Maswali kwa rais Kikwete na yatokanayo

Maswali kwa rais Kikwete na yatokanayo

Nyaraka za dini zimesisitiza vita dhidi ya ufisadi kupoteza dira na hivyo jamii kuelekezwa kuchagua 2010 kwa kuzingatia watu waadalifu. Mzee wa nchi na mafisadi wengine wanaipaka rangi tofauti hoja ya msingi na kuona nyaraka zinatuelekeza tuchague watu wa dini zetu. HATARI KUBWA
 
Hivi waziri wa miundombinu na wasaidizi wako pamoja na hiyo Tanroads mnakuwa wapi mpaka issue ya mkandarasi kuendelea kukwangua barabara inayopaswa kuwekwa lami kwa miezi 24 mpaka hili lijulikane kwenye ziara ya raisi? Raisi wetu una kazi kwelil kweli!!
 
Kwa kweli nimechoshwa na ukilaza wa mkuu huyu, hata hiyo digrii ya uchumi nadhani ilipatikana kisanii zaidi. Hata hao waliompasisha walaaniwe!!!. Raisi anatangaza uomba omba PUU. Eti ameenda kuomba vyandarua vya kutoshereza kila familia!!! jamani mliokunywa maji ya bendera ya chama tawala mumuonye sana, anazidi kufulia. kuomba vyandarua??? KULIKONI
 
JK alinishangaza wakati anajibu swali aliloulizwa kwa nini safari za nje ni nyingi? Alijibu kuwa huwa anaenda kutafuta msaada (Kuomba omba) na ni lazima aende yeye mwenyewe physically ili aweze kupewa hiyo misaada.

Hivi kwa kweli rais kama anamtazamo wa kuomba omba na ndio kiongozi wa juu kabisa wa nchi sasa anategemea nini kwa wananchi wake. Ndio maana kila siku atasikia kuna njaa vijijini kwa sababu watu hawataki kujishughulisha.

Rais JK anapaswa aache kabisa hiyo dhana ya kuomba omba na akae na wataalamu wa fedha na uchumi ili waweze kumpa strategic plan ambazo zinaweza kuliokoa taifa letu kwenye ili janga la kutegemea misaada kutoka nje. Nchi hii ina Resources nyingi sana na haipaswi kuwa omba omba.
The farmer,
ubarikiwe.
 
"Rais Kikwete alisema kilichotokea mjini Dodoma ni mazingira ambayo yameonekana kama vile ni uhusiano usioridhisha kati ya wabunge wa CCM na serikali yao."Uhusiano huo kufikia hatua hiyo nini kiini au sababu?

Kwasababu mahusiano yasiyoridhisha ni wazi kuna mgongano wa makundi ndani ya CCM na sio siri katika makundi hayo kwa upande mmoja MAFISADI na wabunge wa kununuliwa wanaowaunga mkono na kwa upande mwingine wabunge wanaopinga ufisadi.

Hapa hakuna haja ya kutoa soga na kupoteza muda kuunda kamati ambazo zanachunguza kitu ambacho kiko wazi na kutumia muda wa vikao visivyo na kichwa wala miguum na pesa badala ya kutatua matatizo yaliyopo.

Hapa CCM wanajaribu kuunda tume kuchunguza mchana kama kweli mchana wakati watu wote wanaoana ni mchana na jua linawaka!

CCM wacheni MAZINGAOBWE MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Tatizo letu hatukai chini na kutafakari tunataka nini na tuamze na nini,tunarukia tu vya wenzetu wakati wao wanaenda systematically, akienda omba msaada ndo hivyo unapewa mkongo wa mawasiliano

Haya matumizi yake ni kwa kiasi gani, itafaidisha wangapi haielezeki! Yapo mambo ya msingi sana ambayo hayapaswi kwenda kuwa omba omba, KILIMO KWANZA, ni kiongozi gani anaeonyesha kwa mfano huu waraka wa kilimo kwanza? Au wanapiga domo jukwaani inaishia hapo?

Ningemwona mzee ni wa maana kama angepambana na kufukuzana na hii azimio la kilimo kwanza hadi aone mwisho wake!

Nchi hii hatujui tunataka nini, unaenda kuomba msaada UAE, Europe, USA, wakati wanachukua mali zetu kibao tena wanaenda kuconvert into monentary ukiomba msaada unamegewa kapande kadogo ka mali zako,bila wewe kujijua ukidhani umesaidiwa kumbe mnagawana mali yako! Hatuna DIRA.

Nimefurahishwa na Mzee JK alivyojibu swali la NEC na wabunge wa CCM.
 
Ukimsikiliza mheshimiwa raisi JK kuhusiana na mambo mbalimbali, hapendi kuonyesha msimamo wake moja kwa moja kuwa anataka nini au anaunga mkono lipi. Kutokana na mazungumzo yake na wananchi tarehe 9/9/2009 imenifanya niwe na hisia kwamba aidha:

Ana nia njema ya kushuhulikia mambo kama ufisadi na utendaji wa watumishi wa serikali lakini anawaogopa wahusika hivyo anaacha yarekebishwe na vyombo vingine kama waandishi wa habari na wanaharakati mbalimbali.

Au haelewi kabisa kinachoendelea na anaongea tu anachoelezwa na wasaidizi wake.

Nyie mnamwelewaje huyu mheshimiwa?
 
Nani angeulizwa wakati simu dar zilikuwa hazipatikani?
I have a bad feeling kama kipindi kilikuwa LIVE...

Salva tengenezeni DVD muziweke online tuweze kumsikiliza tena kwa uzuri, lakini sasa tatizo hata hiyo website ya IKULU haieleweki. Mnaweza kushirikiana na kitengo cha computer chuo kikuu watengeneze website na kuihost, kuna mtaalamu pale anaitwa DR. Twaha huyu anaeza sana kusaidia.

Halafu wakati mwingine mheshimiwa apate na muda wa kuchat online kupitia hiyo website ya IKULU maana kupitia simu na sms nafasi ni finyu sana.

Tido hivi hicho kipindi kilikuwa LIVE kweli? ni hayo tu Hongera sana mheshimiwa Raisi kwa kujibu maswali vizuri.
 
JK jana alijitahidi sana kujibu kile alichoulizwa na sishangai tiyari alikuwa anajua mchezo utachezwa vipi tena waliutumia kwa umakini mkubwa, kwa hilo amejitahidi. Kizuri kisifie.

Pia hata Tido alijitahidi vya kutosha kuendesha hicho kipindi isionekane ni kupiga siasa za CCM. Hasa alivyomuuliza kuhusu Spika, kwani alikuwa anarusha rusha maneno.

Ila nilishangaa alivyoelezea kuwa wajumbe wa NEC walifikia kutamka maneno makali! nadhani hapo moja kwa moja alionyesha kutokusimamia vizuri hicho kikao akiwa Mwenyekiti kama tunavyosikia kwenye magazeti.

Pia kuhusu chama kugawanyika, kwakweli alijiumauma kwani jibu analo ni kuwaondoa mafisadi ndani ya chama lakini anakwepa kwepa kuwa kamati iliyoundwa itaweka sawa haya mambo, sitegemei kama wapambanaji na mafisadi kwa sasa kama wanaweza kukaa meza moja!

Acha tuwape muda aliimba Mpoki!
 
kwa kweli Rais wetu amejitahidi sana kujibu hoja na keroro mbalimbali za wananchi ila nadhani TBC waangali sula la muda naona hautoshi,maswali ni mengi,ila cha msingi karibu maswali yaliyokuwa yasemwa sana na jamii yaliulizwa na kujibiwa kwa ufasaha na umakini mkubwa.
 
Staili hii ya TV, Radio na simu ni nzuri kuliko ile ya mwanzo ya kurekodi hotuba kwenye mikanda. Nzuri zaidi ni pale atakapo kutana na waandishi/wahariri na wachambuzi wengine makini halafu mahojiano hayo yakarushwa live. Jana alijitahidi kujibu maswali yale alooulizwa.
 
kwa kweli Rais wetu amejitahidi sana kujibu hoja na keroro mbalimbali za wananchi ila nadhani TBC waangali sula la muda naona hautoshi,maswali ni mengi,ila cha msingi karibu maswali yaliyokuwa yasemwa sana na jamii yaliulizwa na kujibiwa kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Mbona tuliyajua hayo mapema? Mtego tayari umewanasa wengi na sasa 80% zake zilizoanza kupata mgogoro zitapona tu. Kwa vile wengi watauvaa mkenge kama unavyoonesha, Mkwere anainyanyua CV iliyofulia na mwakani anapiga 90%😕
 
IT experts question govt over use of private email account

Source: THIS DAY

THE government has been criticized for using a private email address for official state business in yesterday’s scheduled first-ever interactive national address by President Jakaya Kikwete.

Members of the public were set to be given a rare chance to send their questions or views directly to the president via phone calls, text messaging (SMS), or e-mail.

However, the scheduled commissioning of a private Yahoo! email address " swalikwarais@yahoo.com " for public use in communicating with the president, was roundly faulted by various information technology (IT) and digital security experts in the country.

President Kikwete’s live, prime time address to the nation was set to begin at 8.30 pm last night, lasting for one and a half hours. Along with the Yahoo! email address, the State House directorate of communications on Tuesday evening issued a series of landline and mobile telephone numbers listed to the state-run Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) for the occasion.

According to the critics, the use of the private Yahoo! email account - which is understood to have been hastily created the same day that State House announced the plans for the innovative presidential interaction with radio and television listeners and viewers - could pose a security breach.

"There are serious security and privacy issues to consider. It is very easy for hackers to plunder the Yahoo! email account," said a Dar es Salaam-based IT expert who preferred not to be named.

"Why on earth would the government decide to use a private email address for official state business, when it has its own secure server at www.tanzania.go.tz?" the expert added.

The State House Director of Communications, Salva Rweyemamu, was yesterday not immediately available for comment despite repeated attempts by THISDAY to reach him by phone.

It is understood that various sensitive government agencies and institutions, including State House itself, have routinely been using private email accounts for official government business.

For example, the State House directorate of communications alternately uses an email account from a secure government server " press@ikulu.go.tz " as well as a private email address " ikulucommpress@googlemail.com " to issue official press releases to the media.

The communications units of the Vice-President’s Office (makamupress@yahoo.co.uk), Zanzibar State House, and the Prime Minister’s Office (PMO) have also been using private email accounts for official purposes.

Even the Tanzania Information Services (MAELEZO) department, the government’s official mouthpiece organ, routinely communicates with the mainstream media outlets through the private email address maelezopress@yahoo.com.

According to local IT experts interviewed by THISDAY during the course of yesterday, it is important for the government to use official email addresses to avoid falling victim to fraud, hacking, and/or other security breaches.

The experts say it is relatively easy for hackers to gain illegal access to Yahoo! and other personal email accounts, and the contents ' official government emails, email addresses, and other sensitive information ' thus becoming compromised.

Major changes are needed in the way information security is being handled within government, the experts emphasize.

"Cyber-security matters and ensure coordination of government ministries, departments and agencies in this aspect, so that security standards are met and the government is properly protected from possible cyber-attacks," one IT expert suggested to THISDAY.
 
Mbona tuliyajua hayo mapema? Mtego tayari umewanasa wengi na sasa 80% zake zilizoanza kupata mgogoro zitapona tu. Kwa vile wengi watauvaa mkenge kama unavyoonesha, Mkwere anainyanyua CV iliyofulia na mwakani anapiga 90%😕

Mkuu hapo umenena!
Majibu aliyo yatoa Jk mengi yalikuwa ni bla bla za tunajitahidi, tumeanza kufanyia kazi kama kawaida yake! machache alijitahidi.

Kilichoniboa, ni pale alipo ulizwa swali la kwanini hawajawashughulikia watu wa RICHMOND na KAGODA, kwanza akakwepa kabisa kugusia kagoda akakimbilia kutoa historia ya RICHMOND, halafu anaridhika kwamba viongozi wa kisiasa tayari walisha wajibika! eti lililo baki ni watendaji wa serikali. Hivi kweli kujiuzuru kunatosha kwa mtu aliyeliingiza taifa mkenge wa mabilioni ya RICHMOND?

Hivi kweli raisi bado anaamini na kuridhika kwamba wamiliki wa RICHMOND ni maruhani?? Ghost? Hivi huu ni uswahili gani huu? kwa mamlaka yote aliyo nayo anakuja mbele yetu wananchi kutwambia eti wamiliki ni maruhani?

Halafu kitu kingine niliona kama maswali mengine yalikuwa yameandaliwa wala hayakuwa ya papo kwa papo. yale majibu ya takwimu za barabara yaridhihirisha hilo! kwa mtaji huo ni janaja fulani inafanyika kukarabati stinking Cv
 
Mnasema JK alijitahidi kujibu maswali ama alijitahidi kumwaga bla bla kama alivyo zipanga ? Huwezi kuulizwa swali la Kigoma unaanza kuelezea Tanzania nzima . Then unakuja unasema JK alijitahidi una akili kweli ? Kuna namna ilichezwa. JK ameniacha hoi kabisa pale ambapo imeonakena wazi kwamba Kingunge alikuwa ana bwatuka akiwa nabaraka zake JK juu ya Waraka maana JK naye ana mawazo kama ya Kingunge na alienda mbali kupotosha kwamba uchaguzi utakuwa wa wetu kashinda ama wao kashindwa . Sikutegemea Rais aseme maneno yake inaonekana hara waraka hajausoma .
 
Kama kweli JK anataka kusikia kero za Watanzania kwanini asifanye townhall meeting? Kwa dar afanye mkutano Kinondoni, Temeke and Ilala watu wamuulize maswali kwa kuchagua moja kwa moja.

Then kama azunguke hata mikoa mitano au sita, kuliko huu upuuzi wa maswali ya kwenye TV. Unadhani bibi yangu pale Kongei, Lushoto ameona JK alichozungumza kwenye TV? Kwanza hata umeme hana. Jee % ngapi ya Watanzania wana access ya TV?

Aliyetoa hii idea ya TV lazima atakuwa ni mmoja wa wana mtandao wenzie. This is total insane.
 
HILO NI CHAGUO LA MUNGU

Alinifurahisha sana pale aliposikia sauti ya mwanadada kutoka Singida, nikasikia mkuu anaitikia "UJAMBOO EHHEE"

KAAAZI KWELI KWELI

Mimi nadhani huyu jamaa ana IQ ndogo sana sidhani kama hata kuamua kudanganya watanzania ndio kuwe kwa kiasi hicho:

1) Kuhusu mkandarasi huyo wa Kagera waliyemtimua jamaa aliwapeleka mahakamani na ameshinda kesi na bado anaendelea na hiyo project, sasa iweje aseme wamepata mkandarasi mwingine?

2) Hivi kweli rais anathubutu kutuambia kuwa Hazina na wizara ya kazi wanatumia vifaa vya kazi vimoja (wanashare computers), labda sijamwelewa vizuri, lakini haiingii akilini kabisa kuwa watu wa wizara ya kazi hawezi kufanya kazi mpaka wa Hazina wamalize kazi zao, kwa hiyo kuna group la watu wanaendaga kutembea tu maofisini, hivi hili lina ukweli kwa walio Dar tunaomba ufafanuzi

3) Hivi jamaa kawaweka watu zaidi ya milioni moja kusikiliza jinsi atakavyoongelea matatizo yaliyolisibu Taifa, lakini tunashangaa yaani hakuna seriousness kabisa katika sura wala maneno ya huyo jamaa, yeye kila swali akiulizwa ni kucheka kwa kebehi tu, na badala ya kujibu swali anaanza kuzunguka kusikokuwa na maana kabisa

4) Kuhusu hizo kesi zilizopo mahakamani na hat ile iliyoukumiwa ya Zombe, hivi kweli mkuu halioni tatizo liko wapi, kesi kama ya Zombe Jugde kipenga, alikusanya ushahidi tosherevu kabisa na aliuwakilisha serikalini vizurili tu, lakini kuna Vibuyu kiko pale serikalini yaani DPP na Mwanasheria wake mkuu, hawa jamaa ni mabogus sijawahi kuona, Hakimu wa kina Zombe anauhakika kabisa wakina Zombe wameua lakini ushahidi uliofika hapo mahaakamani ni shalow mno, na ukifatilia utakuta hao jamaa walipata vyeo hivyo kwa sababu ya urafiki tu na kuacha wasomi waliobobea kwenye hizo fani.

Waungwana tuna kazi kubwa, miaka kumi inapita hivihivi bila hata step moja ya maendeleo?

Kweli tuna kasi mpya ya kuelekea kwenye umaskini
 
Kwa wale mlio angalia mazungumzo ya Rais na wananchi, kwanza nadhani tumsifie JK kwa kudhubuti kuwa na live discussion ya issues. Pili tumfagilie kwa kuruhusu uhuru wa watu kutoa mawazo na dukuduku zao bila vitisho.

Nilivyo ona mimi nadhani Tido na wenzake pale TBC1 walikuwa wanachuja maswali ya watu kwenda kwa JK. Haiwezekani wenye maswali kwa njia ya simu watoke Ukerewe, Arusha, Zanzibar na Kigoma bila wajuaji wa jiji la DSM kupata fursa. Nilidhani kukaa kwa Tido huko BBC London kwa muda mrefu angekuwa a good moderator in terms of time and number of questions put forward to the President but my expectation were totally shuttered.

Let's see what happens next time.
 
Back
Top Bottom