Samahani Mzee je uliwahi kumsikia Suleiman Mbwembwe? Au Hemed Maneti? Au Hassan Rehani Bitchuka? Wote hawa ni watu waoghani sauti zao kwa kutumia sauti ya kwanza au ya pili, mbona wamekuwa ni magwiji wa muziki? Tatizo lipo kwa mahaba ya sauti.
Unawakumbuka Mopero na Josky Kiambukuta. Kuna watu walikuwa ni wapenzi wa Mopero kwa kuwa alikuwa na sauti nene, lakini ukimsikia Kiambukuta yeye alikuwa na sauti kali. Ingawa Mwawaita wabana pua, lakini wanafanikiwa kuteka nyoyo za watu wengi.
Najaribu kumuangalia jinsi King Crazy GK anavyohangaika na muziki wake wa Rap. Pia nikiangalia soko la wanamuziki ambao walikuwa wanasimamiwa na Master J wanavyohangaika kutoboa kwenye soko gumu la muziki wa leo, siipati picha. Ila mahaba ya sauti yasifanye wasimamizi wa muziki kuwaponda baadhi ya vijana, kwani kila binaadamu ameumbwa na bahati yake.