitu fulani, sikukata tamaa nikaendelea kufanya muziki mzuri na kweli Mungu ameniona sasa hivi nimesikika,”

Pia alisema alikuwa anahudhiria show mbalimbali ili kujifunza jinsi ya kuperfom katika matamasha mbalimbali.
Master J hakoseagi akisema no , he means it, hajui kweli kuimba labda kucopy na kupaste hivo anajua
 
Mkuu, hisia zako hazijaguswa? Basi huenda ndio kwanza unabalehe/kuvunja ungo... Ngoja umri usogee sogee uanze kutendwa ndio nyimbo kama hii itakuingia vizuri...
kwa hiyo hizo nyimbo zake mpaka utendwe kama wewe ulivyotendwa na demu wako ndio zinakuwa tamu?!
 
Namkubali sana tena sana harmonize anajua anachokifanya anajua kuimba mpaka anaboa ya ni ile sauti ni adimu mpaka imemshinda simba bosi wake..... Big up harmonize kaza buti usikatishwe tamaa na wanafki wachache wanaokuzikilizs kila unapotoa hits song afu wanajifanya kukuponda kwenye social media honestly your the best singer.
Kupatwa kwa mahaba
 
Back
Top Bottom