ITR
JF-Expert Member
- Sep 22, 2022
- 6,096
- 16,390
Kwani Israel imeanza kuuwa na kutesa wapalestina baada ya hiyo October 7?Unaikumbuka October 7? Unaunga mkono mashambulizi waliyofanya Hamas?
Tukio la October 7 ni matokeo ya vitendo vya Israel viovu na visivyo vumilika dhidi ya wapalestina, katibu wa umoja wa mataifa alisha lisema.
Hata wanasiasa ndani ya Israel yenyewe wanakili kuwa sera za kikatili za Netanyau dhidi ya wapalestina ndo zimechochea shambulizi hilo.
Na Israel isipo badilisha sera yake dhidi ya wapalestina basi jua matukio haya yataendea sana tu miaka ijayo maana hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye anaweza kuvumilia mambo yanayo fanywa Israel dhidi ya wapalestina.
%70 ya wapalestina wanaishi kwenye kambi za wakimbizi baada ya kufukuzwa kwenye nyumba zao na mashamba yao na serikali ya Israel na kuwapatia walowezi wa kiyahudi wanao hamia nchini humo kutoka sehemu mbali mbali duniani.
Maeneo yote yaliyo shambuliwa na Hamas October 7 na maeneo yote yanayo itwa kusini mwa Israel ni maeneo ya wapalestina walifukuzwa na wakaenda kuwarundika hapo gaza hivi hata kama ungekuwa ww ungeweza kuvimilia mambo ya aina hiyo?