Maswali na majibu kuhusu Alliance In Motion Global

Yani mpaka nimesikitika kwa izo fikra zako ndugu cha kwanza sikulaumu kwasababu vijana wengi tuna fikra ya kushindwa,na kutokuwezekana ndo maana ukiona aliyefanikiwa utaanza kumkosoa kwa kila namna badala ya kuuliza nini alifanya.
 
Hao unawapa hela wanakupa mitakatak fla hivi ya bidhaaa, eg mafuta, sabuni, dawa ya meno.
Unajua watu wengi hawana elimu
HAhahahahaha Daaaah umevamia mada asee. Alliance hakuna sabuni, mafuta wala dawa za meno. This is healthy and Wealthy company
 
bakini tu kama mlivyo hakuna mtanzania mwenye akili atafanya biashara na nyinyi(matapeli)
 
Wanasumbua na hawakati tamaa, kuna mdada ananifuatilia karibia miezi sita sasa na hajaacha kunitumia makorokocho yao, video, picha, matangazo, mialiko dah
 
Wanasumbua na hawakati tamaa, kuna mdada ananifuatilia karibia miezi sita sasa na hajaacha kunitumia makorokocho yao, video, picha, matangazo, mialiko dah
aise mtu anakufatilia miezi 6? ningemuitia polisi aisee ...pingu....ndani !!!
hivi hawa ndo wale wanasema ununue saa ya milioni 5 utapata milioni 5 ya ziada [emoji2][emoji2]
 
Hivi kwanini story zenu nyingi uwaga ni za fulani alikuwaga manager bank akaacha mshahara wa 6M akaja huku kwetu baada ya kuanza kuingiza zaidi ya hizo?

Afu kwann hao members wenu wanaopigaga picha na magari mazuri ukikutana nao face to face unakuta hawafanini hayo magari na pia wengi wao viatu vyao vinakuwa vimekwisha upande 1?
 
Kwanini nyinyi Alliance, msitangaze tu hizo products, mfanye marketing za products tu, kama watu watakuja kununua jumla ili nao wauze Hakuna neno... Ila tu isiwe lazima mtu ajiunge kisha atafute watu chini yake nao watafute watu chini yao....yaani chain hadi hukoooo.... Ina maana mtu anaingia akijiunga kwa gharama Fulani mafanikio yake ni kwa jinsi watakavyojiunga chini yake... La hawezi kupata mafanikio atabaki anabugia tu zile dawa chakula...ndio maana waliojoin wanahangaika kumarket kupata watu wa kujiunga zaidi ya kuuza bidhaa hizo...
 
Mimi marketing strategy yao ya mapicha picha ya kushika vibunda vya hela na magari hayanivutii sijui kwa wengine Mimi hainipi picha ya kunivutia kujoin nao, in fact product zao naweza nunua kwa vile zina maelezo mazuri fulani
 
Haya mambo yakubebeshana mamizigo yasiokuwa na soko kwa laki tano nani anayataka?
Kazi kubwa ya hawa jamaa ni kuwatamanisha watu
 
Embu uliza wa foreva living soli zimeisha story za Dubai wanazisikia tuu kwa wale mameneja tuu
Ni bora uje upange vitunguu hapa tandika kama Mimi mkuu,utapata kidogo kuliko kumaliza soli na tai shingoni
Forever living nilijiunga aisee kwa sh. Elf 50 kipindi nipo chuo, na Mimi nikaunga watu wawili basi biashara ikaishia hapo
 
Kuna siku niliitwa tena weekend jumapili nkajua naitwa nikapige hela, basi kufika nikakuta wadau nikakaribishwa mbele kabisa, nikaanza kucheki movie zao nkashtuka maana mm ni akili kubwa, basi vijana wamechachamaa kwa maelezo yakiongozwa na kijana wa Kiganda ambaye anaonyesha picha za nyumba ambazo amedownload na magari ambayo yamefichwa plate no. Nilichokiona ni vijana wa chuo wamechukuliwa mateka kutoa semina kuhadaa raia waliokata tamaa, wamevaa suti mchapio na viatu vilivyoisha upande.

Kwanza hawa jamaa wanalaghai nchi ambazo watu wake wanauelewa mdogo kwahiyo hawawezi kumarket nchi za ulaya na America na isitoshe Amerika walishapiga marufuku biashara za namna hii tokea 1920.

Pili baada ya semina hawaruhusu maswali ya wazi yaani wanakuambia kama una maswali muulize aliyekuita, nikaona ni upuuzi nimepoteza mda halaf nimuulize maswali mtu ambaye hata sura ya 1mil haijui.

Tatu bidhaa wanaziuza kwa jumla yaan hupewi ruhusa ya kujaribu bidhaa moja.

Nne ni kwamba wamejikita zaidi kwenye utajiri na sio kutatua matatizo kwa bidhaa zao wanazodai ni tiba, sasa mwenye akili kubwa utajiongeza kama dawa inatibu pressure na kisukari kweli kweli kwann usitoe hata offer then baada ya matumizi akipima na akiona nafuu ataleta wenzake wengi?

Mwenye uelewa ataelewa
 

Nimekuelewa Boss, lakin si kweli kua hakuna bidhaa za rejareja ukitaka mim naweza kukupatia ujaribu
Pia Marekani hawajakataza busness za MLM kwasababu hata Donald trump ameanzisha MLM yake inaitwa Trump.
Pia maswali mengi huwa wanajibu ma expert
Kama una shida ya afya naweza kukupa dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…