SIO haki kumlaumu (Salva) kama kweli yupo hapo Ikulu na hayupo Masomoni nje !!
Jamani, kiongozi mwenyewe si ndiye anayetakiwa kuhakikisha kila kitu kiko fyee. Mbona Kagame hazungumzi na mtu hufanya vitendo tu na sikuzote kambi yake haina wababaishaji na wavurugaji maana hawacheleweshi kwenda pale wanapopaweza.
Kuna washika dau kadhaa waliokuwemo ikiwa ni pamoja na Bri Kibanga, Ikulu, Uncle Tiddo, TBC, Washikaji Clouds FM na wengineo. Je, wote walishindwa kuhakikisha kuwa wanafanya kitu kiwe mfano wa kuigwa na wengine ?
Lakini kama vijana kwa kuwa Ikulu au Kwa Waziri Mkuu wanawadharau wale waliowafundisha kazi na hawataki tena ushauri toka kwao wewe unategemea nini. Watu wanaweza kuwa wakubwa ndio wakawa wadogo kabisa kimawazo na kifikra. Walijua hilo ?
Halafu hukusoma ile makala ya Mwananchi nadhani mwandishi ni Anko Makilla aliyekuwa Business Times zamani juu ya Wavuti za serikali-kamwaga wazi yanayotakiwa kufanywa lakni ndiyo hivyo sijui hata kama jamaa wamepata nafasi ya kusoma maani serikalini ngumi za chini kwa chini na chamani mateke juu kwa juu basi tutegemee nini kutoka kwao. Unaambiwa hii leo Watanzania wanamtegemea Mungu tu na sio viongozi wao.