Maswali 100 ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022

Maswali 100 ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022

Ilo swali la 3 la kiwaki sana.

Je, wewe ni mwanaume au mwanamke?

Like SERIOUS?
Yes like serious kwa sababu maswali Kama hayo ndio watoa hela za sensa huko majuu wanauliza yaani wewe ndio useme Kama me au ke au transgender
 
Maswali mengi yanaingilia faragha za watu . Mfano mdogo ni huu :

62. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, Je, ulimiliki au ulitumia vifaa vifuatavyo?
  • Simu janja/Kishikwambi
  • Simu ya kawaida
  • Kompyuta ya mezani (Desktop)
  • Kompyuta mpakato
63. Je, ulitumia kifaa hicho katika matumizi yapi?
Majibu ya maswali ya 62 hadi 63 yataiwezesha Serikali kupata taarifa za asilimia ya watu wanaomiliki na wanaotumia vifaa vya TEHAMA. Aidha, Serikali itaweza kupata taarifa za matumizi makuu ya vifaa hivyo vya TEHAMA kama vile kuwasiliana, kutafuta/kupokea taarifa kwa ajili kuboresha zaidi huduma hizo
 
Yes like serious kwa sababu maswali Kama hayo ndio watoa hela za sensa huko majuu wanauliza yaani wewe ndio useme Kama me au ke au transgender
You're very right!

Hili swali limelenga kujua idadi ya transgender.
 
Nimeona utitiri wa maswali.

Hao waandaa hilo dodoso sijui waliwaza nini, yaani mimi na uzee huu nikae mtu ananiuliza maswali zaidi ya mia, siwezi.

Labda kuwe na posho ya wakuu wa kaya.
Hutaulizwa maswali yote. Mfano swali la 30, hutaulizwa. Maswali ya fertility 68 hutaulizwa maana wewe ni zaidi ya miaka 49.
 
Yes like serious kwa sababu maswali Kama hayo ndio watoa hela za sensa huko majuu wanauliza yaani wewe ndio useme Kama me au ke au transgender
Masikini, hili ni swali muhimu sana na makosa yake yanaitwa sex error. Tunapata uwiano kati ya wanaume na wanawake. Kila swali lazima liulizwe, ila uulizwaji ndiyo tofauti. Usisahau siku hizi wanaume wengine wanasuka, wanatoga masikio hata hereni wanavaa.
 
Naona kama maswali 100 n8 mengi sana watwaweza kuuliza yote na kufikia nyumba zote.
 
Nimeona utitiri wa maswali.

Hao walioandaa hilo dodoso sijui waliwaza nini, yaani mimi na uzee huu nikae mtu ananiuliza maswali zaidi ya mia, siwezi.

Labda kuwe na posho ya wakuu wa kaya.
Mimi hawatonikuta kabisa kesho, hayo maswali Kama Kibatala anamuhoji Shahidi wa jamuhuri siwezi kuyajibu, maana ntakuwa hoi
 
55. Je, unajishughulisha na shughuli ndogo ndogo zisizo rasmi/machinga?56.Je, ni ipi shughuli kuu ya kiuchumi unayofanya?
Mkuu Influenza , asante sana kwa maswali haya, Haya ni maswali muhimu sana kwa wale wenzetu wanajishughulisha na ile biashara, the oldest professional kuendesha maisha yao!.

Niliwahi kushauri biashara hii irasimishwe kwasababu ndio inayoongoza kuajiri watu wengi zaidi kuliko ajira nyingine yoyote popote duniani!.

P
 
Wanataka namba za simu kwa ajili ya 'ile pesa itume huku simu yangu imeharibika na kutuma meseji za kampeni 2025"
 
Kwa maswali haya, Makarani wajiandae vizuri. Maana watakutana na vichwa vingine vilishajichokea kitambo. Hapo lazima mtu ale bonge la tusi hata kabla ya kuanza kuuliza maswali.
 
Back
Top Bottom