Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Anajua tu kumkop boss wake na kula makombo yake
 
anajua bwana acheni roho mbaya jamani..
angekua hajui asingehit.
alafu kwanini hamfurahii mafanikio ya wenzenu???
Mi simjui ila kuna muziki fulani clouds wanajaribu kuulazimisha upendwe ijapokuwa naona kama hauna thamani ya kuitwa muziki wao wanasema singeli.Kama ni wa dizaini hiyo ya kubebwa nadhani anatakiwa kufanya bidii zaidi.Nitafuatilia nione kama kweli anajua.
 

watu mnadhambi!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pole harmonizer!!!!
 
anajua bwana acheni roho mbaya jamani..
angekua hajui asingehit.
alafu kwanini hamfurahii mafanikio ya wenzenu???
Umeongea ukweli. Kuna watu wana roho ya kwanini. Hata Master J. Ukimuuliza leo atakubali kuwa dogo Hivi sasa anajua. Hakujua kuimba miaka hiyo, lakini hivisasa anajua.
 
Chacha mimi chijui nichemeje?
mimi naona kama huyu dogo hajui chochote.
Ukweli uwe wachi ili uichi kwa amani.Chiwechi Kumchiliza Harmonaiche hata kiduchu.
 
hakuna anayemuonea wivu, hongera kwa mafanikio aliyofikia mpaka sasa, lakini ukweli unabaki palepake hajui kuimba... na sio mbunifu, anachofanya ni kucopy kwa boss wake.
Unasimamia Ushahidi upi kusema hayo? Kama umempa hongera kwa mafanikio ni kwakuwa unajua kafanikiwa. Na amefanikiwa kwakuwa anajua anachofanya. Kabla hajajua kuimba hakufanikiwa, sasa amejua amefanikiwa. Ila wewe tu humpendi kwa sababu zako ndiyomaana unasema hajui. Dogo amejitahidi kujua, ameweza kujua.
 
Tena mwambie awe na heshima kwa hao wazee aliowataja...

Yaani hii mikelele ya hamonaiz ni muziki??? sasa akina maurice kiria wa Uganda tuuitaje??
 
Watu wana roho za kwann sana 4sure wana wivu waajabu ebu Iga na ww kama ata mama ako ataisikilza tusiwe ivo bhana ebu isikilize matatizo Afu utajua
 
Huyu wakuja mtupu kabisa, diamond kamchukua kibiashara ilienda wale wenye dau dogo anawapelekea huyo dogo wahangaike nae
Siyo kweli. Wewe jaribu kupunguza chuki na wivu kidogo, kisha sikiliza sauti ya huyu dogo. Dogo anastahili pongezi kwa juhudi zake. Diomond anajua biashara, anajua nini wapenzi wa muziki wanahitaji ndiyomaana dogo yupo pale
 
kina shirima wanachonga humu,mmesahau kila watu kuna walichojaaliwa?mbona nyie ni wezi maarufu ila tumenyamaza?
 
Katika mtazamo wa mtaalamu wa muziki ni kweli mdogo wangu hujui kuimba.
Ila kwa mtazamo wetu sisi ambao tunaangalia mashairi na mdundo unajua sana.
Hii haibadilishi ukweli kuwa hujui kuimba.
Hivi mtazamo wa anayejua muziki ndiye nani?!! Kazi za sanaa ni bidhaa kama bidhaa nyingine. Kama mtu anatengeneza bidhaa inayokubalika sokoni na haina madhara, basi hiyo no bidhaa nzuri. Uzuri wa bidhaa unahusu Mambo mengi, kama vile ubora, unafuu wa bei,nk. Hivyo soko ndilo linasema Ipi ni bidhaa nzuri. Dogo anakubalika na Mashabikia, sasa huyo mtaalamu wa muziki ana nafasi gani hapa. Na hata hao anaowakubali yeye mbona wanahaha kupenya kwenye soko bila mafanikio. Master J ni mtaalam wa muziki aina ya HIP Hop siyo aina zote. Hivyo aina nyingine zote yeye si shabiki wake.
 
Mahaba yakizidi chongo linakua kengeza mkuu.
 
Watu wana roho za kwann sana 4sure wana wivu waajabu ebu Iga na ww kama ata mama ako ataisikilza tusiwe ivo bhana ebu isikilize matatizo Afu utajua
Ndo mana utuoni huko kama wao kwakua tumekubali kuwa hatuwezi. Lkn sio sababu ya waliopo huko kujifanya matawi wakati baaado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…