Ritz,
Picha hii ilipigwa mwaka wa 1968.
Katika picha hii kuna vijana kutoka ukoo wa
Tambaza, Sykes, Mwapachu na
Mtemvu.
Wazee wa hao wote wameacha alama katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Inawezekanaje mimi nisiijue historia ya watu hawa na mchango wao katika kupigania uhuru
wa Tanganyika?
Mimi ni mmoja wa hao waliopo kwenye picha hiyo.
Ritz,
Picha hii ilipigwa katikati ya miaka ya 1950 wakati harakati za uhuru ziko moto sana.
Picha hii ilipigwa Mtoni kwenye shamba la Sheikh
Abdallah Idd Chaurembo ambae kwenye picha ni huyo alievaa
hegal kakaa chini mkono wa kulia wa picha.
Mtafute
Nyerere kwenye picha hii.
Mtafute
Rupia kwenye picha hii.
Hawa unaowaona wamemzunguka Nyerere ndiyo waliokuwanaye wakati wa kupigania uhuru.
Hawa ndiyo wazee wetu waliokujasahauliwa na historia zao kufutwa.