Masters voice prophecy: Mtumishi wa Mungu wa kike wa USA ameoneshwa na Mungu kuwa USA itapingwa na Urusi

Hawa wengine tunawajua wanakuwa na matakwa fulani, halafu wanasingizia Mungu kawaonesha.

Ukimtaka athibitishe huyo Mungu yupo, hawezi kuthibitisha, ataishia kukupa longolongo nyingi tu.
Kwani kila unachoshindwa kuthibitisha uwepo wake ndio hua hakipo?
 

Urusi huo ni mtego muuepuke
 
Wewe mbona unaleta tena porojo za masjid ubwabwa ❓ Hicho kitabu cha John Tazama ndicho kitabu gani ❓
 

Ana track record kama ya Baba Vanga au Nostradamus ?
Hao manguli wana rate kubwa sana ya utabiri wao kuwa sahihi , mfano huyo Baba Vanga mpaka aliyotabiri mwaka huu kuna ambayo yanatokea tayari
 
Wewe mbona unaleta tena porojo za masjid ubwabwa ❓ Hicho kitabu cha John Tazama ndicho kitabu gani ❓
NI yule aliye tunga kitabu cha bibilia Apostle John, au humjui dogo 😄
 
Kwani kila unachoshindwa kuthibitisha uwepo wake ndio hua hakipo?
Hapana,

Lakini, uthibitisho ndiyo njia pekee ya kuhakiki kitu kipo au hakipo.

Zaidi, pingamizi langu kwamba Mungu hayupo haliishii tu kwenye uthibitisho.

Dhana ya kuwepo Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliyeumba ulimwengu huu unaoweza kuwa na mabaya, inajipinga yenyewe, ina internal contradictions.

Kwa sababu, Mungu huyo kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya ni contradiction.

Mungu huyo kuwapo na ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwapo ni vitu viwili vilivyo mutually exclusive, yani, kinaweza kuwepo kimoja ama kingine, haviwezi kuwapo viwili vyote.

Maana yake ni, ikiwa Mungu huyo yupo, basi ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo haupo.

Na, ikiwa ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, Mungu huyo hayupo.

Tunaona ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.

Hivyo, Mungu huyo hayupo.
 
Inawezekana kama Osama jeshi la mtu mmoja liliweza kupiga USA , nchi za NATO zimelemazwa na demokrasia na huku nchi zao zinateketea umakini wao kwenye kuzuia adui ni mdogo sana ukilinganisha na Rusia,na China. Israel taifa makini na wao wameanza kulala kama mataifa ya NATO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…