Maswali fikirishi juu ya uuzwaji wa dhahabu yetu

Waweke wazi tu na waseme wanaiuzia financial hub gani?
Kama watauza kinyemela
Wajuavyo wao bila kuwataarifu wananchi/raia
Basi ni yao binafsi wafanye

Ova
 
Na kibaya zaidi sisi watawaliwa hatujui hata hiyo akiba iko kiasi gani na ilikuwa kiasi gani hapo kabla. basi litakalo tokea litabakia mioyoni mwao na wanao lisimamia hilo ili walifanikishe.
 
Kama Bandari tu, watu walitangaziwa wakati dili kishafanyika. Bongo ukisikia serikali imetoa taarifa kama hizo ujue jambo lishafanyika zamani tu, hapo wanatoa taarifa tu ndo maana hata mlalamike vipi huwa jambo halibadiriki sababu tayari limeshaisha.Hapo tutapiga tu kelele na kushauri kitu kilichofanya tayari,haisaidii na wala haibadirishi kitu kwakweli.
100%
 
Wameshakanusha.. Wanasema zinazouzwa ni zilizozidi kiwango cha hifadhi😭
 
Ukiona manyoya ujue ndege ashaliwa.
🥺🥺🥺
IMG-20260130-WA0040.jpg
 
LWAKOLWA...Imekwisha Uzwa Siku Nyingi Habari Tu Imechelewa Kutoka..Ipo Kwa Wajomba Huko....NYANTAKO Zao...!!!
 
Huenda zilishuka bei, Wafipa wamezinunua kwa mkopo. Juni zikipanda bei, Wahehe watazinunua tena kwa bei ya juu. Mkopo utalipwa na cha juu!
 
HIVI UMEWAHI KUJIULIZA
1. Dhahabu ni ya kwetu(Tanzania) halafu TUNANUNUA Dhahabu.
Sasa Tunanunua kutoka kwa Nani?

2. Kwa mwaka juzi pekee 2024 Madini ya dhahabu yaliyochimbwa Tanzania ni Takriban Tani 60. NARUDIA TENA TANI 60 KWA MWAKA MMOJA TU, Yani Kilogram 60,000. Ila Dhahabu yote inayomilikiwa na Bank Kuu ya Tanzania(BOT) tangu tupate uhuru 1961 ni kama Tani 18.9 tu. Yani hata tani 20 hatuna, HII INAWEZEKANAJE?

3. Wanataka kusema, Dhahabu TUNAZOUZA ILI KUPATA PESA ZA KUGHARAMIA MIUNDOMBINU NI NYINGI KULIKO TUNAZOBAKI NAZO? Sasa mbona PESA ZA Kugharamia Miundombinu TUNAKOPA?

4. Wakati Bank Kuu ya South Africa(SARB) inamiliki akiba ya Tani 125.5 za Dhahabu, Bank Kuu ya Tanzania(BOT) inamiliki Akiba ya Dhahabu ya Tani 18.9 tu. Hata tani 20 hatuna.

5. Nawaza kwamba, Ninamiliki Shamba kubwa la Mahindi, HALAFU mimi mmiliki wa Shamba NANUNUA MAHINDI.

6. Nawaza Kwamba Wawekezaji Wakija, Tunachukua kipande chetu cha Ardhi chenye Dhahabu TUNAWAPA WAO halafu sisi Wenye Dhahabu TUNANUNUA dhahabu kutoka kwa Wawekezaji, HUU NI UWENDAWAZIMU. Hebu Wataalamu MNISAIDIE MAWAZO HAPA.
7. Tanzania ni nchi ya 3 kwa Uzalishaji wa Dhahabu Afrika. Lakini Kenya inakiwango kikubwa cha Hifadhi ya Dhahabu Mara tatu zaidi ya Tanzania, Wakati Kenya haipo hata kwenye nchi 15 zinazozalisha Dhahabu Africa.

HAKIKA, KUNA MCHEZO TUNACHEZEWA.
1769969197659.jpg
 
Hofu ya kuwekewa vikwazo vya kuuza Dhahabu nje, vyasababisha wauze Dhahabu haraka

Wahusika wamekuwa wakitengeneza hadithi mbalimbali kuuhadaa umma, lakini ukweli ni kwamba watawala wana hofu ya nchi kuwekewa vikwazo vya kuuza dhahabu nje kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Samia.

Kwa kuwa madini ya Dhahabu na Almasi, kutokana na kuwa na thamani kubwa, na kuwa yamekuwa yakitumika kujenga kiburi cha serikali nyingi za kidikteta Duniani, vikwazo vinavyozuia ununuzi wa madini kutoka mataifa yenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, mara nyingi imetumika kama nyundo ya kwanza kwa tawala za kidikteta.

1. Huko Afrika ya Kati, nchi iliwekwa kwenye vikwazo vya kutokuuza almasi nje kwa miaka 11, vimeondolewa mwaka 2024.

2. Huko Sierra Leone, kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, mwaka 2000 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka vikwazo vya mataifa yote kutonunua almasi ya Sierra Leone.

3. Liberia, mwaka 2001, Umoja wa Mataifa uliweka vikwazo vya kuzuia almasi ya Liberia kuuzwa mahali popote Duniani, baada ya kuthibitika kuwa Liberia ilikuwa inasavidia vikundi vya waasi nchini Sierra Leone.

4. Hapo Angola, mwaka 1998, Umoja wa Mataifa uliwekea vikwazo almasi za Angola kwa sababu ya uwepo wa kundi la UNITA.

5. Pia almasi ya Ivory Coast iliwahi kuwekewa vikwazo tangu mwaka 2005 mpaka 2014.

6. Venezuela, mwaka 2018, Marekani iliweka vikwazo vya kuzuia mauzo ya dhahabu kutoka Venezuela kutokana na utawala wa Maduro kugandamiza haki za wananchi.

7. Nicaragua, mwaka 2022, utawala wa Ortega Murillo uliwekewa vikwazo vya kutokuuza dhahabu yake nje kutokana na serikali yake kukiuka haki za binadamu.

Ikumbukwe kuwa Jumuia ya Madola iliipa Serikali ya Tanzania mpaka mwezi wa March 2026, iwe imetoa ushirikiano kwa Jumuia ya Madola kuunda tume huru kuchunguza mauaji yaliyofanywa na utawala wa Samia Oct 29, mwaka 2025. Jumuia ya Madola ilimteua Rais mstaafu wa Malawi kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo, lakini utawala wa Samia, bila ya kutoa kauli, lakini kivitendo, uliigomea Tume hiyo.
Na Jumuia ya Madola ikasema inaupa utawala wa Samia muda mpaka mwezi wa Machi 2026. Na kama utawala wa kidikteta wa Tanzania utakuwa bado umekaza shingo, kikao cha Jumuia ya Madola kitakachofanyika March 2026, kitatoa Azimio dhidi ya utawala wa Samia.

Bila ya kuweka wazi, utawala wa Tanzania umeamua kuuza haraka akiba ya dhahabu ili kuepuka dhahabu hiyo kuwa mawe yasiyo na msaada, kama vikwazo vitakavyowekwa vitahusisha kuzuia mauzo ya dhahabu yetu nje ya nchi.

Na kama itatokea tukawekewa vikwazo vya mauzo ya dhahabu nje, tumekwisha. Baada ya utalii kudorora, chanzo kikuu pekee cha pesa ya kigeni kilichobakia ni mauzo ya dhahabu.

Hofu ha kuwekewa vikwazo na mataifa ya Ulaya, vimemfanya Kombo kuhamia Ulaya, akijaribu kutumia kila mbinu anazofikiria zinaweza kuiokoa Serikali ya Muuaji.
Huku kuna ICC inayoenda na mtazamo wa kisheria, kwa uoande mwingine kuna mataifa yanayojipanga kuchukua hatua za kuudhibiti utawala hafamu kwa diplomasia ya siasana uchumi.

Hapa anachofanya Kombo ni kutaka kuzuia mti ambao majani yake yanakauka kwa kuyapaka maji majani wakati ardhi ni kavu kabisa, haina maji. Kwenye hili, Watanzania ndiyo ardhi na ndiyo shina la mti unaokauka.
 
Nimekuelewa mtani.
 
Back
Top Bottom