Mdanganywa
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 620
- 342
Kuhusiana na issue ya viongozi wa dini na nyaraka anasema hawawezi kujibizana lakini anasema ni jambo ambalo limeishtua serikali.
Hofu kubwa ya Serikali ni kuelekea kwenye uchaguzi ujao ambapo watanzania watapiga kura kwa maelekezo ya dini zao!
Serikali ilitakiwa iwe na watu wenye akili ya kutafiti kwamba nyaraka za Kanisa Katoliki zimetoka zaidi ya mara 100 kwa muda wa karne sasa. Huwezi kusema serikali imeshtuka wakati miaka yote nyaraka zimekuwa zikitoka kana kwamba serikali za dunia hii zilikuwa zimelala wakatoliki wakitoa nyaraka kila kona ya dunia hii.
Serikali ilikuwa na wajibu wa kueleza kwamba wakatoliki ni kawaida yao kutoa nyaraka hizo duniani na lisionekane jambo la ajabu. Vinginevyo Serikali hiyo inajichelewesha maana hata wakikaa na viongozi wa Kanisa Katoliki hilo ndilo litakuwa jibu na ikibidi watawaonyesha nyaraka zaidi ya 1000 zilizotoka nchi mbalimbali.
Hapohapo serikali itaulizwa na wakatoliki je, huu waraka wa kanisa una toafuti gani na nyaraka zingine tena kali kama zile zinazotoka Marekani ambako hawazishangai?
Au ni ushamba wa baadhi ya watanzania kwa jambo wanaloliona ni geni wakati wangefanya utafiti wasingeona ni geni!