Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

dooooh kweli mziki umeingilia kwa hiyo Suleiman Mbwembwe aka masharubu na Hassani Rehan Bitchuka walikuwa wanaimba kwa kubana pua kama anavyoimba Harmonise?!
Acha kufananisha Barcelona na Mbao fc ya mwanza eti kisa zote ni timu za mpira wa miguu
Au wewe ndio bwana Sallam S.K?!
Samahani Mzee, mimi sio kabisa Sallam SK.
 
wote mnaomponda huyu dogo,najua sio nyinyi binafsi mnaoongea bali ni chuki ndo zinaongea kupitia nyinyi...envy n jealous speak through you!
 
Naona watu wana mgandia kwmb bado hajui kuimb duh,tumtie moyo kijan jamani...kwni alikotoka mbali...na anahitaji support afikie mafanikio ya boss wake...pia binafsi najiulizaga maswali juu ya mashindan ya kusaka vipaji..ni kwann washindi wa mashindao hawawagi masupestar sana...lkn contestant ndio wng huibuka kuw mastaa..!?
 
Bado hajui anamkopi diamond kidogo ina mbeba
 
Dogo anabebwa na level yake tu ya diamond lakin yule yeye kama yeye asingeweza kutoboa hamna kitu pale
 
Umeongea ukweli. Kuna watu wana roho ya kwanini. Hata Master J. Ukimuuliza leo atakubali kuwa dogo Hivi sasa anajua. Hakujua kuimba miaka hiyo, lakini hivisasa anajua.
kuimba ni sauti, juhudi ,utunzi
lakini watu wanaonekana hawajakubaliana na mafanikio ya huyu bwana
 
sasa unaanzaje kumfananisha fundi Hassan Rehan Bitchuka na vitu vya Kijinga Jinga?!
Alivyoanza muziki Hassan Rehani Bitchuka alizogomwa sana na alionekana anaimba kwa kutumia pua. Hawakumkubali haraka, hata TX Moshi William alikumbana na hiyo kadhia, ila taratibu walizoeleka na wakawa ni watu wenye heshma kwa wapenzi wa Msondo.Ukumbuke ile Msondo ya kipindi kile ilikuwa ni ya wandava na magangwe wa mjini.
 
aiseee kwanza tuulizane umri...yaani kabisa bado umeng'ang'ania kuwa Harmonise anaimba kama walivyokuwa wakiimba wakina Hassan Rehani au TX Moshi William?!
wallah mimi mwanzo nilijua unafanya dhihaka tu
 
Hao wooote ninaowataja nimewaona wakiimba mubashara. Mzee ungekuwepo pale Bwalo la Polisi, Kigongo Bar au Kwetu Bar ungenielewa uzuri haya ninayoyasema
 
sema nimegundua kitu. Kuna watu huwa wanasoma heading tu halafu wanarukia kucomment....
 
Samahani Mzee je uliwahi kumsikia Suleiman Mbwembwe? Au Hemed Maneti? Au Hassan Rehani Bitchuka? Wote hawa ni watu waoghani sauti zao kwa kutumia sauti ya kwanza au ya pili, mbona wamekuwa ni magwiji wa muziki? Tatizo lipo kwa mahaba ya sauti.
Unawakumbuka Mopero na Josky Kiambukuta. Kuna watu walikuwa ni wapenzi wa Mopero kwa kuwa alikuwa na sauti nene, lakini ukimsikia Kiambukuta yeye alikuwa na sauti kali. Ingawa Mwawaita wabana pua, lakini wanafanikiwa kuteka nyoyo za watu wengi.
Najaribu kumuangalia jinsi King Crazy GK anavyohangaika na muziki wake wa Rap. Pia nikiangalia soko la wanamuziki ambao walikuwa wanasimamiwa na Master J wanavyohangaika kutoboa kwenye soko gumu la muziki wa leo, siipati picha. Ila mahaba ya sauti yasifanye wasimamizi wa muziki kuwaponda baadhi ya vijana, kwani kila binaadamu ameumbwa na bahati yake.
dah mkubwa mwenzangu kula tano.. kumbe unamkumbuka seleiman mbwembwe.. huyu jamaa alikua ni hatari sana kwa bongo fleva ya sasa hukuna anayemnusa kwa sauti.. pia Hassan rehani bitchuka aka stereo.. hii ni machine kubwa huyu mzee ni fundi na angekua kijana enzi hizi ndio angekua nguli wa muziki huyu mzee anajua ku-balance sauti nakiri hapa bongo kwa muziki wa kale hajawahi kutokea fundi wa muziki na mtaalam wa kubalace sauti kama huyu mzee..
 
dooooh kweli mziki umeingilia kwa hiyo Suleiman Mbwembwe aka masharubu na Hassani Rehan Bitchuka walikuwa wanaimba kwa kubana pua kama anavyoimba Harmonise?!
Acha kufananisha Barcelona na Mbao fc ya mwanza eti kisa zote ni timu za mpira wa miguu
Au wewe ndio bwana Sallam S.K?!
daah seleman mmbembe R.I.P na Bitchuka aka stererio ni mafundi na sauti zao kama unavyozisikia kwenye redio ndio hivyo hivyo wakiimba live zinatoka.. hawa madogo wa saivi wakiimba live ni kichekesho sauti zao zinatengenezwa studio.. kifupi mziki wa saivi ni ujanja ujanja na video kali na promo ya nguvu.... MZEE BITCHUKA WEWE NI NGULI SALUTI KWAKO..
 
Duh! Nyie ndo wabongo haswaaaa, hapa ndo nimejua kuwa umaarufu ni jalala ...yaan mchz anajikunja studio atoe ngoma nzuri lkn majitu yalipotoka yanadiss tu hajui hajui kwan nyi mmebeba na maskio ya watu wengne au ? Eb punguzen chuki km hajui au anajua wasikilizaji kila mmoja kwa binafsi yake atajudge ila siyo kupandikizana chuki na wengn watajikuta wanamchukia tu bila sababu
 
Hata prof. Arsene Wenger alimwambia Yaya Toure ktk trials kuwa hajui soka. Ferguson akamwambia Veron hajui soka. Huwa inatokea.
 
Back
Top Bottom