Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 817
- 881
Ikiwa Bunge la Ulaya wanajiona wanahuruma na wapo tayari kubeba misalaba ya mataifa mengine, basi eem, tujiulize yafuatayo:
1. Ni nani hasa wameizuia CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania? Je, kuna ushahidi wa kisheria au ni maneno ya kisiasa yasiyo na msingi wa kikatiba?
2. Kwa kutumia msingi upi wa kisheria au mkataba gani wa kimataifa, Bunge la Ulaya linajipa mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, taifa huru linalojiongoza kwa mujibu wa katiba yake?
3. Bunge la Ulaya lina mamlaka gani au dhamana ipi ya kuipigania Tanzania kana kwamba Watanzania hawana uwezo wa kujitetea wala kujiamulia mustakabali wao?
4. Tokea lini Tanzania, kama taifa huru, imekuwa ikiingilia na kujadili masuala ya ndani ya nchi za Ulaya ndani ya mabaraza yake ya kisheria au ya kisiasa?
5. Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina?
6. Kwa nini Bunge hilo hilo halikai kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, jambo ambalo linaendelea kutikisa dunia na kusababisha madhara makubwa kwa raia?
7. Kwa nini pia wasikae kujadili ukandamizaji na unyonyaji wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kampuni nyingi za kimataifa zenye makao yao Ulaya zinatajwa kunufaika?
8. Je, Bunge la Ulaya linaamini katika misingi ya utawala wa sheria? Na iwapo jibu ni ndiyo, je, linaamini kwamba kila mtu yuko sawa mbele ya sheria na hakuna aliye juu ya sheria, ikiwemo wao wenyewe?
Mwisho, naomba wajifungie kuijadili Marekani na Udikteta wa Trump, alafu na sisi walau kidogo tutajua walau wanaouchungu na mataifa ya Afrika.