Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,768
Ndugu Waziri wa Afya, naomba kukuuliza MASWALI matatu tu ili nisikuchoshe. Nikiwa mwananchi wa nchi hii ninahitaji majibu sahihi kutoka kwako tena yawe ya kitaalamu na si ya kisiasa:
1) Je, korona ipo au haipo hapa Tanzania, na kama ipo Ni ya aina gani, ya China au ya South Africa?
2) Je, Makamu wa Kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad anaumwa korona kama Chama chake kilivyotoa taarifa au ni ugonjwa wa pneumonia? Ni kwanini serikali haijaujulisha umma juu ya kuugua kwa kiongozi huyu?
3) Ni kipi huleta taharuki kwa wananchi Kati ya uongo na ukweli?
Nakumbuka Bwana Yesu amewahi kusema: "tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru." Mathayo 8:32.
Asante Waziri, nakutakia kazi njema kwa matumaini ya kupata majibu sahihi yatakayoniondolea "taharuki" mimi pamoja na Watanzania wengine walio kama mimi.