Maswali na Majibu kuhusu Kitabu cha Mohamed Said

Maswali na Majibu kuhusu Kitabu cha Mohamed Said

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,606
Reaction score
1,711
Kariu kwenye ukurasa wa maswali na majibu kuhusu Kitabu cha 'The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968): The Untold Story of the Muslim Struggles Against British Colonialism in Tanganyika'. Ukurasa huu ni tofauti na ile mingine hivyo tunaomba isiunganishwe. Hapa tunajikita katika kuhakiki maandishi halisi yaliyomo humo ili kukiboresha kitabu n.k.

Hivyo, ni ukurasa unaoratibiwa. Nitakuwa naweka maswali yanayohitaji ufafanuzi/uthibitisho. Tuanze na hayo hapo chini.

1. "Aziz Ali Dosa was the first African to own a car and was always chauffer driven" (p. 30)

2. "The two [Kleist Sykes and Aziz Ali] were the only Africans in Dar es Salaam permitted by the government to drink beer" (p. 31)

3. "The Germans halted fighting [in World War 1] throughout Tanganyika for seven days in honour of Affendi Plantan [a.k.a. "Mohosh", "Chief of the Imhambane" and husband of "Sykes Mbuwane's sister"] (p. 35)

4. "In a strange twist of fate, Abdulwahid's driver [?] in Burma came to be one of the top brass in the Tanganyikan army" (p. 55)

5. "It was here [Imphal, Burma] on Christmas eve of 1945 that Abdulwahid and other askaris, including his young brother Ally and James Mkande, made a pact to found a political party when they returned home after the war...The name of the party was to be Tanganyika African National Union (TANU). Ally Sykes remembers that Abdulwahid wrote the name of the proposed party in his diary" (p. 57-58)

6. "he [Abdulwahid], certainly no match for [Erika] Fiah" (p. 69)

7. "Stanley [Street] (called Aggrey Street after independence in honour of Dr Aggrey, and later to be renamed Makisi Mbwana Street after one of the founding fathers of TANU" (p. 71)

---
8. "Abdulwahid also came to learn that his former opponent for the union post and his father's political adversary, Erika Fiah, was instigating the union leadership to overthrow 'that South African son of Kleist'" (p. 75)

"Like all politicians of his time, Fiah was a Pan-Africanist first and a nationalist second" (p. 68)
---

9. "Kleist served on the Dar es Salaam Municipal Council, the second African to do so in colonial Tanganyika...He joined the Chamber of Commerce and was probably the first African to do so" (p. 80)

10. "Among the members of the [TAA Political Subcommittee, 1950] Abdulwahidi was the only person representing a multiplicity of interests" (p. 81)
---

11. "[TAA memorandum to the Constitutional Development Committee] surfaced at the TANU founding conference on 7th July, 1954 and was to form the basis of Julius Nyerere's speech before the Trusteeship Council of the United Nations in New York in March 1955" (p. 92)

12. "There are old men, TANU veterans, who believe to this day that the March 1955 speech by Julius Nyerere before the Trusteeship Council was written by Abdulwahid, and, so was the constitution of Tanganyika. The author has come across this story several times in his interviews with early members of TANU. The reason for this belief is that the document was drafted by the TAA Political Subcomittee in 1950" (p. 92)
---

13. "Dr Mutahangarwa was the first African to qualify as a medical doctor" (p. 104)

14. "This [emotional farewell speeh which Nyerere delivered on 5th November, 1985, to Dar es Salaam Elders, an exclusive group of Muslim townsmen who had supported him since the founding of TANU] was one of the very rare occassions at which Nyerere talked publicly about his beginnings and it was the first time he had mentioned Abdulwahid's name in public associating him with his own history and that of the party" (p. 110)

"In his farewell speech Nyerere paid tribute to Muslim elders who supported him during the struggle in spite of his religion, but he played down the role of Abdulwahid and TAA as a political organisation" (p. 110-111)

15. "Nyerere did not have any political experience worth mentioning at that time [1952]" (p. 111)

16. "As a Christian, Nyerere knew that he could never hope to build a political base in Dar es Salaam environment of the 1950s where politis assumed strong Muslim characteristics" (p. 112-113)

17. "Abdulwahid confided with the TAA executive that having the most educated African in the land would strengthen its leadership and portray a good image before the eyes of the colonial government and the United Nations Visiting Mission" (p. 113)

18. "The election was by a show of hands. [Denis] Phombeah who was in charge of the Arnatouglu Hall was the returning officer. Phombeah asked both Abdulwahid and Nyerere to go out of the hall for the voting to begin. The whole week before voting Phombeah was making rounds campaigning for Nyerere. But there was no need of doing that; the TAA inner circle of Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz and Rupia had already decided to make Nyerere president of the Association and the election was a mere formality...Abdulwahid 'lost' the election - the first loss in his whole political career - and Nyerere won by a very small margin" (p. 113-114)
---
19. "It had only been once in the history of Dar es Salaam that a Christian, Erika Fiah, had held the banner against the colonial state" (p. 118)

20. "Soon after Nyerere's takeover, TAA seemed to go into slumber. The militancy and zeal which was associated with the leadership of Abdulwahid was lost. " (p. 118)

"For a while it seemed as if Nyerere was going to be a setback to the movement' (p. 119

"Abdulwahid was aivalable as Vice-President but he was also keen to see Nyerere, as President, assuming his full role in making his own decisions" (p. 119)

"The executive committee of the association, with the exception of Julius Nyerere and Abdulwahid, virtually lost all power as the Muslim elders literally took over the movement. Gradually Abdulwahid would also come to lose his grip on the movement particularly after forming TANU, so as to leave Nyerere and the leadership from the provinces to lead Tanganyika to independence" (p. 121)

"It is said that it was about this time, in the last months of 1953, that Abdulwahid talked to Nyerere seriously about forming an open political party to replace TAA" (p. 121)
---
 
Mods please tunaomba muwe macho hapa kulinda huu uzi ,maana kuna watu hapa jukwaani wamekuwa na nia za kusudi kabisa kuvuruga kila uzi unaomuhusu mzee mohamed said
 
Karibu kwenye ukurasa wa maswali na majibu kuhusu Kitabu cha 'The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968): The Untold Story of the Muslim Struggles Against British Colonialism in Tanganyika'. Ukurasa huu ni tofauti na ile mingine hivyo tunaomba isiunganishwe. Hapa tunajikita katika kuhakiki maandishi halisi yaliyomo humo ili kukiboresha kitabu n.k.

Hivyo, ni ukurasa unaoratibiwa. Nitakuwa naweka maswali yanayohitaji ufafanuzi/uthibitisho. Tuanze na hayo hapo chini.

1. "Aziz Ali Dosa was the first African to own a car and was always chauffer driven" (p. 30)

2. "The two [Kleist Sykes and Aziz Ali] were the only Africans in Dar es Salaam permitted by the government to drink beer" (p. 31)

3. "The Germans halted fighting [in World War 1] throughout Tanganyika for sevend years in honour of Affendi Plantan [a.k.a. "Mohosh", "Chief of the Imhambane" and husband of "Sykes Mbuwane's sister"] (p. 35)

4. "In a strange twist of fate, Abdulwahid's driver [?] in Burma came to be one of the top brass in the Tanganyikan army" (p. 55)

5. "It was here [Imphal, Burma] on Christmas eve of 1945 that Abdulwahid and other askaris, including his young brother Ally and James Mkande, made a pact to found a political party when they returned home after the war...The name of the party was to be Tanganyika African National Union (TANU). Ally Sykes remembers that Abdulwahid wrote the name of the proposed party in his diary" (p. 57-58)

6. "he [Abdulwahid], certainly no match for [Erika] Fiah" (p. 69)

7. "Stanley [Street] (called Aggrey Street after independence in honour of Dr Aggrey, and later to be renamed Makisi Mbwana Street after one of the founding fathers of TANU" (p. 71)

Mdadisi,
Nimesoma maswali yako saba.

Swali la kwanza ni kuhusu Aziz Ali.
Ni kweli Aziz Ali alikuwa Mwafrika wa kwanza Dar es Salaam kununua gari.

Aziz Ali alikuwa mtu tajiri na utajiri wake ulitokana na kazi yake kama
mkandarasi.

Utajiri wa Aziz Ali unaweza kuonekana hadi leo mtu akifika kwenye nyumba
yake Mtoni ambako pamepewa jina Mtoni kwa Aziz Ali.

Nyumba hii ilijengwa katika miaka ya 1940 ni ni nyumba ya vigae na vioo na
inawezekana pia Aziz Ali akawa Mwafrika wa kwanza Dar es Salaam kujenga
nyumba kama ile.

Kwa hiyo kwa Aziz Ali kuwa na dereva wa kumwendesha ni jambo dogo sana.

Ikutoshe tu kuwa mwaka 1947 mwanae wa kwanza Dossa alikwenda Nairobi
kufanya usaili wa kurusha ndege lakini Wazungu wakamkataa.

Dossa akampigia simu baba yake Dar es Salaam huku akilia kumfahamisha
yaliyomfika Nairobi.

Aziz Ali kunariji mtoto wake alimpelekea fedha anunue gari kama kifuta machozi.
Gari hii ilimwendesha Nyerere kwingi wakati wa harakati za kudai uhuru.

Misikiti mingi ya Dar es Salaam imejengwa na Aziz Ali kiasi cha kuwa siku
alipokufa mwaka wa 1951 Tanganyika Standard lilichapa kifo chake na kusema,
''Mjenzi wa Misikiti Amefariki Dunia.''

Miaka yake ya mwisho Aziz Ali alikuwa anaendeshwa na mwanae Juma ambae
alimtangulia kufa baba yake.

Kifo cha Juma kilimuhuzunisha sana Aziz Ali kiasi akatoa moja ya nyumba yake
akamrithisha mtoto wa Juma, Abdallah Aziz.

Nyumba hii ilikuwa mtaa wa Mafia na Kongo.

Abdallah Aziz alikuja kuwa mchezaji mpira maarufu sana na kachezea timu ya
taifa kwa miaka mingi katika miaka ya 1960.

Yapo mengi lakini haya yanatosha kwa sasa.
 
Mdadisi,
Nimesoma maswali yako saba.

Swali la kwanza ni kuhusu Aziz Ali.
Ni kweli Aziz Ali alikuwa Mwafrika wa kwanza Dar es Salaam kununua gari.

Aziz Ali alikuwa mtu tajiri na utajiri wake ulitokana na kazi yake kama
mkandarasi.

Utajiri wa Aziz Ali unaweza kuonekana hadi leo mtu akifika kwenye nyumba
yake Mtoni ambako pamepewa jina Mtoni kwa Aziz Ali.

Nyumba hii ilijengwa katika miaka ya 1940 ni ni nyumba ya vigae na vioo na
inawezekana pia Aziz Ali akawa Mwafrika wa kwanza Dar es Salaam kujenga
nyumba kama ile.

Kwa hiyo kwa Aziz Ali kuwa na dereva wa kumwendesha ni jambo dogo sana.

Ikutoshe tu kuwa mwaka 1947 mwanae wa kwanza Dossa alikwenda Nairobi
kufanya usaili wa kurusha ndege lakini Wazungu wakamkataa.

Dossa akampigia simu baba yake Dar es Salaam huku akilia kumfahamisha
yaliyomfika Nairobi.

Aziz Ali kunariji mtoto wake alimpelekea fedha anunue gari kama kifuta machozi.
Gari hii ilimwendesha Nyerere kwingi wakati wa harakati za kudai uhuru.

Misikiti mingi ya Dar es Salaam imejengwa na Aziz Ali kiasi cha kuwa siku
alipokufa mwaka wa 1951 Tanganyika Standard lilichapa kifo chake na kusema,
''Mjenzi wa Misikiti Amefariki Dunia.''

Miaka yake ya mwisho Aziz Ali alikuwa anaendeshwa na mwanae Juma ambae
alimtangulia kufa baba yake.

Kifo cha Juma kilimuhuzunisha sana Aziz Ali kiasi akatoa moja ya nyumba yake
akamrithisha mtoto wa Juma, Aziz.

Nyumba hii ilikuwa mtaa wa Mafia na Kongo.

Aziz alikuja kuwa mchezaji mpira maarufu sana na kachezea timu ya taifa kwa
miaka mingi katika miaka ya 1960.

Yapo mengi lakini haya yanatosha kwa sasa.

Asante kwa maelezo ya ziada ambayo nayo ni muhimu sana, bado sijaridhika hapo kuhusu uthibitisho - namaanisha hivi:

Una ushahidi gani kuwa Mzee Azi Ali ndiye mwafrika wa kwanza kuwa na motokaa? Je, waafrika wengine waliofanikiwa enzi hizo kama vile Martin Kayamba na Erika Fiah wao hawakuwa na magari?
 
Asante kwa maelezo ya ziada ambayo nayo ni muhimu sana, bado sijaridhika hapo uthibitisho - namaanisha hivi:

Una ushahidi gani kuwa Mzee Azi Ali ndiye mwafrika wa kwanza kuwa na motokaa? Je, waafrika wengine waliofanikiwa enzi hizo kama vile Martin Kayamba na Erika Fia wao hawakuwa na magari?

Udadisi,

Sina ushahidi zaidi ya hayo niliyoeleza.

Katika historia ya Dar es Salaam Mwafrika wa kwanza kuwa na gari ni Aziz Ali.

Martin Kayamba na Erika Fia hawakuwa watu matajiri hata kidogo wala si watu
ungeweza kuwafananisha na Aziz Ali kwa uwezo.

Kipindi kile ni kipindi mahsusi na mengi nayajua katika historia ya Dar es Salaam
kwa kuwa hao ninaokutajia katika maelezo yangu ni watu ambao wazee wangu
wakiwajua vizuri sana.

Nitakupa taarifa nyingine.
Mwafrika wa kwanza kuwa na radio Dar es Salaam alikuwa Kondo Kipatwa.

Kondo Kipatwa akiishi Ilala.
Kondo Kipwata alikujakuwa rais wa Young Africans katika ya miaka 1960.

Inasemekana Yanga walimpa uongozi Kondo Kipwata baada ya kufungwa na
wapinzani wao Sunderland magoli manne mfululuzi kiasi cha watani wao kuwapa
jina la ''four, four'' yaaani ''nne, nne.''

Kondo Kipwata alikuwa ana sifa moja hakuwa anahudhuria mechi za Yanga
wakicheza na Sunderland.

Yeye alikuwa akisubiri matokeo ya mechi nyumbani kwake.
Wakati wa uongozi wake Yanga ilifanikiwa sana.

Radio ilipoanzishwa Dar es Salaam mwaka 1952 watu wakijumuika barazani
kwake kusikiliza taarifa mbalimbali.

Radio hiyo ilijulikana kama ''Sauti ya Dar es Salaam.''

Mmoja wa watangazaji wa mwanzo wa Sauti ya Dar es Salaam alikuwa Bi.
Mahunda Plantan binti yake Afande Plantan dada yao Mwalimu Sauti Plantan,
Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan.

Sasa usije ukaniuliza nina ushahidi gani kwa haya ninayokueleza.
 
asante mzee mohamed kwaajibu murua...
Tafadhali naomba majibu na hapo kwenye #2 .
 
asante mzee mohamed kwaajibu murua...
Tafadhali naomba majibu na hapo kwenye #2 .

Remote,
Hili swali la pili halina maana sana naomba tuliache.

Ni sawa na kuwa Mzee Kleist yeye wakati ule watu wengi wakila chakula
kwenye jamvi au kwenye mkeka yeye chakula chake alikuwa anakula juu
ya meza.

Basi wenzake wakimtania wakisema Kleist anaupenda sana Uzungu.
 
Hapo kila swali lina maana kimethodolojia, nachotaka ni uthibitisho/ushahidi wa yale uliyoandika, yaani mtu anathibitishaje na kuwa na uhakika kuwa ni kweli - je, kwa kurejea tunachoambiwa tu au pia kwa kulinganisha na vithibitisho na kadhalika?

Kwa mfano, ningependa kuona sheria au tamko lilitoa ruhusa hiyo ya kunywa bia kuthibitisha ulichoandika; hiyo itasidia, kwa mfano, nikitaka kukunukuu nawezaje kuwa na uhakika unachosema ni kweli hasa ukizingatia kuna utafiti unaonesha/unaodai kuwa Paul Rupia alikuwa Mtanganyika wa kwanza kupata leseni ya kuuza bia na utafiti huo unarejea sheria za wakati huo.

Rejea Justin Willis, "Unpretentious Bars: Municipal Monopoly and Independent Drinking in Colonial Dar es Salaam, " in Dar es Salaam: Histories from an Emerging African Metropolis, ed. J. R. Brennan, A. Burton & Y. Lawi (Dar es Salaam, 2007), 169.
 
Udadisi,

Sina ushahidi zaidi ya hayo niliyoeleza.

Katika historia ya Dar es Salaam Mwafrika wa kwanza kuwa na gari ni Aziz Ali.

Martin Kayamba na Erika Fia hawakuwa watu matajiri hata kidogo wala si watu
ungeweza kuwafananisha na Aziz Ali kwa uwezo.

Kipindi kile ni kipindi mahsusi na mengi nayajua katika historia ya Dar es Salaam
kwa kuwa hao ninaokutajia katika maelezo yangu ni watu ambao wazee wangu
wakiwajua vizuri sana.

Nitakupa taarifa nyingine.
Mwafrika wa kwanza kuwa na radio Dar es Salaam alikuwa Kondo Kipatwa.

Kondo Kipatwa akiishi Ilala.
Kondo Kipwata alikujakuwa rais wa Young Africans katika ya miaka 1960.

Inasemekana Yanga walimpa uongozi Kondo Kipwata baada ya kufungwa na
wapinzani wao Sunderland magoli manne mfululuzi kiasi cha watani wao kuwapa
jina la ''four, four'' yaaani ''nne, nne.''

Kondo Kipwata alikuwa ana sifa moja hakuwa anahudhuria mechi za Yanga
wakicheza na Sunderland.

Yeye alikuwa akisubiri matokeo ya mechi nyumbani kwake.
Wakati wa uongozi wake Yanga ilifanikiwa sana.

Radio ilipoanzishwa Dar es Salaam mwaka 1952 watu wakijumuika barazani
kwake kusikiliza taarifa mbalimbali.

Radio hiyo ilijulikana kama ''Sauti ya Dar es Salaam.''

Mmoja wa watangazaji wa mwanzo wa Sauti ya Dar es Salaam alikuwa Bi.
Mahunda Plantan binti yake Afande Plantan dada yao Mwalimu Sauti Plantan,
Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan.

Sasa usije ukaniuliza nina ushahidi gani kwa haya ninayokueleza.

Hapo ndipo kwenye tatizo, hatuwezi kusema,kwa mfano, Udadisi ni mwafrika wa kwanza kwenda mwezini kisa tumesikia/tumeambiwa na watu wanaomjua, tunahitaji pia kulinganisha na vithibitisho vingine; kwa mfano, una uhakika gani kuwa hakuna waafrika wengine ambao walikuwa na redio kabla ya Kondo Kipatwa?

Yaani hata Mzee Aziz Ali ambaye umetuambia alikuwa mwafrika wa kwanza kuwa na gari, hakuwa na redio kabla ya Kondo Kipatwa ama Kondo ni mzee sana kwa Mzee Aziz Ali?

Na je Affendi Plantain Sykes ambaye inawezekana ni makamo ya Kondo Kipatwa au mkubwa zaidi, hakuwa na redio kabla hasa ukizingatia kuwa umesema alikuwa amefanikiwa na kupandishwa cheo na wakoloni? Kina Martin Kayamba na Erika Fiah hawakuwa na redio?

Je, huyu jamaa hapa chini hakuwa na redio kabla ya Kondo Kipatwa?

Mtoro bin Mwinyi Bakari

Swahili lecturer and author in Germany
Ludger Wimmelbuker
This book presents a study of the life history of Mtoro bin Mwinyi Bakari (c. 1869 - 1927). Mtoro bin Mwinyi Bakari grew up and studied Islamic Sciences in Bagamoyo, Tanzania. He became a Swahili lecturer and author in Germany and is known to have written Desturi za Wasuaheli, an important work in Swahili culture. The book introduces the wider historical context of his writings, and, in particular, reconstructs the racism and discrimination in both the colonial and metropolitan contexts, features which negatively influenced his career and his life as a whole. The study also offers insights into contributions of the colonized to the study of African languages and cultures during this same historical context.

African Books Collective: Mtoro bin Mwinyi Bakari
 
Mimi sina kawaida ya kung'ang'ania kuwa lile nilijualo mimi ndilo hilo hilo la hasha.

Nimeeleza kama nilivyoelezwa na wazee wangu ambao wao ndiyo waliishi miaka
hiyo na wakiwajua watu hawa.

Endapo wewe utakuwa unajua vinginevyo hapana tabu nitakusoma na nitakuwa
umenipa maarifa ambayo sikuwanayo.

Ila mfano uliotoa wa Martin Kayamba, Affendi Plantan na Mtoro Mwinyi Bakari
umenifahamisha kitu kimoja kwako kuwa huna ujuzi wa historia ya Tanganyika.

Hao wote uliowataja wamekufa radio bado hazijaingia Tanganyika.
Matangazo ya radio yalianza mwaka 1952.

Nadhani tumefahamiana vizuri.
 
Hapo kila swali lina maana kimethodolojia, nachotaka ni uthibitisho/ushahidi wa yale uliyoandika, yaani mtu anathibitishaje na kuwa na uhakika kuwa ni kweli - je, kwa kurejea tunachoambiwa tu au pia kwa kulinganisha na vithibitisho na kadhalika?

Kwa mfano, ningependa kuona sheria au tamko lilitoa ruhusa hiyo ya kunywa bia kuthibitisha ulichoandika; hiyo itasidia, kwa mfano, nikitaka kukunukuu nawezaje kuwa na uhakika unachosema ni kweli hasa ukizingatia kuna utafiti unaonesha/unaodai kuwa Paul Rupia alikuwa Mtanganyika wa kwanza kupata leseni ya kuuza bia na utafiti huo unarejea sheria za wakati huo.

Rejea Justin Willis, "Unpretentious Bars: Municipal Monopoly and Independent Drinking in Colonial Dar es Salaam, " in Dar es Salaam: Histories from an Emerging African Metropolis, ed. J. R. Brennan, A. Burton & Y. Lawi (Dar es Salaam, 2007), 169.

Mdadisi,
Wajua hapa nilipo nacheka peke yangu.

Huyo James Brennan...
Huyu hapa chini.

Picha hiyo tumepiga mwaka 2006.
Tunajuana kiasi sasa miaka 20.

Kilichotukutanisha ni historia ya Tanganyika.
Nadhani maelezo haya yatakutosha.

CIMG0236-1.JPG

Mdadisi,

Brennan kanipa lifti ya gari yake kutoka Ohio kwenda Chicago nikapande
ndege kwenda New York.

Tulipofika Mto Mississippi akawa ananieleza habari zake.

Mimi nikamwambia, ''Jim dont waste your breath I know the river.''

Brennan akawa kashangaa vipi huyu mtu wa Kariakoo aseme anaujua
Mto Mississippi?

''I used to have two friends here once upon a time...Huckleberry Fin
and Tom Sawyer...'' Nikamwambia.

Hakika alikuwa amepigwa na butwaa.
''Mohamed you amaze me.''

Huyu ndiye James Brennan na mimi.
Maktaba yake ndiyo maktaba yangu.
 
Hiyo nukuu ni ya Justin Willis, sio ya Jim Brennan, asante lakini kwa kutuongezea visa mkasa
 
Mdadisi,
Mimi sina kawaida ya kung'ang'ania kuwa lile nilijualo mimi ndilo hilo hilo la hasha.

Nimeeleza kama nilivyoelezwa na wazee wangu ambao wao ndiyo waliishi miaka
hiyo na wakiwajua watu hawa.

Endapo wewe utakuwa unajua vinginevyo hapana tabu nitakusoma na nitakuwa
umenipa maarifa ambayo sikuwanayo.

Ila mfano uliotoa wa Martin Kayamba, Affendi Plantan na Mtoro Mwinyi Bakari
umenifahamisha kitu kimoja kwako kuwa huna ujuzi wa historia ya Tanganyika.

Hao wote uliowataja wamekufa radio bado hazijaingia Tanganyika.
Matangazo ya radio yalianza mwaka 1952.

Nadhani tumefahamiana vizuri.

Kuuliza sio ujinga, maswali yangu ni ya kujifunza, matamko ya uhakika yanahitaji uthibitisho mfano siwezi kusema mlima mrefu kuliko yote ni Mlima Kilimanjaro kama sijui urefu wa Mlima Meru, tafadhali jibu au, maswali mengine yapo njiani kadri navyoendelea kusoma kitabu chako; na kama umeona nauliza pale tu ambapo napata utata au napokosa ushahidi - sote tunajua ku-triangulate ni mbinu muhimu katika utafiti, hicho ndicho tunachofanya hapa, hivyo tuvumiliane hivyo hivyo tu.
 
Back
Top Bottom