cyrustheruler
JF-Expert Member
- Jul 20, 2015
- 2,044
- 1,869
Hahahaha hawa masela wanatumia slogan moja hiyo hiyo hawabadilishi[02/03 14:54] Tonny Montana: What have you achieved so far in network marketing
Alot
1. Kwanza nimweza kumsomesha mdogo wangu yupo cbe Dodoma certificate
2. I have shifted from home to dar while living in an apartment which I pay 700k my self sinza
3.i have hired a house girl whom I pay her 50k ever month
4. Me and my family are healthy because of the company products na juz tu last born wetu Kapona ulcers because of the products
5. I have managed to meet with Alot of people and create a big team from which even if I won't be around still I will receive my earnings
6. Am socially and financially free
Kama si utapeli ni nini swagger yao eti nataka acha kazi niwe full time. Bullshit MI demu namtaka tuu nimle mzigo
Hahahaha Hiyo ndo spirit ya kuwakamata mapetaHivi kwanini story zenu nyingi uwaga ni za fulani alikuwaga manager bank akaacha mshahara wa 6M akaja huku kwetu baada ya kuanza kuingiza zaidi ya hizo?
Afu kwann hao members wenu wanaopigaga picha na magari mazuri ukikutana nao face to face unakuta hawafanini hayo magari na pia wengi wao viatu vyao vinakuwa vimekwisha upande 1?
Kuna siku niliitwa tena weekend jumapili nkajua naitwa nikapige hela, basi kufika nikakuta wadau nikakaribishwa mbele kabisa, nikaanza kucheki movie zao nkashtuka maana mm ni akili kubwa, basi vijana wamechachamaa kwa maelezo yakiongozwa na kijana wa Kiganda ambaye anaonyesha picha za nyumba ambazo amedownload na magari ambayo yamefichwa plate no. Nilichokiona ni vijana wa chuo wamechukuliwa mateka kutoa semina kuhadaa raia waliokata tamaa, wamevaa suti mchapio na viatu vilivyoisha upande.
Kwanza hawa jamaa wanalaghai nchi ambazo watu wake wanauelewa mdogo kwahiyo hawawezi kumarket nchi za ulaya na America na isitoshe Amerika walishapiga marufuku biashara za namna hii tokea 1920.
Pili baada ya semina hawaruhusu maswali ya wazi yaani wanakuambia kama una maswali muulize aliyekuita, nikaona ni upuuzi nimepoteza mda halaf nimuulize maswali mtu ambaye hata sura ya 1mil haijui.
Tatu bidhaa wanaziuza kwa jumla yaan hupewi ruhusa ya kujaribu bidhaa moja.
Nne ni kwamba wamejikita zaidi kwenye utajiri na sio kutatua matatizo kwa bidhaa zao wanazodai ni tiba, sasa mwenye akili kubwa utajiongeza kama dawa inatibu pressure na kisukari kweli kweli kwann usitoe hata offer then baada ya matumizi akipima na akiona nafuu ataleta wenzake wengi?
Mwenye uelewa ataelewa
Kwa hiyo kumbe kweli!! Kuwa yale magari mnayo piga nayo picha sio yenu. DahSidahani kama kuna mpango wa limitation kama nini uweke na nini usiweke kwenye matangazo yoyote ya biashara. Kama ilivyo watu wanavyoweka magari au kushika fedha kwenye Matangazo mengine mengi kama nia ya kuonyesha nini mtu analenga kupata. Kama ingekuwa unapata miswaki, Bajaji.. ungeona picha za vielelezo hivyo
Vip, Bado unaendelea na bizness mzeeeSio utapeli. Nicheki tuyajenge 0659633720
Kuna mwamba kipindi tupo college alikuwa anapiga hizi ishu ana nivutia, walikuwa kama 3. Wakaja kupotezea wenyewe, wao walikuwa ORIFLAME.
Hahahaaa sikuwahi kufikiria angle hiyo aiseemagari sio yao mark this, ukiona picha za magari hazina plate number au wanaficha ukiona plate number ya gari ingiza kwenye ile site ya trafic ya kuangalia fine ingiza number ya gari compare na jina la aliyepiga picha.
magari sio yao mark this, ukiona picha za magari hazina plate number au wanaficha ukiona plate number ya gari ingiza kwenye ile site ya trafic ya kuangalia fine ingiza number ya gari compare na jina la aliyepiga picha.
Hahahaaa sikuwahi kufikiria angle hiyo aisee
Ila kifupi ni kwamba machizi wana hali mbaya kinoma halafu kuna ile dhana ya kuficha umasikini ambayo inajidhihirisha wazi kabisa
Yani unamuona mtu kanyuka suti lakini unaona kabisa suti imemkataa. Mwingine kapiga ya mtumba shati la ndani ule weupe umechange kua rangi ya dona.
Kuna demu mmoja alikua akijinadi kua amepiga bingo ya 50+ millions na ana mkoko ambao unaogopwa na watu kwasababu unakula sana utuli nikimcheki usoni naona fenesi yani pimples kibao. At the same time wanakutangazia package zao kua zinauwezo wakutoa pimples
Mwingine wakati anapita mbele kwenda kuhamasisha watu, alipita karibia yangu nikasikia harufu ya sabuni aina ya jamaa.
Huwezi amini jamaa hata aibu hana eti anasema anamiliki milion 100 na yeye anakamilisha mwaka tangu ajiunge. Mara sijui niliacha kazi ya udokta nikaamua kujiunga na hii global mi nikawa namuona kama joker tu.
It's Scars
Magari sio yao na kitu kimgine extra nilicho observe pale nikua wachache sana wenye uhakika wa kutimiza milo mitatu
Halafu wanaishi kwa mateso ya kujificha ficha sana ili watu wasiwasanukie kua wanahaso. Pale makumbusho kwenye jengo lao la semina hakuna hata gari iliyopaki eneo lile ambayo wakiwa ndani wanayazungumzia kua wanayamiliki
It's Scars
Biashara yoyote ambayo focus yake ni kutafuta wauzaji na sio wanunuaji kuwa na hofu nayo Sana, unahudhuria Masaa Matatu MTU anataka akupe utajiri kupitia dawa za chunusi na kadhalika na wakati wote huo wala hashitukii kukushauri na wewe uitumie kwasababu chunusi unazoHabar zenu wakuu, natumai wote muko imara na mnazidi kupambana na hali zenu katika hii awamu ambayo Malaika tunawaona wakiishi kama Mashetani
Bila kupoteza mda leo nina suali nahitaji mawazo au maelekezo mawil matatu
Ni hivi kuna yeyote aliwahi kusikia au kujiunga na hii Bussiness Network inayoitwa Alliance In Motion (AIM Global Network Bussiness)? Kama yupo naomba maelezo , kuhusiana na hii kitu
Mimi nimeona sehemu wakiitangaza hio biashara so nataka kupata uhakika kuhusu hawa watu ili kama ni wapiga dili tu niwapotezee
Ahsantenii