Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

kama Bwana Malinzi havunji sheria yeyote basi sioni kama kuna haja ya yeye kuachia uongozi wa KRFA labda tuu iwe kwasababu ya ufanisi na kuachia wengine

Unatakiwa uje sheria si lazima ziwe zimekamilika na ndio maana kuna utaratibu wa kufanya mabadiliko ya sheria mara kwa mara (amendements) sasa hapa ni busara kutumika sababu ata utawala wa kikaburu nchini afrika kusini ulikuwa unafata sheria hivyo basi kuna mazingira sheria inaweza kuwa mbaya na kuna mazingira sheria inaweza kuwa kimya hapo ndipo busara na hekima utumika kuchukua maamuzi sahihi.
 
Kocha mpya wa timu ya Taifa atakuwa Mholanzi Mart Nooij.Aliwahi kuifundisha timu ya vijana ya Burkina Faso,akawapeleka Msumbiji fainali za Afrika na kwa sasa alikuwa anafundisha St George ya Ethiopia.
 
Kama mwenyeji wa Kagera siamini kama hakuna mwenyeji yeyote wa Kagera asiyeweza kuongoza KRFA but Jamal Malinzi pekee. Jinsi Wakagera tunavyopenda kuwa Viongozi hata kwa vitu tusivyovijua ndani na nje lazima patakuwa na mtu mwingine ambaye angeweza kuendesha KRFA kwa ufanisi zaidi ya mtu anayeshikiria nyadhifa mbili kimkoa na kitaifa. Itakuwa jambo la busara kwa Malinzi kuachia uongozi wa mkoa kwa maendeleo ya Kagera na wanamkoa.
 
Mheshimiwa Rais naomba utolee ufafanuzi maswali yangu hapo juu kwani naamini lengo la kupewa nafasi hii ni wewe kujibu maswali yote magumu na mepesi.
 
Angalia amevunja Timu yetu nzuri ta T-Stars na kuanzisha Chekechea yake.Hii ni kurudisha nyuma maendeleo ya Soka.
 
Angalia amevunja Timu yetu nzuri ta T-Stars na kuanzisha Chekechea yake.Hii ni kurudisha nyuma maendeleo ya Soka.

Tutegemee makubwa zaidi ya haya mkuu maana hii sera yake mpya Jamal Malinzi sijui team ya maboreshe HAIJAWAHI KUWEPO sehemu yyt duniani zaidi ya TZ

Mpira ni sera za muda mrefu sio kama hizi za TFF!Hawa vijana wa Tukuyu kabla hawajaenda Tukuyu walikuwa wapi?Walifundishwa na nani?Maneno ya kaka yangu Rukambura kuhusu mategemeo mengi ya watz kuhusu Malinzi naanza kuyakumbuka sasa!

Malinzi ni mbabaishaji tu kama akina Rage enzi zile
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mainzi bora ya Ndolanga!
Hakuna kitu hapo, ni ujinga tu!
 
by Jamal Malinzi;
Malafyale ukitaka niwe najibu hoja zako tumia lugha ya uungwana,who is joking here?

Ona sasa! vitisho vya nn sasa? hivi wewe na mbayuwayu kumbe hamtofautiani Ubongo etiieeee?

Haya tushapigwa 3 tatu sasa na burundi!
 
Jamal Malinzi
Kwa mara ingine unaleta mzaha kwenye maswali muhimu sana!Onyesha japo seriousness kidogo!Waambie hivi KRFA HAUNA KITU UTACHOSHINDWA kuwafanyia KRFA kwa nafasi yako ya U-Rais wa TFF!

Tuache majibu ya kisiasa kwenye issue muhimu kama hizi!JIUZURU haraka maana unaonyesha wazi wazi u dikteta wako!!

Malafyale ukitaka niwe najibu hoja zako tumia lugha ya uungwana,who is joking here?

Jamal Malinzi, hivi katika hiyo comment ya bwana Malafyale kuna lugha gani isiyo ya kiungwana au kukuvunjia heshima?
 
Jamal Malinzi, hivi katika hiyo comment ya bwana Malafyale kuna lugha gani isiyo ya kiungwana au kukuvunjia heshima?
rubaman huyu asikutishe,kashindwa kazi aliyochaguliwa kaanza sasa kuleta sera za ajabu kwenye soka letu!Kuokota wachezaji wa mitaani tusiojua wametoka wapi na waliandaliwa na nani kabla hawajaitwa Stars sio tu ni kichekesho bali kinaonyesha Jamal Malinzi aligombea TFF bila kuwa na sera zozote za kumuongoza!

Kuna siku nilikuwa naongea na kaka Rukambura pale Mwanza alinionya kuwa niache kuweka matumaini kwa Malinzi kwani ni mbambaishaji tu,leo hii naungana na kaka Mtingojela walipokata jina la Malinzi mchakato wa awali TFF!Malinzi ni janga la kitaifa!
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi, hivi katika hiyo comment ya bwana Malafyale kuna lugha gani isiyo ya kiungwana au kukuvunjia heshima?

Rubaman kulikuwa hakuna sababu ya malafyale kumwambia ndugu rais kuwa anaonesha UDIKTETA wake hapo kamuhukumu moja kwa moja kuwa ni dikteta kitu ambacho sitaki kuamini rais wa TFF bwana Malinzi yupo hivyo sababu kwa kufungua tu ukurasa huu kaonesha jinsi gani anaweza kusikiliza mawazo ya wengine kitu ambacho ni kinyume kabisa na utawala wa kidikteta mimi nadhani tumuulize rais maswali magumu na kumpa solution na yeye awe tayari kusikiliza asiwe mtu mwenye majibu ya kila kitu.
 
Kocha mpya wa timu ya Taifa atakuwa Mholanzi Mart Nooij.Aliwahi kuifundisha timu ya vijana ya Burkina Faso,akawapeleka Msumbiji fainali za Afrika na kwa sasa alikuwa anafundisha St George ya Ethiopia.

Ndugu Rais kocha tumemuona lakini naomba sana twende taratibu na hiyo timu ya maboresho kocha aachwe afanye uchaguzi wa timu yake sababu huu mpango wa maboresho sio wakwake ni wa TFF.

Pili ndugu rais hakuna kitu kimenihuzunisha kama kuona timu yetu ya taifa inavaa jezi za hovyo kabisa zile za ADIDAS hvi kweli timu ya taifa ni ya kufanyiwa majaribio ya jezi na majaribio yenyewe jezi ndio zile? we are not serious ndugu rais? nakuomba uwaambie hao adidas watengeneze haraka jezi zenye ubora na zenye rangi ya nchi yetu hivi kweli TAIFA STARS inataka kurudi enzi za kuvaa jezi za hovyo na tulikuwa tunaenda vizuri kwa upande wa ubora na rangi za jezi ndugu rais hili litawavunja moyo watu wengi na soon ata ule uzalendo wa kuvaa jezi za timu ya taifa utatoweka nani avae zile jezi za hivyo zisizo na mvuto.
 
Jamal E. Malinzi ni rais wa TFF na pia ni mwenyekiti wa chama cha mpira cha mkoa wa Kagera (KRFA). Nakumbuka Azimio la Arusha lilikuwa linakataza mtu mmoja kutumikia vyeo zaidi ya kimoja. Yameisha anza kujitokeza malalamiko kuwa mheshimiwa rais wetu wa TFF anampango wa kukiwekea manyasi bandia uwanja wa Kaitaba licha ya ahadi iliyotolewa na rais aliyetangulia ya kuuwekea nyasi hizo hizo uwanja wa Nyamagana.
Ushauri wangu ni kwako kaka Malinzi kuchukua uamuzi mgumu wa kuachia nafasi hiyo ya kuwa mwenyekiti wa KRFA ili utekeleze majukumu ya TFF kwa ufasaha zaidi bila ya kuwa na manung'uniko ya kupendelea hasa mkoa wa Kagera.
 
Kaka Jamal; hoja yangu kwako kwa sasa ni ndogo sana.

timu ya Taifa isiwe mahali pa kukuzia vipaji.
Kila timu ya Premier League (ya Tanzania) si inayo timu ya vijana?

Tena bado kuna timu za vijana za Taifa?

Timu ya taifa inafaa iwe ni mkusanyiko wa wachezaji waliofanya vizuri kutoka katika timu zao.
Kujaza machipukizi taifa kutachelewesha sana mafanikio.🙂
Kocha mpya wa timu ya Taifa atakuwa Mholanzi Mart Nooij.Aliwahi kuifundisha timu ya vijana ya Burkina Faso,akawapeleka Msumbiji fainali za Afrika na kwa sasa alikuwa anafundisha St George ya Ethiopia.
 
Ligi inaelekea ukingoni,ili kuongeza ushindani msimu ujao wadau na wapenzi wa mpira mnaonaje tukiipanua ikawa ya timu 16 badala ya 14 za sasa?

President, kuingeza timu VPL suafiki, labda kama mtaweka namna ya kuzidhiti timu za Taasisi moja kama Polisi na JKT zisiongezwe VPL.
 
Kaka Jamal; hoja yangu kwako kwa sasa ni ndogo sana.

timu ya Taifa isiwe mahali pa kukuzia vipaji.
Kila timu ya Premier League (ya Tanzania) si inayo timu ya vijana?

Tena bado kuna timu za vijana za Taifa?

Timu ya taifa inafaa iwe ni mkusanyiko wa wachezaji waliofanya vizuri kutoka katika timu zao.
Kujaza machipukizi taifa kutachelewesha sana mafanikio.🙂

Hakika! Timu ya Taifa ni mkusanyiko wa wachezaji nyota katika vilabu ndani na nje ya nchi, hii falsafa ambayo wamekuja nayo TFF sijui wameipata wapi. Ni vema watuambie ni nchi gani imefanikiwa kwa kutumia falsafa hiyo, kazi ya kukuza vipaji sio ya Chama cha mpira bali vilabu.
 
Rubaman kulikuwa hakuna sababu ya malafyale kumwambia ndugu rais kuwa anaonesha UDIKTETA wake hapo kamuhukumu moja kwa moja kuwa ni dikteta kitu ambacho sitaki kuamini rais wa TFF bwana Malinzi yupo hivyo sababu kwa kufungua tu ukurasa huu kaonesha jinsi gani anaweza kusikiliza mawazo ya wengine kitu ambacho ni kinyume kabisa na utawala wa kidikteta mimi nadhani tumuulize rais maswali magumu na kumpa solution na yeye awe tayari kusikiliza asiwe mtu mwenye majibu ya kila kitu.

Kwa hiyo kumpa mtu negative assessments ni kumnjia heshima? Je angemwambia yeye ni kiongozi bora si ingekuwa ni kumhukumu(positively) kutokana na staili ya uongozi wake? Ni vizuri kwa Malinzi kufungua ukurasa huu kusikiliza mawazo ya watanzania wapendao soka vile vile awe tayari kusikia negative na positive comments, constructive criticisms, assessments za kila mtu. It's the price to be on the spotlight. Viongozi wa kibongo huwa wanapenda kusifiwa kila siku, aki criticiziwa anakuja juu. Huu sio ukomavu wa uongozi. Bwana Malafyale alichosema kimetokana na Rais wa TFF kung'ang'ania madaraka ya kimkoa na kitaifa kama isingekuwa hivyo naamini neno la UDIKTETA lisingetumika.
 
watu hawajui Kama ukiweza kuchukua ulilokosolewa ukalifanyia kazi ni jambo Zuri? Na hili ndio watu wetu wengi wakikosolewa kwa kusaidiwa wafanye kitu gani wao wanaona Kama wanachukiwa si kweli na neno Dikteta si baya linakuja vibaya Kama unachofanya ni kibaya na ukiambiwa rekebisha hivi mtu hutaki kusikiliza mtu anakupa wazo uweke sawa , kwajili sio yake yeye peke yake anataka ubadilike kuweka mambo sawa kwa wanadamu wengi sasa ukitoka kurizisha kigroup tu chako mtu peke yenu itafika siku hata hicho kigroup Chenu mnachopeana Nguvu nini cha kufanya kitavunjika kirahisi wote mtakosa bora asikilize wengi aweke sawa ataweza kuendelea kwa amani.
 
Rubaman kulikuwa hakuna sababu ya malafyale kumwambia ndugu rais kuwa anaonesha UDIKTETA wake hapo kamuhukumu moja kwa moja kuwa ni dikteta kitu ambacho sitaki kuamini rais wa TFF bwana Malinzi yupo hivyo sababu kwa kufungua tu ukurasa huu kaonesha jinsi gani anaweza kusikiliza mawazo ya wengine kitu ambacho ni kinyume kabisa na utawala wa kidikteta mimi nadhani tumuulize rais maswali magumu na kumpa solution na yeye awe tayari kusikiliza asiwe mtu mwenye majibu ya kila kitu.

Kuwa Rais wa TFF na kuendelea kuwa Mwenyekiti wa KRFA ni udikteta wa hali ya juu mno wenye dhana kuwa ni yy tu mwenye uwezo wa kuongoza KRFA
MKALIKENYA mm na ww tukisimama imara tunaweza muondoa Jamal Malinzi KRFA!
 
Last edited by a moderator:
Hakika! Timu ya Taifa ni mkusanyiko wa wachezaji nyota katika vilabu ndani na nje ya nchi, hii falsafa ambayo wamekuja nayo TFF sijui wameipata wapi. Ni vema watuambie ni nchi gani imefanikiwa kwa kutumia falsafa hiyo, kazi ya kukuza vipaji sio ya Chama cha mpira bali vilabu.

Sera hii ya Jamal Malinzi na wenzake akina Mayanga HAIJAWAHI kuwepo duniani na inaanzia TZ!Sijapata ona popote duniani nchi ikaendelea kisoka bila kuwekeza!Kama issue ni vijana kuna vijana wengi wanacheza soka la hali juu league zetu!Hawa wa mitaani wameandaliwa lini,wapi na nani?
Tunacheza na Zimbabwe kufuzu mataifa huru baadae mwezi ujao tutegemee kipigo kikali!
Malinzi kashindwa kazi akae miaka yake 4 aondoke!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom