MKALIKENYA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,196
- 486
kama Bwana Malinzi havunji sheria yeyote basi sioni kama kuna haja ya yeye kuachia uongozi wa KRFA labda tuu iwe kwasababu ya ufanisi na kuachia wengine
Angalia amevunja Timu yetu nzuri ta T-Stars na kuanzisha Chekechea yake.Hii ni kurudisha nyuma maendeleo ya Soka.
Jamal Malinzi
Kwa mara ingine unaleta mzaha kwenye maswali muhimu sana!Onyesha japo seriousness kidogo!Waambie hivi KRFA HAUNA KITU UTACHOSHINDWA kuwafanyia KRFA kwa nafasi yako ya U-Rais wa TFF!
Tuache majibu ya kisiasa kwenye issue muhimu kama hizi!JIUZURU haraka maana unaonyesha wazi wazi u dikteta wako!!
Malafyale ukitaka niwe najibu hoja zako tumia lugha ya uungwana,who is joking here?
rubaman huyu asikutishe,kashindwa kazi aliyochaguliwa kaanza sasa kuleta sera za ajabu kwenye soka letu!Kuokota wachezaji wa mitaani tusiojua wametoka wapi na waliandaliwa na nani kabla hawajaitwa Stars sio tu ni kichekesho bali kinaonyesha Jamal Malinzi aligombea TFF bila kuwa na sera zozote za kumuongoza!Jamal Malinzi, hivi katika hiyo comment ya bwana Malafyale kuna lugha gani isiyo ya kiungwana au kukuvunjia heshima?
Jamal Malinzi, hivi katika hiyo comment ya bwana Malafyale kuna lugha gani isiyo ya kiungwana au kukuvunjia heshima?
Kocha mpya wa timu ya Taifa atakuwa Mholanzi Mart Nooij.Aliwahi kuifundisha timu ya vijana ya Burkina Faso,akawapeleka Msumbiji fainali za Afrika na kwa sasa alikuwa anafundisha St George ya Ethiopia.
Kocha mpya wa timu ya Taifa atakuwa Mholanzi Mart Nooij.Aliwahi kuifundisha timu ya vijana ya Burkina Faso,akawapeleka Msumbiji fainali za Afrika na kwa sasa alikuwa anafundisha St George ya Ethiopia.
Ligi inaelekea ukingoni,ili kuongeza ushindani msimu ujao wadau na wapenzi wa mpira mnaonaje tukiipanua ikawa ya timu 16 badala ya 14 za sasa?
Kaka Jamal; hoja yangu kwako kwa sasa ni ndogo sana.
timu ya Taifa isiwe mahali pa kukuzia vipaji.
Kila timu ya Premier League (ya Tanzania) si inayo timu ya vijana?
Tena bado kuna timu za vijana za Taifa?
Timu ya taifa inafaa iwe ni mkusanyiko wa wachezaji waliofanya vizuri kutoka katika timu zao.
Kujaza machipukizi taifa kutachelewesha sana mafanikio.🙂
Rubaman kulikuwa hakuna sababu ya malafyale kumwambia ndugu rais kuwa anaonesha UDIKTETA wake hapo kamuhukumu moja kwa moja kuwa ni dikteta kitu ambacho sitaki kuamini rais wa TFF bwana Malinzi yupo hivyo sababu kwa kufungua tu ukurasa huu kaonesha jinsi gani anaweza kusikiliza mawazo ya wengine kitu ambacho ni kinyume kabisa na utawala wa kidikteta mimi nadhani tumuulize rais maswali magumu na kumpa solution na yeye awe tayari kusikiliza asiwe mtu mwenye majibu ya kila kitu.
watu hawajui Kama ukiweza kuchukua ulilokosolewa ukalifanyia kazi ni jambo Zuri? Na hili ndio watu wetu wengi wakikosolewa kwa kusaidiwa wafanye kitu gani wao wanaona Kama wanachukiwa si kweli na neno Dikteta si baya linakuja vibaya Kama unachofanya ni kibaya na ukiambiwa rekebisha hivi mtu hutaki kusikiliza mtu anakupa wazo uweke sawa , kwajili sio yake yeye peke yake anataka ubadilike kuweka mambo sawa kwa wanadamu wengi sasa ukitoka kurizisha kigroup tu chako mtu peke yenu itafika siku hata hicho kigroup Chenu mnachopeana Nguvu nini cha kufanya kitavunjika kirahisi wote mtakosa bora asikilize wengi aweke sawa ataweza kuendelea kwa amani.Kwa hiyo kumpa mtu negative assessments ni kumnjia heshima? Je angemwambia yeye ni kiongozi bora si ingekuwa ni kumhukumu(positively) kutokana na staili ya uongozi wake? Ni vizuri kwa Malinzi kufungua ukurasa huu kusikiliza mawazo ya watanzania wapendao soka vile vile awe tayari kusikia negative na positive comments, constructive criticisms, assessments za kila mtu. It's the price to be on the spotlight. Viongozi wa kibongo huwa wanapenda kusifiwa kila siku, aki criticiziwa anakuja juu. Huu sio ukomavu wa uongozi. Bwana Malafyale alichosema kimetokana na Rais wa TFF kung'ang'ania madaraka ya kimkoa na kitaifa kama isingekuwa hivyo naamini neno la UDIKTETA lisingetumika.
Rubaman kulikuwa hakuna sababu ya malafyale kumwambia ndugu rais kuwa anaonesha UDIKTETA wake hapo kamuhukumu moja kwa moja kuwa ni dikteta kitu ambacho sitaki kuamini rais wa TFF bwana Malinzi yupo hivyo sababu kwa kufungua tu ukurasa huu kaonesha jinsi gani anaweza kusikiliza mawazo ya wengine kitu ambacho ni kinyume kabisa na utawala wa kidikteta mimi nadhani tumuulize rais maswali magumu na kumpa solution na yeye awe tayari kusikiliza asiwe mtu mwenye majibu ya kila kitu.
Hakika! Timu ya Taifa ni mkusanyiko wa wachezaji nyota katika vilabu ndani na nje ya nchi, hii falsafa ambayo wamekuja nayo TFF sijui wameipata wapi. Ni vema watuambie ni nchi gani imefanikiwa kwa kutumia falsafa hiyo, kazi ya kukuza vipaji sio ya Chama cha mpira bali vilabu.