Hahahaaa sikuwahi kufikiria angle hiyo aisee
Ila kifupi ni kwamba machizi wana hali mbaya kinoma halafu kuna ile dhana ya kuficha umasikini ambayo inajidhihirisha wazi kabisa
Yani unamuona mtu kanyuka suti lakini unaona kabisa suti imemkataa. Mwingine kapiga ya mtumba shati la ndani ule weupe umechange kua rangi ya dona.
Kuna demu mmoja alikua akijinadi kua amepiga bingo ya 50+ millions na ana mkoko ambao unaogopwa na watu kwasababu unakula sana utuli nikimcheki usoni naona fenesi yani pimples kibao. At the same time wanakutangazia package zao kua zinauwezo wakutoa pimples
Mwingine wakati anapita mbele kwenda kuhamasisha watu, alipita karibia yangu nikasikia harufu ya sabuni aina ya jamaa.
Huwezi amini jamaa hata aibu hana eti anasema anamiliki milion 100 na yeye anakamilisha mwaka tangu ajiunge. Mara sijui niliacha kazi ya udokta nikaamua kujiunga na hii global mi nikawa namuona kama joker tu.
It's Scars