Ntuzu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 17,418
- 10,877
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hili swali lanihusu Mimi Au?
Cool running unaongea na mtu mzima tena mwenye busara sana kuliko unavyomfikiria. Ni vyema kama unaitaji elimu maneno yenye muelekeo ya kupotosha au kejeli yakaepukwa ili kuendeleza mjadala huu. Mimi nipo kitambo katika mjadala huu nafuatilia kwa makini na sipendi ufungwe bali nataka niendelee kupata ujuzi wa historia ya nchi yangu.
Ndugu gombesugu nilidhani tumeshalimaliza hili suala. Kwa kweli dhamira/nia yangu ni safi kabisa. Hakika mimi ni muumini wa kisomo/elimu ya wazi. Huu mjadala ningeufanya peke yangu na Mzee Mohamed Said kwa njia ya barua pepe tungekosa michango ya watu wengine. Huu ni mjadala wa wazi wa kuiboresha historiografia yetu.
Hapa nilitegemea wajuvi wa historia kama wewe muwe mnachangia kwenye hizo nukuu za kitabu chake, ama kuzishibisha kwa rejea zingine, majina ya wahusika wengine, wasifu au visa mkasa zaidi. Na mkifanya hivyo inatusaidia hata watafiti wanagenzi kama mimi kuzifuatilia na kutimiza azma ya Mzee wetu Said ya kuiweka wazi historia iliyoweka pembezoni.
Tusiogope. Tuvumiliane. Tujadiliane.
Yote ya nini haya?
Mzee wangu hawa wala wasikuumize kichwa....kama wanaona ulichoandika kwenye kitabu chako sio sahihi, watoe vitabu vyao waweke historia yao wanaohisi ni sahihi...
Mimi ninacho kitabu chako na naheshimu mtu yeyeto anayetoa kitabu.....hao nao watoe vyao tusome tuone
Kimambo na Temu wameandika historia ya Tanzania.
Hamna kitu na wala hakuna aliyewauliza.
Mzee wangu hawa wala wasikuumize kichwa....kama wanaona ulichoandika kwenye kitabu chako sio sahihi, watoe vitabu vyao waweke historia yao wanaohisi ni sahihi...
Mimi ninacho kitabu chako na naheshimu mtu yeyeto anayetoa kitabu.....hao nao watoe vyao tusome tuone
Hakuna mtu katika mjadala huu aliysema kitabu cha Mohamed Said sio sahihi, tafadhali rejea tena mtiririko wa mada
Sijawahi
Temu na Kimambo hawajaandika historia ya Tanzania, wamehariri kitabu chenye sura zilizoandikwa na waandishi wengi
Kitabu ambacho tunaweza kusema ni cha historia ya Tanzania ni cha John Iliffe, yeye hayupo JF hivyo hatuwezi kumuuliza
Hapa hatujaja kubishana, tumekuja kujadiliana ili kuboresha uandishi na utafiti wa historia ya Tanzania/Tanganyika/Zanzibar
Kwa jinsi ulivyo mdadisi wa ukweli, naomba ufanye hivyo...nasema hivi sababu naona unaweza, pili waandishi wa Tanzania huoni vitabu vyao kwenye maktaba za nchi jirani kama zambia, Zimbabwe, Malawi na Botswana...
Waandishi wengi wamejikita kwenye riwaya za kipuuzi....
Mdadisi,
Kama kweli una nia ya kuboresha nakushauri kaboreshe kitabu cha Historia ya
TANU kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni.
Ninapomweleza mtu kuwa TANU Tanganyika ilizungumzwa kati ya Abdu Sykes
na Chifu Kidaha Makwaia mwaka wa 1950 kwenye chakula cha jioni nyumbani
kwa Abdu, wewe unataka kuboresha kitu gani?
Au ndiyo hiyo TANU kajanayo Nyerere?
Unataka unifunze mimi historia ya wazee wangu?
Mimi ni muhali sana kujua historia ya wazee wako vipi wewe uijue ya watu
wangu kiasi cha kutaka uisahihishe?
Niwie radhi na kubali uamuzi wangu sina haja ya kujadili hili na wewe.
Ukipenda andika pitio la kitabu changu na sema lolote upendalo.
John Iliffe kafanya hivyo, James Brenan kafanya hivyo, Jonathan Glassman
kafanya hivyo.