Maswali na Majibu kuhusu Kitabu cha Mohamed Said


Ina maana 1952 kina Adam Sapi Mkwawa, Paulo Bomani, Paul Rupia wote hawakuwa na redio? Swali la msingi la kimethodolojia hapa ni: Mbinu gani umetumia kuthibitisha (kwa uhakika kabisa) kuwa Kondo Kipwata ndiye alikuwa Mwafrika wa kwanza kuwa na redio? Ina maana hata watoto wa matajiri Kleist Sykes na Aziz Ali walipata redio baada yake?
 

Udadisi,

Ikiwa wewe una taarifa kuwa Kondo Kipwata hakuwa Mwafrika wa kwanza
Dar es Salaam kununua radio hapana neno ni sawa tu.

Mimi nimeeleza kama nilivyopokea kwa hao waliokuwapo nyakati hizo.
 
Udadisi,

Unachofanya sio kuuliza kwa ajili upate jawabu ya maswali, unachokifanya ni cross examination ya kumsuta Maalim Mohammed Said. Kama bingwa wa kufanya research kwanini hufanyi yako kwa nguvu zako halafu ukatoa counter sessith au rebutal book dhidi ya kitabu chake? Ninachokiaona hapa ni kama vile undegraduate anafanya utafiti lakini wakati huo huo unqogopa kutumia marejeo ya kitabu chake kwa sababu yana maana na humpendi au umeshawishiwa kuwa usitumie marejeo katika maandishi yake lakini moyo haukupi.

Pls jifunze kujieleimisha kwa upole na juhudi sio kukebehi kazi za watu na hali wewe mwenyewe ni mwanagenzi bado.
 
Last edited by a moderator:

sina chuki binafsi na mohamed said, mimi ni msomaji wake mzuri tu; nimemnukuu sana kwenye maandishi yangu; sasa nafanya utafiti wa kina na vizuri nijiridhishe kabisa kabla sijanukuu baadhi ya vitu muhimu, kwa mfano nahitaji sana kunukuu hilo la mwafrika wa kwanza kuwa na motokaa na hilo la waafrika wa kwanza kuruhusiwa kunywa bia.

pia kumbuka mohamed said amepata fursa ya kupewa makabrasha muhimu sana ya familia ya sykes. na pia uhakiki wa vitabu ni utaratibu mzuri sana wa kuboresha vitabu. kwa mfano, mchakato huu unaweza kusaidia atoe toleo jipya la kitabu hicho ambalo linaweza kuwa na vithibitisho zaidi. tuvumiliane tu badala ya kudhani kila mtu anayemhoji ana chuki binafsi.
 

Na huu hapo chini ni uthibitisho wa jinsi navyouheshimu mchango wa Mohamed Said, sasa nakisoma tena hicho kitabu na kila napokutana na hivyo vitu ambavyo vinanitatiza naviuliza hapa, na sio lazima ajibu yeye tu, wengine mnaojua jibuni pia.

"With slight modification the same argument can be extended to Mohamed Said's (1998) Abdulwahid Sykes (924-968): The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika. Nyerere and Sykes were both elites as far as their social status in the colonial context and political position in the struggle for independence were concerned, however, one became marginalized in the nationalist historiography presumably because he belonged to a religious group that was ostensibly being forced into becoming a subaltern category" - http://udadisi.blogspot.com/2013/10/nationalist-historiography-of.html

cc: Mohamed Said
 
Last edited by a moderator:

Averoes,
Mambo haya yana matatizo yake kwa hawa ndugu zetu.

Kilipochapwa hiki kitabu Uingereza kikaja nchini na kuanza kusambazwa kilileta
mtafaruku mkubwa.

Kubwa zaidi cha kwanza ni kuwa ''brains'' nyuma ya TANU hakuwa Nyerere
bali Abdulwahid Sykes.

Wapenzi wa Mwalimu Nyerere walipigwa na mshtuko mkubwa wa kufa mtu.

Kiasi kitabu na mimi nikajadiliwa katika ngazi za juu kuwa huyu Mohamed Said
ni nani?

Nikafahamika kuwa ni kijana wa Kidaresalama na wazee wake walikuwa ndani
ya harakati za uhuru na wakifahamiana na Nyerere toka alipofika Dar es Salaam.

Kuna waliotaka ''nishughulikiwe'' kwa kuandika kitabu hiki.

Kuna mmoja akauliza, ''Huyu Mohamed aliandika hiki kitabu kwa Kiswahili
kwanza kisha kikatafsiriwa?''

Hii ilikuwa husda.
Hata huyu Mswahili atakuwa na Kiingereza hiki?

Kuna katika jamaa zetu heshi kuandika akisema kuwa, ''Ukisoma kitabu
cha Mohamed Said utajua kuwa kimeandikwa na ''native speaker.''

Hasad inakula moyo wake.
Alichokiona katika kitabu kizima ni hicho Kiingereza basi na kikamuuma.

Nakala moja ya kitabu hiki kipo East Africana Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Wanafunzi wanakatazwa na walimu wao wasikiweke katika rejea zao kwa
kuwa Mohamed Said si ''academician.''

Kwa utangulizi huu unatosha kuelewa vipi ndugu zetu wanavyokitazama
kitabu hiki na wanavyotuangalia.

Kwa hiyo basi kwa haya niliyokuwekea hapa nadhani wewe utakuwa na maswali
mengi ya kujiuliza.

Hii cross examination mimi hainipi tabu hata kidogo.
In Sha Allah nitatoa ushirikiano wa kutosha kabisa kwa Mdadisi.

Nina kitabu cha shule za msingi, ''Torch on Kilimanjaro,'' Oxford University Press,
Nairobi toka 2007.

Oxford kwa utaalamu wao huwa hawachapi kazi mbovu.

Hiki ni kiabu cha mwanafunzi wa msingi kujifunza Kiingereza na wakati huo huo
kusoma historia ya nchi yake.

Huu ni mradi wa Afrika ya Mashariki na Kenya wanavyo vitabu kama hiki cha kwangu
maarufu ni, ''The Kapenguria Six,'' kuhusu kifungo cha Kenyatta na wenzake.

Wizara ya Elimu wamekipiga vita.
Hasad inawala na mfumo uko kazini.
 

Averoes,
Hebu angalia hii hapa chini:

 
Sheikh Mohamed Said nakufuatilia mno na hizo bayana zako.
 
Last edited by a moderator:

Kwani waislam wanaruhusiwa kunywa bia mzee wangu?hata hivyo kwenye historia uko vizuri sana ingawa natofautiana nawe ktk mambo machache!
 
Samahani jamani, mimi ndio natafuta hiyo copy ya kitabu cha mzee wetu huyu niweze kusoma nakujua zaidi, lakini NINI SWALI MOJA TU DOGO, hiki kitabu kimejikita katika tafsiri ya DHANA GANI? kuwa kwa mfano Historia inatengenezwa na WATU WACHACHE maarufu? au JAMII?

Kwa haraka haraka naona na wewe umeingia kwenye mtego wa HISTORIA INATENGENEZWA NA WATU MAARUFU WACAHCHE, ambao ndio naona kama unaupinga hapa. Nadhani historia ya Uhuru wa Tanganyika si Dar es Salaam na Watu wa Dar es Salaam ndio walioshiriki, ni watu wengi wa dini mbalimbali na sehemu tofauti. Kwa mfano soma kitabu cha Kimambo na Temu (1969/1997) A History of Tanzania kidogo wameweka watu wengi kidogo ingawa na chenyewe kiliandikwa katika mtazamo wa afrocentric zaidi.

La muhimi sasa tujikite katika kuandika historia shirikishi hasa inayowashirikisha watu wa chini (underdogs) kwani nao wanamchango katika historia yetu. Tusibishane kuhusu tu hawa watu maarufu hiyo sio historia nzuri bali inakuwa historia ya watu wakubwa, hii inajengwa katika mtazamo unaoitwa BOURGEOIS PERSPECTIVE.
 

Gakato,

Msimamo wako ndiyo msimamo wangu.

Nilinyanyua kalamu baada ya kuona zimeandikwa historia ambazo zimewaweka
pembeni wahusika wakuu.

Mathalan huwezi kuandika historia ya TANU bila Abdulwahid Sykes, Sheikh Hassan
bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate kwa uchache.

Hii ni Dar es Salaam.

Jimbo la Kusini huwezi kuandika historia ya uhuru bila kumtaja Sheikh Mohamed
Yusuf Badi, Yusuf Chembera, Salum Mpunga, Ali Mnjale, Suleiman Masudi Mnonji.

Hii kwa uchache.

Kilimanjaro huwezi kutomtaja Mzee Mbowe, Mama biti Maalim, Yusuf Olotu, Bi
Halima Selengia, Juma Ngoma.

Kwa uchache.

Jimbo la Magharibi.

Huwezi kutomtaja Bilal Rehani Waikela, Abdallah na Maulid Kivuruga, Fundi
Muhindi, Dharura biti Abdulrahman.

Nk. nk. nk.

Umekitaja kitabu cha Kimabo na Temu...
Sikuwaona hao ''watu wengi.''
 

Hunitendei haki. Mimi nakunukuu sana, nimeweka rejea ya mfano hapo juu labda hujaiona. Naiweka tena hapo chini. Wewe kama mwandishi unapaswa kufurahia kitabu chako tunapokisoma kwa makini na kukifanyia hicho kinachoitwa "cross-examination" . Sasa niko ukurasa wa 80 na maswali niliyouliza kupata uthibitisho/ushahidi ni 7 tu, huoni hiyo inamaanisha kuwa kuna mengi tu humo ambayo sijaona kama yana utata wowote na hivyo kuhitaji ufuatiliaji na maelezo zaidi ndugu?

"With slight modification the same argument can be extended to Mohamed Said's (1998) Abdulwahid Sykes (924-968): The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika. Nyerere and Sykes were both elites as far as their social status in the colonial context and political position in the struggle for independence were concerned, however, one became marginalized in the nationalist historiography presumably because he belonged to a religious group that was ostensibly being forced into becoming a subaltern category" - http://udadisi.blogspot.com/2013/10/...graphy-of.html
 

Mdadisi,
Niwie radhi ikiwa unaona labda majibu yangu hayendi sawa na mategemeo yako.

Labda nami nikuulize hadi hapo ulipofika...
Kipi kipya kwako hukuwa unakijua kabla?

Umekijua baada ya kukisoma kwangu.
 

Mdadisi,
Jibu la swali la 3.

Kleist kabla hajafariki aliandika maisha yake na mswada huu alikuwa nao mwanae Abdulwahid Sykes kuanzia mwaka 1949 alipokufa baba yake.

Katika mswada huo ndimo mlimo taarifa za maisha ya Klest Sykes katika Vita Vya Kwanza 1914 - 1918 yeye akiwa askari katika jeshi la Wajerumani chini ya Von Lettow Vorbeck.

Kifo cha Affendi Plantan kiliwakuta Kleist na na ndugu yake Schneider Abdillah Plantan Mwele Juu, Tanga walipokwenda kupambana na majeshi ya Waingereza yaliyokuwa yanatokea Kenya kupitia Taveta.

Katika mswada huo ndimo Kleist anaeleza kuwa walipopata taarifa za kifo cha Affendi Plantan wakiwa Mwele Juu walipewa likizo kurejea Dar es Salaam katika msiba wa baba yao na Kleist akaeleza kuwa kwa heshima ya Affendi Plantan Wajerumani walisimamisha
mapigano.

Affendi Planta ndiye aliyekuwa Kiongozi wa Germany Constabulary katika Tanganyika na aliingia nchini kama mamluki akifuatana na Herman Von Wissman miaka ya mwisho ya 1800 akitokea Mozambique kijiji cha Kwa Likunyi, Imhambane.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Balozi Abbas Sykes akihojiwa na mwandishi katika kipindi cha televisheni nyumbani kwake Sea View[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mdadisi,
Niwie radhi ikiwa unaona labda majibu yangu hayendi sawa na mategemeo yako.

Labda nami nikuulize hadi hapo ulipofika...
Kipi kipya kwako hukuwa unakijua kabla?

Umekijua baada ya kukisoma kwangu.

Mengi sana, kwa mfano, kuna majina ya watu wengi tu humo nilikuwa siyajui; pia sikuwa najua kuhusu 'majungu' dhidi ya 'wasauzi' wa dar ila hilo limeniletea swali la (8), niko mbali na kitabu hivyo nitaliuliza baadaye maana nataka kuweka nukuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…