HILO NI CHAGUO LA MUNGU
Alinifurahisha sana pale aliposikia sauti ya mwanadada kutoka Singida, nikasikia mkuu anaitikia "UJAMBOO EHHEE"
KAAAZI KWELI KWELI
Mimi nadhani huyu jamaa ana IQ ndogo sana sidhani kama hata kuamua kudanganya watanzania ndio kuwe kwa kiasi hicho:
1) Kuhusu mkandarasi huyo wa Kagera waliyemtimua jamaa aliwapeleka mahakamani na ameshinda kesi na bado anaendelea na hiyo project, sasa iweje aseme wamepata mkandarasi mwingine?
2) Hivi kweli rais anathubutu kutuambia kuwa Hazina na wizara ya kazi wanatumia vifaa vya kazi vimoja (wanashare computers), labda sijamwelewa vizuri, lakini haiingii akilini kabisa kuwa watu wa wizara ya kazi hawezi kufanya kazi mpaka wa Hazina wamalize kazi zao, kwa hiyo kuna group la watu wanaendaga kutembea tu maofisini, hivi hili lina ukweli kwa walio Dar tunaomba ufafanuzi
3) Hivi jamaa kawaweka watu zaidi ya milioni moja kusikiliza jinsi atakavyoongelea matatizo yaliyolisibu Taifa, lakini tunashangaa yaani hakuna seriousness kabisa katika sura wala maneno ya huyo jamaa, yeye kila swali akiulizwa ni kucheka kwa kebehi tu, na badala ya kujibu swali anaanza kuzunguka kusikokuwa na maana kabisa
4) Kuhusu hizo kesi zilizopo mahakamani na hat ile iliyoukumiwa ya Zombe, hivi kweli mkuu halioni tatizo liko wapi, kesi kama ya Zombe Jugde kipenga, alikusanya ushahidi tosherevu kabisa na aliuwakilisha serikalini vizurili tu, lakini kuna Vibuyu kiko pale serikalini yaani DPP na Mwanasheria wake mkuu, hawa jamaa ni mabogus sijawahi kuona, Hakimu wa kina Zombe anauhakika kabisa wakina Zombe wameua lakini ushahidi uliofika hapo mahaakamani ni shalow mno, na ukifatilia utakuta hao jamaa walipata vyeo hivyo kwa sababu ya urafiki tu na kuacha wasomi waliobobea kwenye hizo fani.
Waungwana tuna kazi kubwa, miaka kumi inapita hivihivi bila hata step moja ya maendeleo?
Kweli tuna kasi mpya ya kuelekea kwenye umaskini