Maswali na Majibu kuhusu Kitabu cha Mohamed Said

Chamviga,
Ahsante sana.

Ndugu zetu wanachomwa sana na historia hii kama vile Mjerumani Krapf
alivyochomwa na ustaarabu wa Chifu Kimweri alipomkuta Vuga.

Kamkuta Kimweri na wanae wote wanajua kusoma na kuandika na waungwana.
Krapf kaja kukutana na ''washenzi'' anakutana na wastaarabu.

Hii saikolojia bado wanayo hawa ndugu zetu.
Duniani kote nilikoalikwa kuhadhir Alhmadulilah nimepongezwa na kupigiwa makofi.

Cha ajabu kipi hapa JF?

Mzee MS naomba ufafanuzi unapotumia neno "hawa ndugu zetu" unamaanisha ni kina nani hao?
 
Mzee wangu hawa wala wasikuumize kichwa....kama wanaona ulichoandika kwenye kitabu chako sio sahihi, watoe vitabu vyao waweke historia yao wanaohisi ni sahihi...

Mimi ninacho kitabu chako na naheshimu mtu yeyeto anayetoa kitabu.....hao nao watoe vyao tusome tuone
Unaposema hawa, hawani kina nani hebu be specific.
 
Kwa kweli Maswali ni Mazuri, ni maswali yanayohitaji uafafanuzi wa njia gani ilitumika kupata hizo data (Research, mapokeo nk), mimi sioni ubaya wowote wa hayo maswali.

Tatizo kubwa linalonisikitisha ni uwa kuna watu Ritz, gombesugu faizafox nk, wanaona mapungufu yaliyopo kwenye simulizi za Mohamed Said lakini hawawezi kuyasema hapa,
wengine tuko humu kujifunza na kuchukua vilivyosahihi kwa faida ya vizazi vijavyo,
mtu anaposema fulani ndio alikuwa mtu wa kwanza kumiliki Radio Dar es salaam? au alikuwa wa kwanza kuwa na gari au ndio waafrika wa kwanza waliruhusiwa kunywa pombe hapo ndio watu tunapohitaji ufafanuzi kidogo, lakini kama haya hayakuwekwa wazi na wanayoyajua basi kinachosimuliwa hapa hakitakuwa na tofauti na vilivyosimuliwa sehemu nyingine kwani zote zitakuwa ni habari za upande mmoja zenye kuegemea sehemu ama jamii fulani ya watu
 
Last edited by a moderator:
Kituko kwani kalazimishwa mtu kuamini?

Mkubwa mimi wala siko huko kwa kusema kulazimisha watu wayaamini hayo unayoyaandika, lakini wewe uliandika hicho kitabu ili kusahihisha makosa uliyoyaona kwenye vile vitabu vya "Kivukoni" kwa maana uliona ile historia ina mapungufu,

angalizo nililokuwa naliweka ni kuwa umakini na usahihi wa maelezo unatakiwa ili na wewe usije kuandika tena mapungufu mengine. hayo maswali ya Mdadisi ni changamoto za kuangalia usahihi wa data na maelezo yako,
mwaka 1952 ni zamani lakini mji ulikuwa umechangamka kwa kiasi chake, maeneo kama , Magomeni yalishakuwa na watu wa kutosha tu na kulikuwa na waafrika wengi tu waliokuwa wanajiweza hta huko kununua redio na hata hiyo Kariakoo yenyewe pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa na uwezo huo na walikuwa nazo hizo redio

hili la redio hujaliweka kwenye kitabu chako lakini mimi nalizungumzia kwa sababu nimelisoma kwako, sasa kama hili lina mushkel hayo mengine tuyaamini vipi?

na hata wanaokusupport, "watoto" wenzio wa Kariakoo Ritz wana mashaka na hilo
 
Last edited by a moderator:
17. "Abdulwahid confided with the TAA executive that having the most educated African in the land [i.e. Julius Nyerere?] would strengthen its leadership and portray a good image before the eyes of the colonial government and the United Nations Visiting Mission" (p. 113)(p. 113-114)

"After completing his primary education at the Mission of Rutabo, where he learned to read and write his native dialect, besides English, Latin, Italian and Swahili, Laurean [Rugambwa] entered the Regional Grand Seminary of Katigondo, Uganda, under the care of the White Fathers. Ordained to the Priesthood at 31 years of age on December 12, 1943, by Bishop Burkhard Huwiler M.Afr., he pursued further studies at the Scientific Missionary Institute De Propaganda Fide in Rome, Italy, between 1948 and 1951, obtaining a Doctorate Magna Cum Laude in Canon Law" - http://www.findagrave.com/cgi-bin/fg.cgi?page=gr&GRid=88295422
 
Wala usiamini hakuna shida.

Kaka Mohamed Said, shida ipo,
hicho sio kitabu cha kufungiwa ndani , ni kitabu cha maarifa, cha kuelimisha na kupashana habari za matukio yaliyotukia siku za Nyuma, ni kitabu cha manufaa wa wale ambao hawakuwepo kipindi hicho na hata kwa wale waliokuwepo lakini hawakuwa na nafasi sahihi ya kupata habari hizo ulizoziweka

unaposema hhawa ndio waliokuwa waafrika wa kwanza kupewa kibali cha kunywa beer, lazima mtu ajiridhishe na utafiti wako ulipoupata, ulisoma huo waraka wenye ruhusa au ni dogma za vijiweni tu?
 
Last edited by a moderator:
Mkubwa mimi wala siko huko kwa kusema kulazimisha watu wayaamini hayo unayoyaandika, lakini wewe uliandika hicho kitabu ili kusahihisha makosa uliyoyaona kwenye vile vitabu vya "Kivukoni" kwa maana uliona ile historia ina mapungufu,

angalizo nililokuwa naliweka ni kuwa umakini na usahihi wa maelezo unatakiwa ili na wewe usije kuandika tena mapungufu mengine. hayo maswali ya Mdadisi ni changamoto za kuangalia usahihi wa data na maelezo yako,
mwaka 1952 ni zamani lakini mji ulikuwa umechangamka kwa kiasi chake, maeneo kama , Magomeni yalishakuwa na watu wa kutosha tu na kulikuwa na waafrika wengi tu waliokuwa wanajiweza hta huko kununua redio na hata hiyo Kariakoo yenyewe pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa na uwezo huo na walikuwa nazo hizo redio

hili la redio hujaliweka kwenye kitabu chako lakini mimi nalizungumzia kwa sababu nimelisoma kwako, sasa kama hili lina mushkel hayo mengine tuyaamini vipi?

na hata wanaokusupport, "watoto" wenzio wa Kariakoo Ritz wana mashaka na hilo
Naona unawashwa wewe wapi mimi nina mashaka usipende kunisemea wakati mim nipo.
 
Last edited by a moderator:
Naona unawashwa wewe wapi mimi nina mashaka usipende kunisemea wakati mim nipo.

kuwashwa nini tena kaka, na wewe ndio umekuwa wa lugha hizo?,

tatizo kaka huwezi kuwa wazi hata kama kuna mapungufu
 
Kwa kweli Maswali ni Mazuri, ni maswali yanayohitaji uafafanuzi wa njia gani ilitumika kupata hizo data (Research, mapokeo nk), mimi sioni ubaya wowote wa hayo maswali.

Tatizo kubwa linalonisikitisha ni uwa kuna watu Ritz, gombesugu faizafox nk, wanaona mapungufu yaliyopo kwenye simulizi za Mohamed Said lakini hawawezi kuyasema hapa,
wengine tuko humu kujifunza na kuchukua vilivyosahihi kwa faida ya vizazi vijavyo,
mtu anaposema fulani ndio alikuwa mtu wa kwanza kumiliki Radio Dar es salaam? au alikuwa wa kwanza kuwa na gari au ndio waafrika wa kwanza waliruhusiwa kunywa pombe hapo ndio watu tunapohitaji ufafanuzi kidogo, lakini kama haya hayakuwekwa wazi na wanayoyajua basi kinachosimuliwa hapa hakitakuwa na tofauti na vilivyosimuliwa sehemu nyingine kwani zote zitakuwa ni habari za upande mmoja zenye kuegemea sehemu ama jamii fulani ya watu
Wewe kauzu kweli kinachokusikitisha wewe nani umelazimishwa kuamini mijitu mingine bana.

CC; Tayeb Mipangomingi mfumo
 
Last edited by a moderator:
Ni kitabu cha kijiweni.

kama wewe unakiona hivyo (cha kijiweni) sawa, lakini mimi nakipa uzito, nimeyajua mengi kupitia hichi kitabu, ninakipa credit sana, ila kwenye walakini na mashaka ndio unahitajika ufafanuzi
 
kuwashwa nini tena kaka, na wewe ndio umekuwa wa lugha hizo?,

tatizo kaka huwezi kuwa wazi hata kama kuna mapungufu
Wewe utakuwa unawashwa kwa nini uniwekee maneno mdomoni wapi mimi nimesema mapungufu ya Mohamed Said, hii lugha nimeitumia kwako kutokana kuni quote kipuuzi.
 
Last edited by a moderator:
Wewe utakuwa unawashwa kwa nini uniwekee maneno mdomoni wapi mimi nimesema mapungufu ya Mohamed Said, hii lugha nimeitumia kwako kutokana kuni quote kipuuzi.

asante kaka
naomba uelewa wako kuhusu hili la Kleist na Azizi Ali ndio walikuwa waafrika wa kwanza kuruhusiwa kunywa beer hapa Dar es salaam
 
Wewe kweli Kituko halafu unataka kujibiwa majibu gani kama siyo ya kipuuzi.

Wapi Mohamed Said kataja mambo ya bia, ndiyo maana nakuambia unawashwa wewe si bure.
 
Last edited by a moderator:
asante kaka
naomba uelewa wako kuhusu hili la Kleist na Azizi Ali ndio walikuwa waafrika wa kwanza kuruhusiwa kunywa beer hapa Dar es salaam

hata mie wanajamvi nngependa kujua kuhusu hili
 
Back
Top Bottom