Sharif kulia kwa JKN ni Bilal Mshorwa liwali kutoka Tabora na kulia Ahmed Saleh liwali Dar. Ntakufahamisha kuhusu Mangara Tabu.
Sheikh
Mohamed Said,
Huyo
Bwana Liwali Bilal Mshorwa...nafikiri huyo itakua ndo Babuye
Bwana Bashir Mshoro...japo
sina hakika kubwa kwalo?!
Hawa ndugu zetu kama ndo wao ,basi family yao ina history ndefu pale Tabora khasa kwenye Ilm,biashara na mangineyo!
Nafikiri naliwahi kuzungumza kiduchu na
Kahtaan,kuhusu watu/family hiyo...kwenye thread fulani humuhumu-JF!
Bwana Bashir Mshoro,pana wakti alikua ndo Chief Accountant na baadae Branch Manager wa ile NMC pale Arusha.
Pia aliwahi kuwa mmojawapo ya ma-Commisioners wa awali pale TRA...mara ya mwisho nalisikia alikua kwenye shughuli za siasa na aliwahi kugombea Ubunge pale Tabora mjini!?
Nalimfahamu huyo Bwana kupitia mmojawapo ya Uncle zangu...ndo nikapata hiyo
history kiduchu ya family yao pale
Tabora na ukarimu walokua nao kwa ndugu zao na wageni woote walokua wakipitia pale Tabora zama hizo,kwa shughuli mbalimbali!
Nasikia yakua,pia walikua na
Madrasat/Islamic Seminary kubwa pale Tabora zama hizo...na wakitoa Ilm kwa ndugu na jamaa wengi mno kutoka takriban pembe nyingi za hiyo
Tanganyika na hata
Zanzibar!?
Nitajaribu kumtafuta huyu Bwana Bashir Mshoro ili kuthibitisha haya!?...na kama ndo wao,basi nitakujuza pindi tukikutana penye majaaliwa.
Bakhti mbaya huyo Uncle yangu alokua very close na Bwana Bashiri Mshoro...amefariki/ametangulia mbele ya haki maskini,myka michache ilopita! Maana walisoma woote pale
Tabora School,na Wazee Wao/families zao pia zikijuana na kufahamiana kwa ukaribu mno.
Ahsanta.